Nahitaji ushauri juu ya ndoa hii niliyokuwa msimamizi

Nahitaji ushauri juu ya ndoa hii niliyokuwa msimamizi

Asante kwa ushauri ingawa mama mwenyewe yaani ukimwambia uwe mpole du kwa hali ilipofikia ni hatari.Mimi nilikuwa nimeshagota nikamwambia atafute washauri nasaha waingilie kati maana du inachanganya sana

Mkuu huyo BB harusi hawezi kuwa mPOLE sababu inavyoonekana alimuamini sna jamaa so anajihis km alikuwa ----- ingawa baadae atatulia
 
Mpenz Remote hebu njoo hapa.kwanza uone shughuli hii
 
Last edited by a moderator:
Kosa la kwanza kumruhusu mume kwenda moro, la pili kuruhusu awe na housegirl. Hapo ndo mwanamke alipaswa kuexercise power zake, yeye katulia. Hakuna namna ingine ya kuinusuru zaidi ya mume kuchagua either familia au kazi. Fullstop
 
Mkuu @
bornagain kwa mtazamo wangu Mapenz huwa hayana mshauri,,,,!! Yaani hata msemeje wenyewe wacpokubalina hakuna NDOA ninachofahamu nakm naww ulivyosema Wacmamiz ndio watu wa kwanza kujua matatizo ya NDOA hucka mimi nimecmamia Harusi nyingi na ninyingi pia nimezikataa sababu baadhi yao wameshindwa kujibu maswali yangu mojawapo likiwa kwanini mnataka kuOANA,,,,! huwa napenda kuuliza swali hili nakwakweli lazima nishawishike na majibu yao ndio nakubali kucmamia hiyo Harus na B4 nawapa mashart yangu moja wapo km wamependana wenyewe nwakivurugana nilazima wamalize wenyewe Kwakweli misimamo yangu imenisaidia kucmamia HARUSI nyingi zisizo na Majanga huwa nafanya hv kwasababu kucmamia maHARUSI nizaidi yakuvaa SUTI kanisani unatakiwa muda mwingi ujue maendeleo yao n matatizo.km hayo Yakupasa uwajibike bila kujali muda,,,Ushauri wangu kwako Mkuu kwanza uckate tamaa,then mFACE B B harusi peke yake mckilize mawazoo yake atapike yote kwako then mwambie utamtafuta cku nyingine kisha Funga safari hadi Moro,ongea na Jamaa hii inatakiwa uwe Serious hata km jama ni mshakaji wako unapoongea nae issue hii akuone tofauti na alivyokuzoea nayee mckilize atapike yote kwakokisha Mwambie utarudi tena kisha kutana na MKEO mwaga yote uliyopata kwa mke wa jamaa na mume mwenyewe shaurianeni na mkeo Kisha ombeni kukutana nao wote wawili tena iwe MORO,, mwambie jama km utaenda Moro bt ucmwambie km utaenda na YF wa jamaa km mnajiweza chukueni Hotel nzuri wewe na MKE wako nahuyo B harusi then mwambie jamaa aje HOTELIN mfanyie Surplise then wakutanishe na mke wake kisha Mzee unafunguka kutokana nayale uliyoyackia kwakila mmoja Lkn ktk yote waambieni wao ndo wenye uamuzi wakuinusuru NDOA pia mkuu wewe na MKEO epukeni kuwa na Upande kwa maana yakumtetea mmoja wapo,,,Alie kosea mmwambie LIVE natena ongeeni.km watu mlio na mamlaka dhidi yao ingawa ni watu wazima,,,,,,,! Kila la heri mkuu,,,!
 
Tunatofautiana aisee..my hubby amekaa na hg mwaka karibu wa nne huu...na wala sina pressure...kama mumeo anajiheshimu it doesn't matter anakaa na hg, hboy au peke yake...
Imagine huko mbali afu eti unatafuta house boy kukaa na familia kisa unaogopa mumeo kitombi...what about your kids...hujasikia story za wanachowafanyia watoto

I am about to go bck home for good...na mume wangu hajawahi kumpa mimba hg...and my assumption hajawahi kutembea na hg...

si kila mwanaume ni fisi kuwa hawezi kaa na mfupa karibu...

Kuna wanaume nawajua mabachela na wanakaa na ma house girl kwa heshima zote...hata kama ni uzinzi lazima ufanye zero grazing?

Huyu mwanaume hata kama si house girl angeoa muuza bar...tabia haina dawa...

Hilo nalo neno maana kuna matukio siku hizi ya ubakaji especially house boy akiwa karibu na watoto ambao nao wanamkubali kaka yao wa hiari, huyo jamaa nae ni kitombi tu maana Dar na Moro mbona karibu ukizingatia ndoa ni changa, kabla ya kufanya conclusion ya sijui ushirikina umetumika labda mleta uzi angetupa background ya jamaa kuhusu warembo kabla ya kuoa alikuaje. Kuna mambo mengi sana yapo nyuma ya pazia kwenye huu uzi maana panapotokea tatizo wahusika huwa hawapo wazi ku-share kila kitu ili iwe rahisi kwa washauri kufanya cause and effect analysis.

Tabia yake ya awali kabla ya ndoa ndio inaweza kutoa jibu kama jamaa karogwa au shetani amempitia kama tunavyomsingizia siku zote, maana tulishaona wanaume wenzetu hata kabla ya kuoa walikuwa ni wanyonge mbele ya girl friend wao ajabu akioa akawa mnyonge kwa mkewe tunasema karogwa kumbe ana history ya uzoba
 
duh inauma..hata mama yangu ilimtokea kasafiri kurudi dingi kamtia mimba hausgel..na hadi leo mke mwenzie na watoto kedekede
 
That's the point...ukishaanza kukosa amani na house girl..sijui wadogo zako...jua ulizembea kwenye kuchagua mume...
Ndoa ni kuaminiana na kuheshimiana...
Kumshuku mumeo tu kuwa ana affair na housegirl ni dharau ya hali ya juu...
Na mara nyingi hao so called smart wa kuchunga wana sababu za kufanya hivyo...wanajua walipojiingiza in the name of ndoa...

Mi nimeshakaa na ma house girl wenye mvuto haswa ...maana sitishiki na uzuri wa mtu kwani kwangu house girl ni part ya familia...na sijawai kupata tatizo na mume wangu...kuna mmoja alikuwa anatokea Singida...she was very beautiful na alikuwa hajatulia...lakini hakuwa anacheza ndani maana tulikuwa tunaishi nae kama ndugu...


Sometimes ma house girl wanajilengesha kwa wanaume sababu wanakusoma unavyomuona mtu nusu; manyanyaso kibao...oooh usikae sebuleni...oooh usiangalie TVooooh usivae nguo hiyo...angekuwa mwanao ungemyanyapaa hivo...na anataka akutie adabu...

Hivi unafikiri ukianza kuweka masharti ndani house girl ni mjinga...anakuwa anajua fika we have an animal in this house (your husband) kwa maneno mengine unamwambia huyu mume wangu kitombi stay away...na hapo ndio anajua what to do next akiingiwa na roho ya ushindani...na at the same time unamdhalilisha mumeo kuonyesha kuwa hana uwezo wa kufunga zipu...

Yani kuna wanawake wanakiri wazi kuwa hawana amani hata kuwaacha binti zao na baba zao...kweli???? bado huyu ni mumeo???? eti watawabaka watoto wa kuwazaa wenyewe...kazi ipo...


shemeji yangu anafanya kazi mbeya, ana housegirl. Huku dar mke ana housegirl na houseboy. wanawasiliana kwa simu na kutembeleana mara 2 kwa mwezi huku baba akiendelea na juhudi za kurudi dar. kwamba anazini na housegirl huko mbeya au mwanamke mwingine hakuna ajuaye ni siri ya moyo wake. kikubwa ni kuwa yeye na mkewe wanaaminiana. tuache kubebesha wanawake mzigo waume zao wanaposhindwa kujidhibiti na kujiheshimu. unadhani huyu baba asingeenda moro asingeweza kuzini na housegirl chini ya pua ya mkewe? na unafikiri kuweka houseboy utapunguza uwezekano wa mume bazazi kuzini? ni kuomba tu neema ya mungu maana kuna watu wakiwa ndani ni waume, wakiwa nje ni mabasha. utamchunga mume na housegirl utaweza? ukiugua ukalazwa housegirl unaenda nae hospitali au unamrudisha kwao mpaka upone? ukienda kazini unaenda nae? ukiwa usingizini mumeo unamfunga pingu kwenye mkono wako ili usiku asinyate kwenda kwa housegirl?
 
Mkuu @
bornagain kwa mtazamo wangu Mapenz huwa hayana mshauri,,,,!! Yaani hata msemeje wenyewe wacpokubalina hakuna NDOA ninachofahamu nakm naww ulivyosema Wacmamiz ndio watu wa kwanza kujua matatizo ya NDOA hucka mimi nimecmamia Harusi nyingi na ninyingi pia nimezikataa sababu baadhi yao wameshindwa kujibu maswali yangu mojawapo likiwa kwanini mnataka kuOANA,,,,! huwa napenda kuuliza swali hili nakwakweli lazima nishawishike na majibu yao ndio nakubali kucmamia hiyo Harus na B4 nawapa mashart yangu moja wapo km wamependana wenyewe nwakivurugana nilazima wamalize wenyewe Kwakweli misimamo yangu imenisaidia kucmamia HARUSI nyingi zisizo na Majanga huwa nafanya hv kwasababu kucmamia maHARUSI nizaidi yakuvaa SUTI kanisani unatakiwa muda mwingi ujue maendeleo yao n matatizo.km hayo Yakupasa uwajibike bila kujali muda,,,Ushauri wangu kwako Mkuu kwanza uckate tamaa,then mFACE B B harusi peke yake mckilize mawazoo yake atapike yote kwako then mwambie utamtafuta cku nyingine kisha Funga safari hadi Moro,ongea na Jamaa hii inatakiwa uwe Serious hata km jama ni mshakaji wako unapoongea nae issue hii akuone tofauti na alivyokuzoea nayee mckilize atapike yote kwakokisha Mwambie utarudi tena kisha kutana na MKEO mwaga yote uliyopata kwa mke wa jamaa na mume mwenyewe shaurianeni na mkeo Kisha ombeni kukutana nao wote wawili tena iwe MORO,, mwambie jama km utaenda Moro bt ucmwambie km utaenda na YF wa jamaa km mnajiweza chukueni Hotel nzuri wewe na MKE wako nahuyo B harusi then mwambie jamaa aje HOTELIN mfanyie Surplise then wakutanishe na mke wake kisha Mzee unafunguka kutokana nayale uliyoyackia kwakila mmoja Lkn ktk yote waambieni wao ndo wenye uamuzi wakuinusuru NDOA pia mkuu wewe na MKEO epukeni kuwa na Upande kwa maana yakumtetea mmoja wapo,,,Alie kosea mmwambie LIVE natena ongeeni.km watu mlio na mamlaka dhidi yao ingawa ni watu wazima,,,,,,,! Kila la heri mkuu,,,!

Mtoa mada ifikilie hii na uifanyie kazi.
 
unashauri kitu ambacho hata wewe unaweza kukifanya? Unawezaje kumshauri mke amkaribishe vyema mumewe ahakikishe anapata na mtoto haraka? VVU je? Labda VVU tuache pembeni. Anabebaje hiyo mimba na stress? Analeaje huyo mtoto na baba aliye na makao kwa mpogolo moro? ingekuwa mimi ningefanya moja kati ya haya mawili: kutaliki /kutengana au kusamehe kutakakoambatana na masharti.

NANDERA;
Si kwamba siwezi kufanya, naweza na ndivyo ilitakiwa tufanye. Kuanza kupambana na mumewe ni kuonesha alivyo dhaifu. Kama kweli alimpenda mume wake, aliruhusuje, huyo mume aende Moro peke yake? Aliruhusuje huyo mume awe na H/girl?? Alidhani kazi ya H/girl ni kufua na kudeki tu??
Mbona na yeye pale pale mwanzoni hakuomba kuwa na H/boy wa kulinda lindo la usiku asije vamiwa na majambawazi yanayo msumbua Kamanda Kova?
Kalikoroga mwenyewe, sasa atulie tuli, ambembeleze huyo mume. AAche kelele, hakuna VVU tena kwani mechi zilikuwa zikichezwa live bila chenga(Mipira ya kinga). Leo uje kuogopa VVU kwa sababu umesikia kaoa??
Ambembeleze mumewe, wala asiende kwa wakwe. Mkwe hajamuoa. Walioana wawili, wamalize wawili. Hata Baba Paroko hana nafasi hapo teena.
 
Mpenz Remote hebu njoo hapa.kwanza uone shughuli hii

huyo jamaa katekwa na mtoto wa kipogolo yeye cha kufanya abgeendelea kula huo mzigo house girl ila weekend lazima aende kwa wife wake.
 
Last edited by a moderator:
awachukue wote wawe wake zake... cha muhimu bi dada apunguze wivu.. akubali kuwa mke mkubwa mwenzie mke mdogo.
 
Mimi najua kuwa
kusimamia harusi ni shughuli siyo ile ya ukumbini bali shughuli yake ni
siku mambo ya hao wapendanao yanapoenda kombo maana najua wasimamizi
ndiyo wanakuwa watu wa mwanzo kuelezewa kinachojiri.

Sasa kuna ndoa nimesimamia miaka miwili iliyopita yaani bwana bibi
harusi na bwana harusi walipendana zaidi ya wale ndugu wa kwenye movie
ya Romeo na Julieth yaani kila dakika baby umekula, baby unafanya nini
sasa hivi yaani ni shida kama hujawahipita huko basi utadhani wapo
peponi.

Kisa chenyewe kilianza mwezi wa kwanza mwaka huu, mwanaume alipata kazi
mpya Morogoro na bi dada yeye anapiga mzigo hapa Dar.

Walikuja home kutuomba ushauri kwamba wafanyeje, mimi nikafunguka
kisawasawa nikawaambia kuwa Morogoro wanaweza wakapaona ni karibu sana
na Dar ila issue ya distance relationship siiungi mkono hata kidogo.

Nikashauri jamaa akomae hapahapa mjini atapata kazi nyingine tu nzuri
maana familia bado changa. Ebwana kwa kuwa bado wapo mahabani bi dada
akasema yeye hana shida Moro si mbali sana yupo radhi jamaa aende Moro
akapige mzigo ila kwa sharti kwamba kila Ijumaa jioni mpaka Jtatu
asubuhi ama Jumapili jioni ahakikishe anarudi nyumbani.

Kweli jamaa akahamia Moro na kufika Moro akatafuta house girl wa
Kipogolo.To cut the story short ni kwamba jamaa sasa si weekend wala
nini haji nyumbani tena ni kwamba ameoa house girl wake huyo na sasa ana
house girl mwingine kumsaidia yule wa house girl wa mwanzo maana
amekuwa mother house.

Sasa bwana bibi harusi amerudi nyumbani kuniomba ninusuru ndoa yake,
nimewasiliana na jamaa Moro akakubali kuwa kweli amemuweka ndani house
girl wake na akaniambia kuwa hana shida na mama watoto Dar maana na yeye
ni mke wake na hakuna kitakachopungua.

In short watu wazima wenye ushauri wa kunisaidia kunusuru ndoa hii
naombeni msaada wenu maana akili yangu imegota.

This is serious kabisa wala sitanii naombeni mwenye ushauri wa nini
kifanyike anisaidie

mkuu h/g wa kwanza ana mimba? jibu. sasa subir na h/g wa pili atamlala usisahau kutuletea majibu
 
NANDERA;
Si kwamba siwezi kufanya, naweza na ndivyo ilitakiwa tufanye. Kuanza kupambana na mumewe ni kuonesha alivyo dhaifu. Kama kweli alimpenda mume wake, aliruhusuje, huyo mume aende Moro peke yake? Aliruhusuje huyo mume awe na H/girl?? Alidhani kazi ya H/girl ni kufua na kudeki tu??
Mbona na yeye pale pale mwanzoni hakuomba kuwa na H/boy wa kulinda lindo la usiku asije vamiwa na majambawazi yanayo msumbua Kamanda Kova?
Kalikoroga mwenyewe, sasa atulie tuli, ambembeleze huyo mume. AAche kelele, hakuna VVU tena kwani mechi zilikuwa zikichezwa live bila chenga(Mipira ya kinga). Leo uje kuogopa VVU kwa sababu umesikia kaoa??
Ambembeleze mumewe, wala asiende kwa wakwe. Mkwe hajamuoa. Walioana wawili, wamalize wawili. Hata Baba Paroko hana nafasi hapo teena.

sawa mama. mawazo yako nayaheshimu kwa sababu ndivyo yanavyofanya kazi kwenye ulimwengu wako na wengine wenye mtazamo kama wako. Mimi mume akisaliti ndoa kupambana nae si udhaifu, bali ni udhaifu kupambana na wanawake wenzio. Utapambana na wangapi, mpaka lini? Kwamba mumeo ni robot halina akili hawa wanawake ndo wenye akili wameli-manipulate? Kuna "mume" hapa kasema alipogundua housegirl wake anamtega alimfukuza. Kumlaumu dada wa watu kwamba kwa nini hakwenda na mumewe moro kama anampenda ni kumhukumu bila kujua mazingira. Familia zinatengana kwa sababu nyingi zilizo nje ya uwezo wao. Kwa vyovyote vile sidhani kama maisha ya moro na dar walipanga yawe ya kudumu. Na ukisema hivi unamaanisha wanaume wakiishi nyumba moja na wake zao hawawezi kuzini na wasichana wa kazi.

Kusema ambembeleze mumewe nayo sijailelewa vizuri. Kwamba "baba nanii nisamehe mume wangu mimi ndo nimekukosea....najua shetani alikupitia....najua huyo msichana kakuloga si bure....tafadhali rudi mume wangu.."!!!!!!?? Anyway, labda ndo hekma zenyewe, mimi sijui. Pia sioni ubaya huyu mke akiamua kushirikisha wakwe na paroko. hawa wote wana nafasi ya kulinda hii ndoa maana wote walichangia kuifanya iwepo. ndoa ni ya wawili mkiwa na maelewano. Mkikorofishana hata serikali itahusika.
 
Ingekuwa vema kama wazaz wangefahamishwa jambo hili huenda wana chochote cha kushauri hapo
 
Jibu ni rahisi kabisa. Huyo mume aambiwe amfukuze huyo House girl haraka sana then usuluhishi na mke wake halali ndio ufuate. Tofauti na hapo mke akubali matokeo haya, ama avunje ndoa(watengane) au akubali uke mwenza(ndoa ya wake wengi) au yapelekwe kwa wazee(wakwe na viongozi wa Dini). Tatizo sio Moro wala House girl bali ni tamaa za mwanaume. Hatua zifanyike haraka sana kabla house girl hajazalishwa mtoto. Maana akizalishwa tu issue itakuwa ngumu zaidi, maana House girl ataanza naye kudai haki za kifamilia na kindoa.
 
Wote kwa ujumla nimependa michango yenu ya dhati, hata kama sitaweza kuleta mwafaka kwenye ndoa hii ila kusema ukweli nimepata mwanga sana tena sana.In short nimepata pa kuanzia na kama si pa kumalizia.Kila kitu hapa kimekuwa very clear kwa hiyo nawashukuru sana.Shukrani za dhati kabisa ziwaendee wote waliotoa mawazo yao na zaidi kabisa kwa mheshimiwa dolevaby, NANDERA, nyumba kubwa dada yangu upo vizuri sana una confidence asilimia 100% pia dada christine ibrahim upo vizuri unisaidie katika maombi yako maana inaonekana upo vizuri kwenye kupiga goti Heaven Sent na MankaM mpo vizuri nyie mnatumia formula ya zero grazing safi sana, Mamndenyi nilikuwa nakuaminia lakini hii ya leo kidogo na wewe imekuchanganya sana kama ilivonichanganya mimi
 
Nakushauri fanya hivi, week end moja wewe, huyu aliyekua bibi harusi pamoja na wife wako mwende wote Morogoro hadi nyumbani kwa jamaa tena bila kumtaarifu then na huyu bi mdogo aelezwe nini kilicho waleta from there then mnaweza kuanza mazungumzo.

Hilo moja, la pili ni hili, before huja wasimamia, uliwapa semina elekezi? Unajua wapogoro wanavyojua kukimudu KITANDA kaka!
 
Back
Top Bottom