Mnanaa ni mmea ambao unapatikana sana katika nchi mbalimbali ikiwemo za hapa Afrika Mashariki, huku wengi wakiutumia mmea huu kwa kuupanda kama maua katika nyumba zao pamoja na bustanini.
Mmea huu huwasidia sana kinamama ikiwemo kuondoa maumivu wakati wa hedhi, kizazi kuuma pamoja na kuongeza maziwa kwa kina mama wanaonyonyesha.
Aidha, mnanaa pia husaidia watu wenye tatizo la misuri inayokaza ama kustuka , kutuliza maumivu ya sikio, kutuliza maumivu, sambamba na kutibu homa ya manjano.
Mnanaa pia husaidia maradhi ya koo, minyoo kwa watoto wenye chai yake,kuzui kichefuchefu na kutapika, kutoa gesi tumboni na kuzuia kuharisha na matatizo ya tumbo.
Hata hivyo, mnanaa bado unauwezo wa kutibu maradhi mengi zaidi ambayo ni pamoja na matatizo ya meno, ambapo mhusika hupaswa kusukutua au kutafuna mmea huo, huku ukifahamika kwa kuwa dawa nzuri ya kulinda meno yasiweze kumeguka au kung’oka na kuvuja damu kwenye fizi. SOURCE GOOGLE FROM MANDAIBLOG