Nahitaji Ushauri hii kwa wanaume wenzangu tu

Usikute hujawahi mtamkia unampenda hata siku moja unasubiri demu ndo akwambie wewe.....jiongeze wewe...Mungu akupe ujasiri wa kuushinda udomo zege

NB: NA WEWE UNA TATIZO LA KUPENDA USIPOPENDEKA
 
Jaribu kuongea naye taratibu mapenzi ni feeling pia usichoke kumfanyia vitu vizuri lakini usimforce utamuudhi na utamkosa jaribu kumuonesha kuwa wewe upo tofauti na mtu mwingine
 
KLM mkuu, hiyo unayosema mbona ni ya line maintenance engineers na hapo bado inategemeana na leseni alizonazo
klm ni shirika la nje na hata kwa ulaya dola 6000 ni ndogo mkuu. hapa dar sidhani kama kuna anayelipa zaidi ya fj na wao pia wako hali mbaya kifedha
 
Jaribu kuongea naye taratibu mapenzi ni feeling pia usichoke kumfanyia vitu vizuri lakini usimforce utamuudhi na utamkosa jaribu kumuonesha kuwa wewe upo tofauti na mtu mwingine
ntajaribu maana naona nilishamuudhi kipindi cha nyuma
 
I wanted to ask the same. Nadhani Jf inabid waanza ku limit age
ndugu yangu kwani cha ajaabu ni nini, unashangaa rubani kuitwa mlalahoi hahahaha labda ni hasira ila nilichoshamaanisha ni hajiwezi kifedha zaidi yangu halafu ni kijana mdogo sana zaidi yangu ambae bado anaishi kwa wazazi na ndo kwanza alikua anaanza kazi sio kama akina sie tuliooshiba makazini teyari
 
My brother, kwanza nianze kwa kusema yaliyokukuta nami yamenikuta mara nyingi zaidi yako. Nina stori zaidi ya 4 za aina kama yako. Nimefanya yote yanayostahili kumfanyia mwanamke lakini niliishia kuwaona wakienda kwa majamaa wengine ambao walikua hawawajali hata punje.

Baada ya kutafakari kwa muda mrefu nilikua nakosea wapi nilikuja na mahitimisho yafuatayo
1. Sikuwa Muwazi wa Hisia Zangu mapema kwa hao mabinti. Sikuwaambia wazi wazi kwamba nawataka bali niliwekeza zaidi ktk kuwaonesha nawajali kwa kiasi gani kwa kupitia matendo yangu jambo lililofanya niishie kuonekana "mtu mwema" tu asie na nia nyingine wakati nilikua naumia moyoni kwa hisia kali za mapenzi.
2. Nilitengeneza sura feki ya mtu mwema kwao kwa sababu niliwapenda na kuwataka sana ktk maisha yangu. Niliwapa kila kitu, Sikuwakosoa. Kwa kifupi I was never myself with them.
3. Sikuonesha Kujiamini na maisha yangu kwa kiasi kikubwa. Kupitia matendo yangu niliwaonesha "nina shida nao" sana kiasi cha kufanya nionekane kama mwanaume nisiejithamini kiasi kilichopelekea wanikimbie japo niliwatreat vizuri.

NAKUSHAURI NINI?
1.Kama binti umempenda na unataka kua nae kimapenzi Baada ya kujuana tu, Mwambie Waziwazi mapema, ili kama hakutaki ujue moja. Majuto ktk mapenzi yanauma zaidi ya Kibuti, Bora aseme hakutaki mapema ili uavoid kupoteza muda wako na hela kuliko kungojea hadi utakapo kata tamaa kwa vioja atakavyokuwa anakuletea.
2.Jiamini. Kua mkweli kwake. Kama hupendi jambo lolote analofanya au tabia yake, mweleze mara moja. Atakuheshimu na kukupenda.
3.Chunga sana matendo yako. Usimwoneshe kama yeye ndio kila kitu kwako, Huo ni mzigo kwake na atakukimbia tu.
4.Usifatilie maisha yake. Wewe kama umegundua ana mtu anaetoka nae nyuma yako achana nae tu. Kaa kimya ishi maisha yako.
5.Mwisho kabisa na hii ni Kidonge kwako, Huyo bibie ashakuona kama Baba yake. Kwa kifupi havutiwi na wewe kimapenzi tena na Mwanamke akishafikia hapo ni vigumu kidogo kubadili mtizamo wake. Hivyo basi achana nae maana hutampata tena na hata ukitumia njia zingine za ushawishi huyo akirudi atakua anajilazimisha kwako tu kitu ambacho sio healthy. Kubali umefanya kosa na songa mbele na maisha yako. Huyo abaki kua ukurasa kwenye kitabu cha maisha yako tu.

LONG BUT WORTH IT
 
klm ni shirika la nje na hata kwa ulaya dola 6000 ni ndogo mkuu. hapa dar sidhani kama kuna anayelipa zaidi ya fj na wao pia wako hali mbaya kifedha
Kaulize vizuri mkuu, ni kweli ni shirika la nje lakini wana base yao hapa tz kwa ajili ya line maintenance na wameajiri wabongo pia... Sikatai hiyo hela kwa ulaya inaweza ikawa ndogo lakin kibongobongo huwezi ukamuita mtu ka huyo mlala hoi
 
Kama unataka ukweli sio unafiki ndio huu, Wewe sio type yake labda kwa umbo (Unene, wembamba, ufupi, au urefu) au muonekano wa rangi ya ngozi yako (mweusi sana au mweupe sana) au hapendi tabia zako kama majivuno au hiyo ya kumchongea jamaa ili waachane. Lakini usinichukie kwa ukweli , kitu kizuri ni kuwa kuna mwanamke mzuri sana pengine kushinda huyo yuko sehemu anakupenda na kukutamani na wewe haujui tu. Mpotezee huyo msichana ili akili yako iwe huru umuone anaekujali na kukupenda.
 
naurdia kukueleza, ni shirika la nje tu. Hata United Nations wana ofisi Tanzania ila sio kampuni ya kitanzanania na hawalipi kw standards za kitanzania. Ila kwa kweli huwezi fananisha muajiriwa na mfanyabiashara. tena kijana mdogo aliyeanza kazi, labda hii ndio ilionipeleka kumuita jamaa mlalahaoi na hasira ya kunipokonya tonge mdomoni dah.
 
Kama unataka ukweli sio unafiki ndio huu, Wewe sio type yake labda kwa umbo (Unene, wembamba, ufupi, au urefu) au muonekano wa rangi ya ngozi yako (mweusi sana au mweupe sana) au hapendi tabia zako kama majivuno au hiyo ya kumchongea jamaa ili waachane. Lakini usinichukie kwa ukweli , kitu kizuri ni kuwa kuna mwanamke mzuri sana pengine kushinda huyo yuko sehemu anakupenda na kukutamani na wewe haujui tu. Mpotezee huyo msichana ili akili yako iwe huru umuone anaekujali na kukupenda.
Asante mkuu umekuwa muwazi sana. inawezekana basi tu hajanipenda jinsi nilivyo
 
My brother, kwanza nianze kwa kusema yaliyokukuta nami yamenikuta mara nyingi zaidi yako. Nina stori zaidi ya 4 za aina kama yako. Nimefanya yote yanayostahili kumfanyia mwanamke lakini niliishia kuwaona wakienda kwa majamaa wengine ambao walikua hawawajali hata punje.

Baada ya kutafakari kwa muda mrefu nilikua nakosea wapi nilikuja na mahitimisho yafuatayo
1. Sikuwa Muwazi wa Hisia Zangu mapema kwa hao mabinti. Sikuwaambia wazi wazi kwamba nawataka bali niliwekeza zaidi ktk kuwaonesha nawajali kwa kiasi gani kwa kupitia matendo yangu jambo lililofanya niishie kuonekana "mtu mwema" tu asie na nia nyingine wakati nilikua naumia moyoni kwa hisia kali za mapenzi.
2. Nilitengeneza sura feki ya mtu mwema kwao kwa sababu niliwapenda na kuwataka sana ktk maisha yangu. Niliwapa kila kitu, Sikuwakosoa. Kwa kifupi I was never myself with them.
3. Sikuonesha Kujiamini na maisha yangu kwa kiasi kikubwa. Kupitia matendo yangu niliwaonesha "nina shida nao" sana kiasi cha kufanya nionekane kama mwanaume nisiejithamini kiasi kilichopelekea wanikimbie japo niliwatreat vizuri.

NAKUSHAURI NINI?
1.Kama binti umempenda na unataka kua nae kimapenzi Baada ya kujuana tu, Mwambie Waziwazi mapema, ili kama hakutaki ujue moja. Majuto ktk mapenzi yanauma zaidi ya Kibuti, Bora aseme hakutaki mapema ili uavoid kupoteza muda wako na hela kuliko kungojea hadi utakapo kata tamaa kwa vioja atakavyokuwa anakuletea.
2.Jiamini. Kua mkweli kwake. Kama hupendi jambo lolote analofanya au tabia yake, mweleze mara moja. Atakuheshimu na kukupenda.
3.Chunga sana matendo yako. Usimwoneshe kama yeye ndio kila kitu kwako, Huo ni mzigo kwake na atakukimbia tu.
4.Usifatilie maisha yake. Wewe kama umegundua ana mtu anaetoka nae nyuma yako achana nae tu. Kaa kimya ishi maisha yako.
5.Mwisho kabisa na hii ni Kidonge kwako, Huyo bibie ashakuona kama Baba yake. Kwa kifupi havutiwi na wewe kimapenzi tena na Mwanamke akishafikia hapo ni vigumu kidogo kubadili mtizamo wake. Hivyo basi achana nae maana hutampata tena na hata ukitumia njia zingine za ushawishi huyo akirudi atakua anajilazimisha kwako tu kitu ambacho sio healthy. Kubali umefanya kosa na songa mbele na maisha yako. Huyo abaki kua ukurasa kwenye kitabu cha maisha yako tu.

LONG BUT WORTH IT
Boss ni maneno magumu kumeza ila kwa hili imenipa mengi ya kufikiria kweli nilimtendea mengi zaidi ya kusema neno moja tu 'nakupenda' unaachaje kumfuatilia unayempenda yaani kila napokaa kitaaa napewa tu stori si unajua washkaji wakishajua umekufa kwa mtu mara utasikia 'demu wako siku izi hadi fellowship kanisani anaenda' na pia naanzaje kuachana nae, akinipigia simu akinitafuta akiwa na shida naanzaje kumpotezea mkuu ni shida ya kubadilishana mawazo
 
Kaka katika maisha jifunze kitu kuwa watu wengine ni bora akaendelea kuwa rafiki yako na si mpenzi au mke wako.na ndio kitu huyo dada anakiona kwako.umeshamjua sana na sasa hivi unaweza kuona mnaweza kuishi vizuri ila siku mkizama tu dimbwini vitu vitabadilika na utadhangaa mambo yatakavyokuwa ndivyo sivyo. Nadhani kumuweka karibu kama rafiki inatosha na kwambe hutokuja kubadili moyo wake. Na kama atarudisha urafiki kwako achana na habari za kufuatilia wanaume anao date nao. Inakupunguzia heshima kwake kaka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom