Nahitaji kurudi nyumbani

Nahitaji kurudi nyumbani

Nimegundua mumeo hajakushirikisha c anajua una roho ya korosho.

Yeah...nampa big_up sana jamaa kwa kujitambua mkuu...mtu kama una uwezo wa kumudu familia yako...sion ni kwanini usisaidie ndugu zako.....kamsoma mke wake ana tabia mbaya.
 
Yeah...nampa big_up sana jamaa kwa kujitambua mkuu...mtu kama una uwezo wa kumudu familia yako...sion ni kwanini usisaidie ndugu zako.....kamsoma mke wake ana tabia mbaya.

Hapo angekuja nd yake isingekuwa tatizo
 
We huitaki ndoa? Yani ndugu wa mume ndo akufanye ukimbie nyumba?
Tena ukute hata salam hamjasalimiana..

Kweli wanawake wengi ila wake wanahesabika....

Swali la kizushi, Somo yako nani vileee?
Ndo alikufundisha wakija ndugu wa mume urudi kwenu?
 
Habari zenu wapendwa, imani yangu ni kuwa mu wazima,

Kuna tatizo hapa, asubuhi ya leo nimekaa najiandaa kutoka kaja binamu wa mume wangu na mabegi kuuliza eti amekuja kukaa nyumbani kwangu asome chuo.

Kumuhoji kawa mkali eti mimi sina ubinadmu na mambo mengi mabaya nikasema tatizo siyo huyo binti kuja tatizo kwa nini hakunijulisha kama walishapanga amlete hapo nyumbani.

Nilichofikiria mimi naondoka niende nyumbani kwetu kidogo nirudi baada ya wiki moja coz haya mambo hata katika familia nilivyokulia baba hawezi fanya kitu kama hicho bila kumjulisha mama.

Hapa nipo sahihi wapendwa?

Wanaume wote hawawezi kuwa sawa na baba yako, kila mtu anaendesha familia kivyake. Kila familia yaani mme na mke ni unique duniani - hakuna zinazofanana. Kuondoka nyumbani sio ufumbuzi. Ukirudi ukakuta kuna mwingine hapo nyumbani usije kulia tena hapa. Gangangamala nyumbani kwako utafute ufumbuzi na mumeo!
 
umeona eeh afu unakuta mtu anakuwa ivo ukiangalia familia aliyotoka unachoka mwili na roho...kila kukicha afazali ya jana

Hao wanataga ndg zao tu ndio wasaidiwe...familia za kiafrica huwezi kuacha kusaidia ndg kama una uwezo
 
Wanaume wote hawawezi kuwa sawa na baba yako, kila mtu anaendesha familia kivyake. Kila familia yaani mme na mke ni unique duniani - hakuna zinazofanana. Kuondoka nyumbani sio ufumbuzi. Ukirudi ukakuta kuna mwingine hapo nyumbani usije kulia tena hapa. Gangangamala nyumbani kwako utafutev ufumbuzi na mumeo!

Wewe unajitambua..........hawa kina manka wamezidi ubinafsi mkuu.......
 
haupo sahihi hata kidogo siyo jambo la kukufanya uondoke mpendwa... muuleze huyo mumeo kuwa hujapenda siku nyingine asifanye hivyo tena
 
ha ha ha ha uuuuuupsi ondoka wenzio tuhamie loo

acha utot kaa na mumeo muongeee

kumbuka baba ni kichwa cha familia kosa alofanya ni kukutokukushirikisha tu
anatoa nafasi nzuri ya mchepuko ha ha ha
 
Mwenzako kafanya kosa kwa kutokushirikisha katka suala kama hilo. Hata hivyo uamuz wa kuondoka uache familia si mzuri nadhani bado mna muda wa kukaa mkazungumza juu ya hilo hata kama kosa la awali lishafanyika. Hiyo ni familia yako na we kama mama una mchango mkubwa kuhakikisha inakaa stable. Kitendo cha kuondoka hata kama ni wiki kinaweza kuwa na madhara makubwa kuliko unavyoweza kufikiria

kwani uyo binamu kaja kuchukua nafasi ya mke ili uyu aondoke au amekuja kusoma akimaliza anakula winga...roho mbaya yake tu
 
Wanawake wengine bana ni Viazi, inamaana wewe mtu akitaka kuja kwa mmeo lazima akwambie wewe ndio umpe Visa ama? Nathubutu kusema ni utoto unakusumbua na pili ni kwakuwa hauna watoto bila shaka ndio maana!
we kweli strong rula!
 
nanusa harufu ya matatizo mengi yaliyojificha ktk ndoa yako.!,
1. Unaonekana ni Jeuri.
2. Humshirikish mumeo ktk mambo yako.
3. Akimwaga mboga wewe wamwaga ugali.
4. Si mvumilivu.
5. Unahasira za pupa.
6.umeshaichoka ndoa.
7. Kati yenu kuna michepuko.
8. Umeshamuona mumeo mzigo.
9. Mnakomoana.

..ushauri,
ongozaneni kwenye maombi mnusuru ndoa.
 
Nenda tu mwehu wewe,una roho mbaya kuliko hata bokoharam.


mgeni hata ugali hajala unataka kuondoka,.

Mijanamke kama nyinyi mnafaa mtupambie jukwaa letu pendwa kule chini na wala sio kuolewa.
 
hatuachi nyumba kirahisi hivyo lauuuu!
utaratibu wa mawasiliano nyumbani kwako uko vipi?
unajua aina ya mume uliye naye?
familia ulikotoka haifanyi hivyo sawa,familia aliyotoka je?
ndoa yenu ina muda gani?
kama nikwambie uchague miongoni mwa wanyama,ndugu wa mume wako ungewapa jina llipi?
mumeo je?
nsaidie hapo kwanza af twende sawa my wee!
 
Habari zenu wapendwa, imani yangu ni kuwa mu wazima,

Kuna tatizo hapa, asubuhi ya leo nimekaa najiandaa kutoka kaja binamu wa mume wangu na mabegi kuuliza eti amekuja kukaa nyumbani kwangu asome chuo.

Kumuhoji kawa mkali eti mimi sina ubinadmu na mambo mengi mabaya nikasema tatizo siyo huyo binti kuja tatizo kwa nini hakunijulisha kama walishapanga amlete hapo nyumbani.

Nilichofikiria mimi naondoka niende nyumbani kwetu kidogo nirudi baada ya wiki moja coz haya mambo hata katika familia nilivyokulia baba hawezi fanya kitu kama hicho bila kumjulisha mama.

Hapa nipo sahihi wapendwa?

Wanawake wa siku hizi, majanga tu. Kwa style hii, mtawafanya watu waogope kuoa. Ondoka tu mama, iko siku utapata mnayefanana muishi peke yenu kama wachawi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom