Kila mtu ana shida a kimapenzi, leo nimeona nielezee za kwangu
Nina rafiki yangu wa kike, rafiki wa mda mrefu nahisi miaka mitano. Tumekuwa marafiki sana ila nimetokea kumpenda bila ye kujua. Nimekuwa rafiki yake muda mrefu na nachopendea toka kwake, hana tamaa (kwao wapo vizuri sana baba ana kampuni ya kilimo kubwa tu tanzania na vyeo kede kede) ni mcha Mungu kanisani hakosi na ana akili balaa yani yupo smart sana kichwani sio kama wanawake wengine, mnaweza mkakaa msichana akakuchambulia uchumi wa urusi mpaka marekani china yaani humdanganyi, pia ni mtafutaji balaa. Huyu dada kawa rafiki yangu miaka takribani 5, hajawahi kuniomba hela hata siku moja na nikimnunulia wine kesho ananinulia bia kwa kweli me nimemwona wife material yuko very caring pia mkienda sehemu akinunua kitu lazima na wewe akununulie. Ila shida moja tu, huyu msichana ana penda watu wasiompenda , alikuwa na uhusiano na jamaa flani rubani mlalahoi kwa kumwona tu jamaa mtandaoni nikajua huyu jamaa ni wa kupita tu. kujisikia sana maisha ya kificho ficho mno na alikuwa hajiamini kwa huyo mwanamke ka jinsi rafiki yangu alivyokuwa ananisimulia. Alimfanyia vituko vingi sana huyu binti na iliniuma maana nilikuwa najua huyo ndo bwana wake wa pili tu tangu aanze kujihusisha na mahusiano yani alikuwa fresh kabisa kwa mchezo wa mapenzi jamaa wake wa awali alikuwa mlevi na alikuwa akilewa anampiga waliachana baada miezi 6 tu, na binti ni mdogo bado, mwaka huu ana 23 kama sio 24 nimemjua toka anamaliza chuo akiwa na miaka 19, basi wakaachana na huyo jamaa rubani mlalahoi nikajua yes nimepata sasa wakati wangu wa kumuinga mara bin vuuup jamaa wakarudiana. nikaamuuliza vipi tena? akasema amemsamehe kwa yote na amebadilika. Basi mi nikafanya uchunguzi mdogo tu nikagundua jamaa ana mwanamke mwingine ana mimba yake na kamuahidi ndoa (nilimuona facebook nikamdadisi huyu mwanamke wa rubani mlalahoi mpaka instagram) nikamwonesha huyu binti ila cha kushangaza akaacha kuongea namimi akaweka vipicha vya jamaa wake instagram ikaniuma sana ila sikufanya lolote, nikaendelea kumdadisi huyo mischana wa jamaa mpaka akaniblock (nadhani niliblow my cover au demu alimwambia jamaa). Basi hatukuongea tena. Baadae nikaja kusikia wameachana na jamaa kaoa tayari mwanamke mwingine ( in a span of 3 months baada ya kuachana jamaa kaoa). Maskini huyu binti hakuwa vizuri aliachana kabisa na mapenzi hata nikimtamfuta anasema hayupo tayari kwa mapenzi kwani haamini tena wanaume. Cha kunishangaza yani ni mzuri mno sura shepu figa mzuri wa roho na ni mcheshi haswa huwezi boreka hata chembe ukikaa nae, kwanini kuwakibmbilia wasiompenda? Nimpataje huyu bidada maana nimeoza kwake na ye ndo hataki kabisa mapenzi, kahama kabisa na mkoa anafanya biashara maeneo tofauti, ana mashamba mafinga, ana nyumba za kupanga dodoma, ana biashara nyingine mbeya yani ni mtafutaji ila nashindwa kabisa jinsi ya kumuingia.
update
nimejaribu mbinu nyingi, nimeshawahi mkatia ticket twende serengeti huko tukashangae nikijua binti atakubali ila waaaapi. Kila nachofanya anadecline, wenzangu nipeni mawazo