Nahitaji mshirika katika ufugaji kuku wa kienyeji na bustani

Rogart Ngaillo

JF-Expert Member
Apr 27, 2013
899
1,887
Msimu wa sikukuu uwe mwema kwenu!

Tangu mwaka jana niko kijijini kutafiti namna gani ufugaji na vifanananavyo vinaweza kuniongezea kipato,kwa ufupi kila nilichojaribu kimeonesha kina uashiria wa tija hapo mbeleni.

Mfano:
■ Nilinunua tetea wanne na jogoo mmoja,wamenizalishia zaidi ya kuku 60 (wote wakubwa )

■ Nilijaribu bustani ya mboga na pilipili, hadi sasa matokeo ni chanya.

Nimeona hawa kuku (ambao wengi ni matetea) wanataka kunizidi nguvu maana naona wanaanza kutaga hovyohovyo...nimeanza ujenzi wa banda lao maana chumba waishimo hakikidhi matakwa yao!

● Nahitaji yeyote mwenye ndoto za ufugaji kama zangu tupigane "kampani"

●Niko mbele kidogo ya mkoa wa Njombe kuelekea Ludewa (Mwendo wa saa 3)
●Nina nyumba ya kuishi yenye umeme na maji (kwa umwagiliaji)
●Ukiamua nawe unaweza kuja kuishi huku.

Kama uko interested nichek PM au piga/sms namba hii:-
0765395666
 
PM yako imefungwa. Kuna maswali nadhani ni too personal nataka kukuuliza. Ni PM

Msimu wa sikukuu uwe mwema kwenu!

Tangu mwaka jana niko kijijini kutafiti namna gani ufugaji na vifanananavyo vinaweza kuniongezea kipato,kwa ufupi kila nilichojaribu kimeonesha kina uashiria wa tija hapo mbeleni.

Mfano:
■ Nilinunua tetea wanne na jogoo mmoja,wamenizalishia zaidi ya kuku 60 (wote wakubwa )

■ Nilijaribu bustani ya mboga na pilipili, hadi sasa matokeo ni chanya.

Nimeona hawa kuku (ambao wengi ni matetea) wanataka kunizidi nguvu maana naona wanaanza kutaga hovyohovyo...nimeanza ujenzi wa banda lao maana chumba waishimo hakikidhi matakwa yao!

● Nahitaji yeyote mwenye ndoto za ufugaji kama zangu tupigane "kampani"

●Niko mbele kidogo ya mkoa wa Njombe kuelekea Ludewa (Mwendo wa saa 3)
●Nina nyumba ya kuishi yenye umeme na maji (kwa umwagiliaji)
●Ukiamua nawe unaweza kuja kuishi huku.

Kama uko interested nichek PM
 
Shamba lako ni la umwagiliaj? Linapitiwa na mto usio kauka? Lina ekari ngapi?
Sio shamba hasa...ni eneo lililozunguka nyumba niishiyo,ila ukihitaji eneo kubwa unapata tu tena maeneo yaliyopitiwa na mto usiokauka.

Maji niliyonayo yamevutwa toka mtoni hadi nyumbani...hayakauki,ndiyo nitumiayo kumwagilia bustani ya hapa nyumbani!

Nadhani nimekujibu!
 
Mkuu jitahidi ujikune pale mkono unapofika.

Inaweza ukapata mtu asiye sahihi ukapoteza hata hao wachache. Jitahidi hao wachache kwa sababu wameanza kutaga tumia mayai yao kuwatunza na kuwajengea Banda Bora. Hiyo ni ajira ishikilie.
 
Ahsante!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom