Ramthods
JF-Expert Member
- Jun 2, 2009
- 515
- 186
Ndugu wana JF,
Mama yangu anafanya semina mara kwa mara, na pia ni mtoa mada mzuri sana katika mambo mbali mbali ya kijamii. Ameanzisha ministry ambayo hualika watoto yatima, na wana ndoa, wajane n.k kwa ajili ya mafunzo mbali mbali ... that's it.
Nilimuahidi kuwa ningemnunulia vyombo vya muziki - speakers, mixer, amplifier n.k ili wapunguze gharama wanazotumia kukodisha hivi vyombo.
Pia, nadhani vitamsaidia sana maana yeye hutoa pia mada kwenye kitchen parties, send off na harusi.
Binafsi, sina utaalamu kabisa na hivyi vyombo - jambo ambalo limenipa shida sana kujua "Quality ya vyombo, price, na wapi naweza kuvipata"
Nimejaribu kuzunguka maduka tofauti tofauti mjini, na pia kuulizia watu wanaofanya shughuli kama hizi - lakini bado sijapata ushauri wa kueleweka.
Naomba kama unafahamu, una utaalamu wowote kuhusu vyombo vya muziki utoe mchango wako kwenye hii thread.
Vyombo vinavyohitajika vinatakiwa viwe na uwezo wa kupiga muziki, na kutangazia kwenye ukumbi wa kawaida (watu 300 hadi 600). Kama vile tunavyoviona kwenye sherehe mbalimbali za maharusi au send off.
Natanguliza shukrani!