Naomba kufahamu usafiri wa kunifikisha Mombasa kutokea Sirari.

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Wiki ijayo ninatarajia kwenda Mombasa nchini Kenya. Nipo Mwanza, na nitavukia mpaka wa Sirari. Naombeni mwongozo kwa wenyeji na wazoefu:

1. Ni muda gani mzur kusafiri kutoka Sirari kwenda Mombasa? Najua Kenya kuna usafiri masaa 24 kwa siku.

2. Kuna gari la moja kwa moja kutoka Sirari hadi Mombasa?

3. Nauli ni shilingi ngapi Sirari hadi Mombasa?

4. Lodge gani nzuri lakini ya bei nafuu Mombasa? Kipaumbele cha kwanza ni usalama.

Bei ya lodge/gesti ni shilingi ngapi?

5. Shughuli inayonipeleka Mombasa inaweza ikanichukua siku mbili kuikamikisha. Baada ya hapo, nitarejea Tz.

Ninafikiria kurudi kwa kuzungukia Kampala, kama gharama haitakuwa kubwa sana. Inaweza ikanigharimu shilingi ngapi kutoka Mombasa hadi Mutukula kwa kupitia Kampala? Kuna changamoto yoyote kwenye mpaka wa Kenya kwenda Uganda (sijawahi kuingia Uganda kupitia Kenya).

Ni magari gani yanayoenda Kampala/ Mutukula kutokea Mombasa Kenya?

Naomba kuwasilisha🙏
 
Naomba kuwasilisha
Toka Mwanza mapema asubuhi
Ukifika Sirari fanya booking ya Nairobi, gari zinatoka Sirari 20:00

Utafika Nairobi around 04:00 hivi, asubuhi yake panda kwenda Mombasa
 
Safari ndefu hiyo ila 1 kwa 1 hadi huko sidhani,

Kwa Sirare (Isbania) panda bus gurdian, easy coach au nyamira ila (kunguni kama wote) shuka Nairobi asubuhi panda tren kwenda Mombasa iko faster sana shukia Mariakani lodge zipo au uingie city center kabisa lodge zipo nyingi tu japo sio smart ukicompare bei na room ilivyo, kama uko vizuri tafuta room ya Ksh. 2k, 3k angalau
 
Nashukuru sana mkuu. Kama hutajali, naomba makadirio ya nauli ya kutoka Sirari hadi Nairobi kisha Nairobi hadi Mombasa.
 
Sirare Nairobi ni ksh1500 Nairobi Mombasa ni 1700-2000 inategemea na basi ambalo utatumia,Kuna mabasi kibao tu Kama Ena coach, easy coach, guardian angel,nyamira, ukifika migori kwenyewe utapata Tahmeed ni vizuri utumie Tahmeed maana watakueka moja kwa moja kwa mabasi yao ya Mombasa,Ena coach pia wanasafari za Mombasa, ukishukia mariakani hapo ni nyuma Sana Kama mlandizi vile au kibaha itakugharimu Tena nenda mjini kabisa, huwezi ukatumia treni ,ukitaka kutumia treni itakubidi ukate tiketi kabla ya siku ya kusafiri Kama siku tatu kabla ya siku ya kusafiri.
 
🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom