Wafanyabiashara Waikimbia Bandari ya Dar na Kwenda Mombasa Port

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,785
My Take, DP World itakomesha Bandari yetu kuwa shamba la Bibi
===
Sehemu ya wafanyabiashara wa Tanzania sasa wanaamua kuagiza bidhaa zao na kuzisafirisha hadi Bandari ya Mombasa badala ya bandari zao za Dar-es-Salaam na Tanga.

Akizungumza katika kipindi cha Good Morning cha Wasafi FM, mfanyabiashara mmoja alieleza sababu ya kuchagua usafirishaji kupitia Mombasa na kusafirisha bidhaa zake kwenda Tanzania.

"Ninaamini bandari za Tanzania zimepoteza wateja wengi kutokana na kuchelewesha kufungua mizigo kutoka kwenye meli, hivyo kusababisha kuchelewa zaidi kwa muagizaji kupata bidhaa zake. Kwa mfano, ukiangalia bandari ya Mombasa, Watanzania wengi wanapeleka makontena yao huko na kuyafungua kutoka kwenye meli pale. Hata mimi nafanya hivyo. Hii ni kwa sababu wanajua kwamba mara meli inapowasili, mizigo inafunguliwa mara moja. Hakuna malipo ya ziada na ndani ya muda mfupi, anapata bidhaa zake; na gharama za usafirishaji - ada za kusafirisha kontena hicho - ni nafuu zaidi kuliko Dar-es-Salaam. Hii ni kwa sababu majirani zetu wameboresha vifaa vyao, wanajua jinsi ya kutoa huduma haraka na wana ufanisi," alisema mwendeshaji wa Perfect Ocean Freight.

Mombasa ni bandari kubwa zaidi katika Afrika Mashariki kwa ukubwa na uwezo. Inashughulikia mizigo mingi kwa nchi zisizokuwa na ufikiaji wa bahari, ikiwemo Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudan Kusini, Rwanda, na Burundi kwa kuwapa njia moja kwa moja kwenda baharini. Hata hivyo, bandari hiyo imekuwa ikikabiliwa na ushindani mkali kutoka Bandari ya Dar, ambayo inafanya habari hii ya mwendeshaji iwe ya kushangaza.

Kufikia mwaka 2021, Bandari ya Mombasa ilikuwa inashughulikia mzigo mara mbili zaidi kuliko Bandari ya Dar. Bandari ya Mombasa ilishughulikia tani milioni 34.54 ikilinganishwa na tani milioni 17.03 za Bandari ya Dar. Bandari ya Tanga ilishughulikia tani milioni 0.84, Mtwara tani milioni 0.21, na Lamu tani milioni 0.04.

Kujibu maoni ya mfanyabiashara huyo, baadhi ya Watanzania walitoa maoni tofauti kama yafuatayo:

"Kwa nini niliagiza gari langu kupitia Mombasa? Kwa mtu anayeishi Moshi, Himo, Holili, Rambo, au Marangu, kwanini ungeagiza kupitia Dar wakati Mombasa iko karibu? Tatizo sio kuchelewa kwenye bandari, bali linategemea upande gani wa Tanzania unakoishi. Acheni uwongo," alisema Serengeti One.

"Sawa, basi Mombasa inatoa huduma na ujuzi mzuri. Je, wameshauza bandari yao kwa wageni? Wamewapa nani jukumu la kuendesha bandari hiyo milele? Kwa nini Tanzania isifanye kama Kenya ilivyofanya? Tatizo ni kwamba serikali haitafanya kazi bila rushwa na wanakula pesa kama mchwa," aliongeza Dkt. Calipso.

"Je, bandari ya Mombasa imekuwa ikimilikiwa na watu binafsi? Serikali ya CCM imejaa wafanyabiashara wote nchini Tanzania. Kenya inaendesha bandari yao ya Mombasa kwa ufanisi. Kwa nini serikali ya Tanganyika isiweze kufanya hivyo? Wajinga wote na wasemaji wao ni wapumbavu ambao kwanza wanafikiria juu yao wenyewe badala ya taifa. Mwaka 2025 wataongeza miaka mingine 5, kwa nini?" aliuliza Osei Tutu.
 
Haitakuwa yenu tena, wewe sema bandari ya waarabu wa Dubai.
Si mnawauzia na tena mnawapa bure kabisa.
 
My Take
DP World itakomesha Bandari yetu kuwa shamba la Bibi
Lazima itafutwe justification!!! Yalifunguliwa Maji ili turbines zishindwe kuzunguka watu wapigie hela za mitambo midogo na mikubwa ya nishati seuze/sembuse....!!!!
 
Hili dili linapigiwa upatu sana!!

Umoja na mshikamano wa Watanzania inaelekea kupasuka kwa kasi, watawala wameanza kujificha kwenye kichaka cha udini!!

Watetewe na wadini wao,wanaaminisha wanaonewa na wa dini nyingine.

Dealni dealtu,halinaga dini, maendeleo pia hayana dini Ila kitu Cha hovyo ni Cha hovyo tu pasi kujali dini!!
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Haya maswal yapo juu ya uwezo wa chawa choiceVariable!!! Hatoweza jibu kiufasaha!!
 
My Take
DP World itakomesha Bandari yetu kuwa shamba la Bibi
Hii habari ingekuwa imeandikwa na waandishi wetu tungesema wamelipwa kutetea uwekezaji


Hii habari wameandika waandishi wa nje tena kwa ushahidi. Alafu kuna mijitu inaleta Siasa kwenye maamuzi ya Serikali ambayo yamefanywq kwa faida la Taifa

Tanzania ujinga ni kipaji
 
My Take
DP World itakomesha Bandari yetu kuwa shamba la Bibi
Chuo Kikuu cha Dar (UDSM) Kijitadhimini kuhusu huu mkataba na PhD walioitwaa kwa yule mtu.
1623321C-D129-4183-B6BE-91ECF49B86F5.jpeg
 
My Take
DP World itakomesha Bandari yetu kuwa shamba la Bibi
Yaani kama Serikali inajificha kwenye hiyo kauli na kwa kuona kwamba kubinafsisha (Specific kwa kwa DP Word) ndiyo suluhisho pekee na hao Viongozi inabidi wajitafakari, maana haiwezekani viongozi walio apa kuilinda nchi na Watu wake (+ katiba) ijivunie kuonesha unyonge dhidi ya wabadhilifu wa mali ya umma. kwamaana hiyo wanatuiambia kwamba wabadhilifu hao wako juu ya serikali! hii ni hatari sana. hivi hao DPW wana maajabu gani ya ziada chini ya jua ambayo sisi Wa TZ tukiamua tunashindwa kuyafanya? kama ni Technologia ni kweli kabisa wanayo wao tu na milki yao mtu mwingine haruhusiwi kuitumia? Hivi kiongozi kama ameshinwa kazi na ubunifu inamaana Watanzania wote hawawezi? tTufike mahali kama taifa tujitafakari kwakweli!
 
My Take
DP World itakomesha Bandari yetu kuwa shamba la Bibi
Kwani huo urasimu ni hadi DP world? Sisi hatuwezi umaliza? Vip urasimu wa TRA? apewe mchina? Wacha kuwaza kwa kutumia kisamvu chako cha hapo nyuma.
 
Back
Top Bottom