geek01
Senior Member
- Jul 11, 2017
- 143
- 267
Habari ndugu zangu natumaini mambo yanakwenda kama yalivyopangwa na mwenyezi Mungu. Niende kwenye point moja kwa moja, kazi niliyokuwa nafanya ile kampuni imefunga business na inarudi nchini kwao maana hapa upepo wa biashara sio mzuri(hawapati faida na wanatumia gharama kubwa kwenye expenses kama mishahara na kadhalika) hivyo imepelekea kupunguza wafanyakazi zaidi ya robo tatu hadi sasa.
Hivi sasa nipo mtaani nahangaika kutafuta kibarua kingine. Nilipokuwa nimepanga ambapo nilijitahidi kununua vitu kadhaa vya ndani, mwezi uliopita walinivunjia nikiwa sipo na kuiba vitu karibu vyote na kesi ipo polisi, hivi sana nakaa kwa ndugu hapahapa Dar.
Tatizo kubwa ni hapa ninapokaa kila siku huyu ndugu analalamika na nikikosea kitu hata kwa bahati mbaya anasema niondoke na ni mzigo kwake, yeye ameolewa na ana watoto.
Kiukweli inafika sehemu naona maisha magumu sana na mzazi wangu mmoja aliyebaki(mama) ni mgonjwa na mzee hafanyi shughuli yoyote ya mimi kumtegemea yeye zaidi ananitegemea pia.
Elimu yangu ni degree ya maswala ya IT na uzoefu ninao wa kutosha, nisaidieni nipate sehemu ya kujishkiza kwa muda wakati ninaendelea kupambana kwani naamini muda si mrefu nitafanikiwa na nitarudisha chochote nitakachosaidiwa.
Naweza kufanya kazi nje ya kazi za IT na pia hata mikoani naweza kwenda, ninajua lugha 3 Kiswahili, English na French.
Asanteni, naombeni maswali mengine nitayajbu PM au mnipe mawasiliano zaidi.
Naweza kufanya kazi kama;
-mauzo(Sales)
-Kusimamia biashara
-kazi za site
-data entry and data management
-na kadhalika
Hata ya kulala hapohapo itakuwa vyema zaidi.