Baruti wa Mkojani anafanya vyema kwenye muziki ukilinganisha na sanaa ya maigizo

E Motherland

Member
Oct 1, 2023
20
10
Habari zenu wana JF. Baruti ni kijana anayekuja kwa kasi katika sanaa nzima ya muziki nchini. Hamasa aliyokuwa nayo katika kufikia malengo yake imefanya vijana wengine mitaani kupambana zaidi na zaidi katika kuyafikia makusudio yao maalumu
images.jpeg

Bila shaka kwa wale wakazi na wafanya biashara katika maeneo changanyike humu Dsm hasahasa Mbezi na Tabata tunamfahamu kijana huyu kuanzia katika shughuli nzima ya uchakarikaji katika kuitafuta senti ambayo sehemu ya maokoto aliwekeza katika sanaa yake ya muziki

Baruti anaendelea kututhibitishia kuwa muziki sio sehemu ya uhuni kama wafikiriavyo wazazi walio wengi, bali muziki ni sanaa kama zilivyo sanaa nyingine za ususi, ufinyanzi, uhunzi, udarizi, ushonaji, maigizo n.k Muziki ni ajira, muziki ni pesa, muziki ni ujumbe, muziki ni burudani n.k

Juhudi za msanii Baruti ni za kuigwa kwa vijana wapambanaji wenye dhamira ya kufikia malengo yao. Ili kuyafikia malengo husika yakupasa kutafuta kila kona yenye upenyo utakaokufanya kusogea mbele. Sanaa ya uigizaji kwake imetumika kama daraja la kumfanya awe maarufu kwa kiasi chake

Idea na content zake katika michezo ya runinga ya Mkojani sio tu imeelimisha jamii bali imekuza jina la Mkojani na kuwafanya Mkojani na Samofi kuwa wacheshi pendwa nchini na nje ya mipaka

Muziki wa Baruti ni muziki wa hisia, haandiki kama anaandikia nyumbu kama wafanyavyo wasanii wengi hasa wale wenye majina, music with no sexual content, huimba kwa kumaanisha, pia yuko serious na kipaji chake, tone nzuri ya uimbaji kuliko wasanii wote nchini, pia yuko smart katika utunzi wa idea na mpangilio wa kazi

Baadhi ya kazi zake bora ni pamoja na:

4. For You, wimbo wenye maneno matamu ya kumtamkia mpenzi wako ambaye uko naye kwenye mahusiano yenye amani, wataalamu tunaita kupalilia penzi

"...Najihisi raha, kila nishikapo nywele zako,
You're My Baby, I do never let you go,
Baby, nitakufuata ulipo,
Si unajua nimekuzoea, Jua, mvua unaogelea, kifuani kwangu unabembea, unavyodeka kama mtoto..."

3. Wanangu, hapa ameeleza jinsi ambavyo watu wa karibu wana nafasi katika maisha ukilinganisha na mpenzi, hujui atakaekuzika ni nani. Sawa, mpe mpenzi nafasi katika maisha, lakini sio atawale moyo kiasi cha kusahau marafiki uliotoka nao mbali

"...Welcome maghetoni, hapa ndipo naishi mimi, usione viatu vingi ni vya wanangu mostly I know,
Usiogope wala usitishike, wanangu watu wa dili watu wa mishemishe, sema nikupe tahadhari ningeomba uwe makini, kama ukipika ukipakua waweke, naomba ujue wanangu, hao ndo ndugu zangu..."

2. Playboy, ujumbe maalumu kutoka kwa wanaume waliojikatia tamaa ya kupenda. Hivyo wakaamia katika suala zima la kuHit and Run

" ...Sijui kupenda, nikikupenda jua igizo, naangalia mapenzi sina ushamba wa kupagawa na sura, yaani mimi kukupanga foleni sioni shida sioni tabu, bingwa wa kuchit ninajijua..."

1. Nobody, wimbo wa kuuzunisha unaomhusu kijana aliyekuwa kwenye mahusiano na binti ambaye alikuja kumuona jamaa takataka baada ya kupata mwanaume mwenye pesa ambaye anafahamiana na huyo kijana wa awali

"Just assume, nina picha zako kwa ukuta,
vizawadi vingi ulivyonipa, nimezitunza nimeshindwa kutupa,
Ndivyo vinaniliwaza, japo mengi yanashangaza, madhaifu yangu kutangaza unanitesa, naomba ikawe heri, japo kinyonge, nisingependa tugombane, najua unajua ila unaact nakusumbua, acha niwe kolo Mungu ndo anajua, kama kuna kosa nilokufanyia... Ahsante"

Big Up Sana kwa Kijana Baruti wa Mkojani
 
Hakuna kazi yake bomba ninayoikubali kama Nobody na uhusika wake kwenye ile movie waliomshirikisha Dulla Makabila

Atafika mbali aisee, ana kitu cha ziada
 
Dogoo yupo vizurii...anatakiwa kujibland na kujitumaa
Atajibrand vipi bila kupata support kutoka kwa watu wenye nia ya kufanya muziki-ajira ilihali JF members tulio wengi tuko na uwezo lakini ukomo wa akili zetu ni kwenye kuhonga mabinti na wake za watu?
 
Au unaweza kuta ni ID ya yule mke wa Mkojani kwenye ugaigai. Maake kwa namna ambavyo walipendana na Baruti kupitia shughuli nzima ya upakaji rangi kucha na usuguaji wa magaga, labda penzi lao wamehamishia humu
Watoto wanachoma sigara sheli.🤓🤓🤓🤓🤓🤓🤓
 
Habari zenu wana JF. Baruti ni kijana anayekuja kwa kasi katika sanaa nzima ya muziki nchini. Hamasa aliyokuwa nayo katika kufikia malengo yake imefanya vijana wengine mitaani kupambana zaidi na zaidi katika kuyafikia makusudio yao maalumu
View attachment 2769191

Bila shaka kwa wale wakazi na wafanya biashara katika maeneo changanyike humu Dsm hasahasa Mbezi na Tabata tunamfahamu kijana huyu kuanzia katika shughuli nzima ya uchakarikaji katika kuitafuta senti ambayo sehemu ya maokoto aliwekeza katika sanaa yake ya muziki

Baruti anaendelea kututhibitishia kuwa muziki sio sehemu ya uhuni kama wafikiriavyo wazazi walio wengi, bali muziki ni sanaa kama zilivyo sanaa nyingine za ususi, ufinyanzi, uhunzi, udarizi, ushonaji, maigizo n.k Muziki ni ajira, muziki ni pesa, muziki ni ujumbe, muziki ni burudani n.k

Juhudi za msanii Baruti ni za kuigwa kwa vijana wapambanaji wenye dhamira ya kufikia malengo yao. Ili kuyafikia malengo husika yakupasa kutafuta kila kona yenye upenyo utakaokufanya kusogea mbele. Sanaa ya uigizaji kwake imetumika kama daraja la kumfanya awe maarufu kwa kiasi chake

Idea na content zake katika michezo ya runinga ya Mkojani sio tu imeelimisha jamii bali imekuza jina la Mkojani na kuwafanya Mkojani na Samofi kuwa wacheshi pendwa nchini na nje ya mipaka

Muziki wa Baruti ni muziki wa hisia, haandiki kama anaandikia nyumbu kama wafanyavyo wasanii wengi hasa wale wenye majina, music with no sexual content, huimba kwa kumaanisha, pia yuko serious na kipaji chake, tone nzuri ya uimbaji kuliko wasanii wote nchini, pia yuko smart katika utunzi wa idea na mpangilio wa kazi

Baadhi ya kazi zake bora ni pamoja na:

4. For You, wimbo wenye maneno matamu ya kumtamkia mpenzi wako ambaye uko naye kwenye mahusiano yenye amani, wataalamu tunaita kupalilia penzi

"...Najihisi raha, kila nishikapo nywele zako,
You're My Baby, I do never let you go,
Baby, nitakufuata ulipo,
Si unajua nimekuzoea, Jua, mvua unaogelea, kifuani kwangu unabembea, unavyodeka kama mtoto..."

3. Wanangu, hapa ameeleza jinsi ambavyo watu wa karibu wana nafasi katika maisha ukilinganisha na mpenzi, hujui atakaekuzika ni nani. Sawa, mpe mpenzi nafasi katika maisha, lakini sio atawale moyo kiasi cha kusahau marafiki uliotoka nao mbali

"...Welcome maghetoni, hapa ndipo naishi mimi, usione viatu vingi ni vya wanangu mostly I know,
Usiogope wala usitishike, wanangu watu wa dili watu wa mishemishe, sema nikupe tahadhari ningeomba uwe makini, kama ukipika ukipakua waweke, naomba ujue wanangu, hao ndo ndugu zangu..."

2. Playboy, ujumbe maalumu kutoka kwa wanaume waliojikatia tamaa ya kupenda. Hivyo wakaamia katika suala zima la kuHit and Run

" ...Sijui kupenda, nikikupenda jua igizo, naangalia mapenzi sina ushamba wa kupagawa na sura, yaani mimi kukupanga foleni sioni shida sioni tabu, bingwa wa kuchit ninajijua..."

1. Nobody, wimbo wa kuuzunisha unaomhusu kijana aliyekuwa kwenye mahusiano na binti ambaye alikuja kumuona jamaa takataka baada ya kupata mwanaume mwenye pesa ambaye anafahamiana na huyo kijana wa awali

"Just assume, nina picha zako kwa ukuta,
vizawadi vingi ulivyonipa, nimezitunza nimeshindwa kutupa,
Ndivyo vinaniliwaza, japo mengi yanashangaza, madhaifu yangu kutangaza unanitesa, naomba ikawe heri, japo kinyonge, nisingependa tugombane, najua unajua ila unaact nakusumbua, acha niwe kolo Mungu ndo anajua, kama kuna kosa nilokufanyia... Ahsante"

Big Up Sana kwa Kijana Baruti wa Mkojani
Hatumjui na hatutaki kumjua
 
Hawa wasanii mavi wana nikera na hivyo virasta vyao na vima hereni kama madada poa vile 😡😡
 
Back
Top Bottom