Nahitaji kwenda Mombasa kupitia mpaka wa Sirari

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
5,405
7,382
Naombeni mwongozo wakuu! Safari ni wiki ijayo.

Kwa Sasa nipo Mwanza. Nitavukia mpaka wa Sirari. Naomba kufahamishwa kuhusu yafuatayo:
1. Ni muda gani mzuri kusafiri kutoka Sirari kwenda Mombasa kati ya Asubuhi, Mchana, Jioni na Usiku?

2. Kuna usafiri wa moja kwa moja kutokea Sirari hadi Mombasa?

3. Usafiri gani mzuri kama nataka nifaidi mandhari, wa kuunga unga au wa moja kwa moja?

4. Nauli ni shilingi ngapi kutoka Sirari hadi Mombasa?

5. Ni mabasi gani yanayoenda huko Mombasa? Yanapaki wapi Sirari? Muda wa kuondoka Sirari ni saa ngapi?

6. Lodge/gesti gani Mombasa ni nzuri yenye usalama lakini bei rahisi?

7. Wakati wa kurejea Tanzania, nitapenda kuzungukia Kampala niingie Tanzania kupitia mpaka wa Mutukula. Nauli inaweza ikagharimu kiasi gani kutoka Mombasa hadi Mutukula kupitia Kampala? Ni mabasi gani yanaweza kunifikisha Kampala kutokea Mombasa?

8. Lodge/Guest gani nzuri yenye ulinzi/ usalama Kampala lakini ya bei rahisi?
 
Kwanini usije hadi tanga upite mpaka wa horohoro au moshi holili?
Mkuu, labda kupitia Holili. Kupitia Horohoro kutokea Mwanza ni mbali sana.

Kwa mujibu wa google, umbali kutoka Mwanaza hadi Mombasa kupitia Sirari ni kilomita 1168

Umbali wa kutoka Mwanza hadi Mombasa kwa kuzungukia Holili ni kilomita 970

Na umbali wa kutoka Mwanza hadi Mombasa kupitia Horohoro ni kilomita 1870.

Kwa mchanganuo huo, umbali mfupi kabisa ni wa kupitia Holili, na wa pili kwa ufupi ni WA kupitia Sirari.

Hata hivyo, kwa wakati huu, nimechagua kupitia Sirari. Kuna sababu iliyonifanya niichague hiyo route.
 
Ukivuka Boda ya Sirari utavukia Isibania ambayo iko upande wa Kenya hapo kuna mabasi ya moja kwa moja mpaka Mombasa ukifika hapo maswali yote uliyouliza utajibiwa pale.
 
Mkuu, labda kupitia Holili. Kupitia Horohoro kutokea Mwanza ni mbali sana.

Kwa mujibu wa google, umbali kutoka Mwanaza hadi Mombasa kupitia Sirari ni kilomita 1168

Umbali wa kutoka Mwanza hadi Mombasa kwa kuzungukia Holili ni kilomita 970

Na umbali wa kutoka Mwanza hadi Mombasa kupitia Horohoro ni kilomita 1870.

Kwa mchanganuo huo, umbali mfupi kabisa ni wa kupitia Holili, na wa pili kwa ufupi ni WA kupitia Sirari.

Hata hivyo, kwa wakati huu, nimechagua kupitia Sirari. Kuna sababu iliyonifanya niichague hiyo route.
Aha hapo sawa, kama kuna sababu za kupita sirari.
 
Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni. Wakenya wengi wanajitahidi kwenye eneo la customer "care". Nimeyashuhudia haya katika leo katika "matatu"niliyoipanda kutoka Sirari hadi Kisii:

1. Sehemu za kuchajia simu kwenye "matatu"
2. Tv kila upande ingawa nilisahau kuzihesabu.
3. Abiria ni level seat.
4. Makondakta na madereva wenye kauli nzuri.

Ingawa niliyoipanda kutoka Kisii hadi Nakuru haikuwa na tv wala eneo la kuchajia simu, huduma inaridhisha.

Wahusika wanajitahidi kuwahudumia abiria kistaarabu
1. Mwendo wa kistaarabu pamoja na kwamba hatukukutana na trafiki njiani kuanzia Kisii hadi Nakuru. Ilikuwa hivyo pia safari ya Sirari hadi Kisii.
2. Kauli nzuri kwa abiria
3. Hawawasimamisha abiria kwenye gari.

Hongera zao Wakenya.
 
Attachments

 • VID_20231202_111151.mp4
  31.3 MB
 • IMG_20231202_111143.jpg
  IMG_20231202_111143.jpg
  165.1 KB · Views: 5
 • IMG_20231202_111443.jpg
  IMG_20231202_111443.jpg
  314 KB · Views: 4
 • IMG_20231202_111458.jpg
  IMG_20231202_111458.jpg
  204.4 KB · Views: 5
 • IMG_20231202_111455.jpg
  IMG_20231202_111455.jpg
  108.3 KB · Views: 5
Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni. Wakenya wengi wanajitahidi kwenye eneo la customer "care". Nimeyashuhudia haya katika leo katika "matatu"niliyoipanda kutoka Sirari hadi Kisii:

1. Sehemu za kuchajia simu kwenye "matatu"
2. Tv kila upande ingawa nilisahau kuzihesabu.
3. Abiria ni level seat.
4. Makondakta na madereva wenye kauli nzuri.

Ingawa niliyoipanda kutoka Kisii hadi Nakuru haikuwa na tv wala eneo la kuchajia simu, huduma inaridhisha.

Wahusika wanajitahidi kuwahudumia abiria kistaarabu
1. Mwendo wa kistaarabu pamoja na kwamba hatukukutana na trafiki njiani kuanzia Kisii hadi Nakuru. Ilikuwa hivyo pia safari ya Sirari hadi Kisii.
2. Kauli nzuri kwa abiria
3. Hawawasimamisha abiria kwenye gari.

Hongera zao Wakenya.
Chief naona umebabua hela za dhahabu now unakula raha tu!
 
Ubepari umewatengeneza
 
Na mimi nasubiri majibu kwenye huu uzi...Mkuu upite na kule kwa wajaluo ukaonje dada zake lupita nyong'o.
 
Kuna kipindi kulikuwa na basic za Modern Coast toka Mwanza kwenda Nairobi. Ulizia kama bado zipo upande mpaka Nairobi alafu uunganishe Mombasa

Au panda basi Mwanza to Tanga alafu upitie Tanga kwenda Mombasa.
 
Nashukuru sana mkuu. Safari ilishafanyika na hivi sasa nipo Tz.

Mabasi ya Modern Coast yalisitisha safari za Mwanza - Nairobi tokea kipindi cha mlipuko wa Corona.

Nilienda mpaka Sirari na kisha baada ya kuingia upande wa Kenya, nilipanda magari ya kuunga unga (matatu) ya huko Kenya.

Wakati wa kurudi Tz, nilipanda basi la PALMERS COACH kutoka Nairobi hadi Kampala. Sijui kama walinizidishia nauli 😀 Walinitoza Ksh 3,500/= wakati kama ningepanda Modern Coast ya Nairobi - Kampala ningelipa pungufu ya hiyo.
 
Naombeni mwongozo wakuu! Safari ni wiki ijayo.

Kwa Sasa nipo Mwanza. Nitavukia mpaka wa Sirari. Naomba kufahamishwa kuhusu yafuatayo:
1. Ni muda gani mzuri kusafiri kutoka Sirari kwenda Mombasa kati ya Asubuhi, Mchana, Jioni na Usiku?

2. Kuna usafiri wa moja kwa moja kutokea Sirari hadi Mombasa?

3. Usafiri gani mzuri kama nataka nifaidi mandhari, wa kuunga unga au wa moja kwa moja?

4. Nauli ni shilingi ngapi kutoka Sirari hadi Mombasa?

5. Ni mabasi gani yanayoenda huko Mombasa? Yanapaki wapi Sirari? Muda wa kuondoka Sirari ni saa ngapi?

6. Lodge/gesti gani Mombasa ni nzuri yenye usalama lakini bei rahisi?

7. Wakati wa kurejea Tanzania, nitapenda kuzungukia Kampala niingie Tanzania kupitia mpaka wa Mutukula. Nauli inaweza ikagharimu kiasi gani kutoka Mombasa hadi Mutukula kupitia Kampala? Ni mabasi gani yanaweza kunifikisha Kampala kutokea Mombasa?

8. Lodge/Guest gani nzuri yenye ulinzi/ usalama Kampala lakini ya bei rahisi?

Tanga is the best route, Kwa nn utembee kenya yote wakati unaweza tembea Tanzania to Tanga the 2 hours upo Mombasa
 
Back
Top Bottom