Nahitaji ushauri juu ya ndoa hii niliyokuwa msimamizi

Nahitaji ushauri juu ya ndoa hii niliyokuwa msimamizi

Ndugu yangu ni kwamba hakuna ndoa iliyofungwa kati ya huyo bwana na house girl wake, ila wanaishi kiunyumba na jamaa ukimuuliza anakiri kuwa amemuoa yule house girl ingawa hakuna ndoa ya mahakamani wala ya kanisani,so wazazi na sisi mashuhuda tunafahamu ndoa ya mke aliebakia Dar huyo wa Moro japo bwana anamkiri kuwa yupo nae ni mvurugaji tu,kwa hiyo toa ushauri namna ya kumsaidia mama alieko Dar maana hali ni mbaya

anhaaa!!! sasa ni hivi huwez jua kilitokea nn kwa huyo housegirl mpaka akaamua kuropoka wazi...!!!!
kwani walijenga nyumba na wamefanikiwa mtoto hata mmoja!!!!?
 
Kwa uhalisia huyo baba hajafunga ndoa kwa kua tu hakuna dhehebu lolote la kikristo linalokubali wake zaid ya mmoja kama waislam hiv ndoa yao n batili

Ni kweli hajafunga ndoa na wala hakuna padri atakaekubali kuifunga hiyo ndoa, ila sasa awe amefunga ndoa ama hajafunga ndoa jua kuwa anakaa na mwanamke ndani na anamuacknowledge wala hamkani.Na kumbuka hata kama hajafunga ndoa ila mke wake nyumbani anaumia.Sasa leta ushauri kama ni wewe unaweza ukamshauri nini mama alieko Dar?
 
anhaaa!!! sasa ni hivi huwez jua kilitokea nn kwa huyo housegirl mpaka akaamua kuropoka wazi...!!!!
kwani walijenga nyumba na wamefanikiwa mtoto hata mmoja!!!!?
Wana mtoto mmoja na pia tayari walikuwa wameshaanza mchakato wa kujega maana tayari nyumba ipo kwenye msingi namaanisha kwamba wameshafunga mkanda kwenye msingi kwa hiyo bado kuanza kupandisha tofali tu
 
tatizo dogo sana hilo ampigie simu amwambie anampa mwisho weekend hii awe amefika kuzungumzia suala hilo akishindwa basi atamkuta mtoto wake kwa wazazi wake na sehemu waliyojenga anauza na asije akamtafuta kwani atakuwa ni mke wa bwana mwingine tena!!!!
na ahakikishe kama hakuja hampigii simu wala chochote auchune kimya bila kikomo na akipigiwa simu akate na azime........ afanye hivyo!!!!
sisi wanaume tunafika kipindi tunaumiza kichwa, kitakachotokea uje kutuarifu hapa!!!
 
Kwanza, huyo mheshimiwa hana ndoa na house girl wa Moro, wanaishi tu kama mume na mke lakini hawatambuliki kisheria coz ndoa ya kikristo ni ya mume na mke mmoja.
Pili, Kwa sababu huyo bwana ameshakuambia ukweli kuhusu huyo binti anayeishi naye kinyumb, unachotakiwa kufanya ni kumwita aje Dar ili ufanye mazungumzo pamoja na mke wake. Hapo ndio utapata mwanga halisi wa mustakabali wa ndoa yao.
Hadi ukifikia hatua hiyo ya kusuluhisha na kuona hamna mafanikio, unaweza kuhusisha wazee au familia zote mbili ili wakae na kumuonya huyo jamaa.
 
Mimi najua kuwa kusimamia harusi ni shughuli siyo ile ya ukumbini bali shughuli yake ni siku mambo ya hao wapendanao yanapoenda kombo maana najua wasimamizi ndiyo wanakuwa watu wa mwanzo kuelezewa kinachojiri.

Sasa kuna ndoa nimesimamia miaka miwili iliyopita yaani bwana bibi harusi na bwana harusi walipendana zaidi ya wale ndugu wa kwenye movie ya Romeo na Julieth yaani kila dakika baby umekula, baby unafanya nini sasa hivi yaani ni shida kama hujawahipita huko basi utadhani wapo peponi.

Kisa chenyewe kilianza mwezi wa kwanza mwaka huu, mwanaume alipata kazi mpya Morogoro na bi dada yeye anapiga mzigo hapa Dar.

Walikuja home kutuomba ushauri kwamba wafanyeje, mimi nikafunguka kisawasawa nikawaambia kuwa Morogoro wanaweza wakapaona ni karibu sana na Dar ila issue ya distance relationship siiungi mkono hata kidogo.

Nikashauri jamaa akomae hapahapa mjini atapata kazi nyingine tu nzuri maana familia bado changa. Ebwana kwa kuwa bado wapo mahabani bi dada akasema yeye hana shida Moro si mbali sana yupo radhi jamaa aende Moro akapige mzigo ila kwa sharti kwamba kila Ijumaa jioni mpaka Jtatu asubuhi ama Jumapili jioni ahakikishe anarudi nyumbani.

Kweli jamaa akahamia Moro na kufika Moro akatafuta house girl wa Kipogolo.To cut the story short ni kwamba jamaa sasa si weekend wala nini haji nyumbani tena ni kwamba ameoa house girl wake huyo na sasa ana house girl mwingine kumsaidia yule wa house girl wa mwanzo maana amekuwa mother house.

Sasa bwana bibi harusi amerudi nyumbani kuniomba ninusuru ndoa yake, nimewasiliana na jamaa Moro akakubali kuwa kweli amemuweka ndani house girl wake na akaniambia kuwa hana shida na mama watoto Dar maana na yeye ni mke wake na hakuna kitakachopungua.

In short watu wazima wenye ushauri wa kunisaidia kunusuru ndoa hii naombeni msaada wenu maana akili yangu imegota.

This is serious kabisa wala sitanii naombeni mwenye ushauri wa nini kifanyike anisaidie

Bornagain kama kweli wewe ni born again nenda na Neno badala ya maneno yako, itakuwa rahisi sana
 
Ni kweli hajafunga ndoa na wala hakuna padri atakaekubali kuifunga hiyo ndoa, ila sasa awe amefunga ndoa ama hajafunga ndoa jua kuwa anakaa na mwanamke ndani na anamuacknowledge wala hamkani.Na kumbuka hata kama hajafunga ndoa ila mke wake nyumbani anaumia.Sasa leta ushauri kama ni wewe unaweza ukamshauri nini mama alieko Dar?

Wazazi wanahusika kushaur zaid pande zote mbili
 
Imebidi nicheke tu. Watu wana utani na ndoa jamani, hivi naanzaje kumruhusu mume wangu akae na housegirl tu?? Hapo napo utamlaumu mtu kwa kukucheat au utasema shetani alimpitia? Mwe mwe mwe

Hahahaaaa mume akae na hausi gelo ndani ni utata mtupu jaman mambo ya kujitakia haya
 
tatizo dogo sana hilo ampigie simu amwambie anampa mwisho weekend hii awe amefika kuzungumzia suala hilo akishindwa basi atamkuta mtoto wake kwa wazazi wake na sehemu waliyojenga anauza na asije akamtafuta kwani atakuwa ni mke wa bwana mwingine tena!!!!
na ahakikishe kama hakuja hampigii simu wala chochote auchune kimya bila kikomo na akipigiwa simu akate na azime........ afanye hivyo!!!!
sisi wanaume tunafika kipindi tunaumiza kichwa, kitakachotokea uje kutuarifu hapa!!!

mmmhh sio rahisi kama uwazavyo ndugu
 
Hahahaaaa mume akae na hausi gelo ndani ni utata mtupu jaman mambo ya kujitakia haya

Kwa kweli kuna muda shetani tunamuonea eti. Yani tunamtega tu ili tupate sababu ya kumsingizia. Huyo housegirl ni mama ake mzazi au dada yake useme kuwa hawatatamaniana? Me mme wangu hatokaa na housegirl peke yake milele
 
hapo house girl kafanya manuva ya kishirikins sio bure........ ni kuitana wote wahusika na kuliongelea nje ndani... huku ndugu waendelee na maombi kumnasua huyo jamaa
 
Mke wa Dar akubali matokeo, ndoa imekwisha hapo
 
Kwanza mke aombe likizo kazini n kuhamishia familia huko Morogoro kwa muda bila kuongea nebo lolote.akisha kaa mumewe ata wiki atajua pa kuanzia ni wapi?pili mtoto kam anyonyi atafutwe ndugu /jamaa wa mume kwa kushirikiana na wazazi wa mume mtoto akaishi moro kwa baba yake akiangaliwa na shangazi na dada.hao wanao ishi na mume wanaondoka siku y pili baada ya ile ya kufika.

mama atakuwa anakwenda morogoro kila mwisho wa wiki.dawa ya moto ni moto bila kelele wala nini.

katikati ya wiki mbinu za kivita muhimu kuibuka moro now and then.ndoa nyingine ni kuipeleka kimkanda mkanda.
 
Mimi sijaona ugumu wowote hapo, hilo jamaa la moro limetawaliwa na pepo la ngono tu. Ndoa ya kikristo hata siku hairuhusu kuoa mwanamke zaidi ya mmoja. Nashauri kumwitia wazee wenye busara nadhani watampatia ushauri mzuri na atarudi kwenye ndoa yake
 
Huyo bwana harusi dini gani???? Halafu mambo ya ndoa yataka wale ambao wapo deep washaingia ndoani watu wazima sio wasimamizi na kama housegal kaolewa kwa dini bas tatizo n moja tu hajampa taarifa mkewe mkubwa bas kama n muislam lakini

Dini kwa andiko hili sioni kama ina nafasi
 
Hivi alianzaje anzaje kuajiri hausigelo????

Imebidi nicheke tu. Watu wana utani na ndoa jamani, hivi naanzaje kumruhusu mume wangu akae na housegirl tu?? Hapo napo utamlaumu mtu kwa kukucheat au utasema shetani alimpitia? Mwe mwe mwe
 
Imebidi nicheke tu. Watu wana utani na ndoa jamani, hivi naanzaje kumruhusu mume wangu akae na housegirl tu?? Hapo napo utamlaumu mtu kwa kukucheat au utasema shetani alimpitia? Mwe mwe mwe

Niliwahi ishi na house girl mmoja ilikuwa taabu tupu. Ukifika jioni akisikia muungurumo wa gari anazima taa zoote na kujificha. Ukiingia tu ndani utasikia aah kaka mdudu huku anakukumbatia. Nilivumilia kama mwezi hivi nikamuondoa bila taarifa.
Since then naishi na house boy, japo kuna changamoto ya kutongoza vitoto vya jirani.
 
Back
Top Bottom