ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 19,569
- 44,791
Inasikitisha sana sijui ni kwanini hata nimejikuta nimekwisha tumbukia kwenye ulevi wa kutisha kwa hali niliyofikia ni hatari kwani nakunywa pombe karibu kila siku bila ya kupumzika.
Nimeshakunywa za kienyeji karibu zote, pombe kali zote na kwa sasa nimezamia kwenye bia yaani speed yangu kwa kweli sio nzuri.
Nikinywa nikalewa naanza kujisemesha kuwa Mimi siogopi cha Ukimwi wala kansa nakunywa bia nikalale sitaki mwanamke nawaachia wanywa soda.
Kiukweli naogopa kifo kinachosababishwa na unywaji wa pombe kibaya zaidi nahisi ulevi umenisababishia niwe mbali na Mungu wetu imani imeshuka sana sipati tena muda wa kumkumbuka Yesu.
Nahitaji kubadilika lakini mwenyewe nimeshindwa ndugu wameshaongea mpaka wamechoka wameamua kuniacha tu mwenyewe nifanye ninalotaka nikipata kansa au bawasili au maradhi ya pombe nipambane nayo mwenyewe.
Naomba mtaalam wa saikolojia/kiroho wa kujitolea kunisaidia anisaidie mbinu mbadala, natambua ya kwamba maamuzi ya mwisho yananihitaji Mimi binafsi nijikane lakini kama nilivyosema imekuwa ngumu NASHINDWA.