Nahitaji kubadilisha fani ya uwalimu


Daah yan nimesoma nikajikuta mpka machozi yana nitoka mkuu mungu akubariki uwe na moyo huo huo usiwe kama wengine wanakatisha watu tamaa Asante sana kaka ngoja nifanyie Kazi ushauri wako niishi ndoto zangu
 
Mkuu mishahara ya ualimu siyo midogo kama unavyodhani. Kuna watu wana mishahara midogo sema tu siyo watu wa kulalamika.

Hivi unajua nurses wa diploma anayeanza kazi hafikishi Laki 5 kwa mwezi?

Wafanyakazi wenye mishahara mikubwa ni wale wanaofanya kazi kwenye mashirika maana huko mishahara yao hupangwa na bodi. Lakini wote wanaotegemea kima cha chini haku a tofauti kubwa ya ajabu.

Na kupata kazi huko kwenye mashirika siyo rahisi.

Tofauti kubwa iliyopo ni kwamba Ualimu hauna marupurupu+tips. Lakini Walimu wana muda mwingi sana.
 
Namimi nafuatilia kwa makini .wazoefu watusaidia mana uku maofisini tunatishwa na kukatishwa tanaa mno.
 
I
I correct you.

Halmashauri wenye mishahara minono ni afya.

Na wao ndio wanamarupurupu mengi kwasababu hela zao wao sio own source za halmashauri, zinatoka juu huko.

Japo mishahara ni midogo Ila afya afadhali.

#YNWA
 
I

I correct you.

Halmashauri wenye mishahara minono ni afya.

Na wao ndio wanamarupurupu mengi kwasababu hela zao wao sio own source za halmashauri, zinatoka juu huko.

Japo mishahara ni midogo Ila afya afadhali.

#YNWA
Afya madaraja yao ya misharaha ni tofauti lakini hakuna tifauti kubwa na elimu.

Mashirika wanalipwa zaidi hasa yale makubwa
 

Mishahara inatofauti san kaka mfano watu wa afya wao wako tofauti kabsa hayo ni maeneo ya kairuki miaka ya nyuma na utofauti wa afya na Ualimu

“Alisema kwamba mishahara huzingatia ngazi ya elimu, ambapo ngazi ya astashahada kwa upande wa Serikali Kuu ni Sh 390,000, kada ya walimu Sh 419,000, wauguzi Sh 432,000 na madaktari ni Sh 432,000.

Kwa upande wa stashahada, Serikali Kuu ni Sh 525,000, walimu 530,000 wauguzi 680,000 na madaktari ni Sh 680,000.

Kairuki alisema ngazi ya shahada kwa upande wa Serikali Kuu ni Sh 710,000, walimu 716,000, wauguzi 980,000 na madaktari ni Sh 1,480,000.”
 
Serikalini hawaajiri Postgraduate.
Postgraduate ni added advantage.

Nenda kasome bachelor ya hicho upendacho, then unaajiriwa upya/kubadilisha muundo/recategorization.

Mimi nibadilishiwa muundo kwasababu ya bachelor na hii masters ndio imenipa hiyo nafasi ya ukuu wa Idara.

Wewe unatakiwa kusoma bachelor mpyaa.

#YNWA
 
Gap kama Laki na ushee Mkuu, ndio utumie gharama kubwa kuitafuta hiyo tu
 

Kumbe ni mpaka nikasome upya nilijua nikifanya hivo itakuwa rahisi kufanyiwa recategorization kumbe ni shahada tu na vip kuhusu masters endapo nikisoma itakuwa msaada kwangu kuweza kubadili muundo
 
Kumbe ni mpaka nikasome upya nilijua nikifanya hivo itakuwa rahisi kufanyiwa recategorization kumbe ni shahada tu na vip kuhusu masters endapo nikisoma itakuwa msaada kwangu kuweza kubadili muundo
Inayoajiri ni bachelor.
Kuanzia hapo ni added advantage.

Mimi bachelor ndio imeniajiri Ila masters ikanipa shavu.

Ila bachelor ndio kila kitu.

Sio lazima uende Shule, unaweza kusomea open.

#YNWA
 

Unapotosha kiongozi
 
Acha kwanza huo Ualimu.
Njoo mtaani! Tukae kidogo halafu ujifunze Computer na ICT utapata connection ya Uhamiaji kirahisi sana mkuu.
Trust me!! Na akili itakukaa sawa.
 
mkuu pole sana na changamoto yako

Piaa pole na changamoto za sisi wakosoaji kwenye uzi wako. watu wamekosoa kwa sababu unainekana hujui unachotaka au kama unakijua umeshindwa kukielezea


Any way............


Elimu ambayo inakutambukisha kifani ni Degree. Hii ni muhimu sana.
Usijiangaishe na mambo ya post graduate hasa kama degree yako ya kwanza ni ya ualimu.

Fanya hivi, Soma Diploma potential ya kile unachokitaka, au kama una nguvu soma degree upya kabisa ndio uamze kutafuta ajira upya au kufanyiwa Recategorization

Pia kama hutojali, Jifunze fani ya udereva na uwe compitent uwe VIP driver halafu anza kuvizia nafasi za udereva kwenye Taasisi/ Mashirika ya umma. Huko kuna madereva wana hela hata maofisa wako hapo shuleni au wilayani hawatii mguu.

Kufanya icho nilicho kueleza haizidi mwaka mmoja kama utakuwa flexible.
 
Mkuu 713 haya yaliyosemwa hapa ni madini tupu. Zingatia na uyafuate ikiwa una nafasi na nia.
 
Pole sana mkuu kwa changamoto unazopata kutoka kwa wadau.

Naomba nikutaarifu kuwa kwa ngazi uliyonayo sasa( degree) ndio ngazi kubwa ya elimu inayotambuliwa na serikali. Ni ngumu sana hata kupata ruhusa kwa mwajiri wako kwenda kuchukua degree nyingine. Yaani akupe ruhusa ya miaka mitatu au minne? Ni ngumu.! Ruhusa unayoweza kupata wew ni ruhusa ya miezi isiyozidi 18, yaan wakiamini unaenda kujiendeleza kwa ngazi ya masters! Ungekuwa umeajiriwa na diploma ungekuwa na nafasi hiyo
ila kwa degree hapana!


USHAURI
Achana na mawazo ya kubadili hiyo fani kwani ni ngumu kupata ruhusa.
Jambo la msingi pambana ukasome Masters yoyote inayorelate na mambo ya uongozi na zaidi na zaid... Wakati huo kama utaweza jiingize kwenye siasa ya chama tawala uuze CV yako na
ili uweze pata connection mbalimbali ikiwemo kuteuliwa kuwa afisa elimu wilaya au mkoa!
 
Reactions: 713
Na kama yupo mji wenye vyuo anaweza kusoma hata diploma kwa kujiiba maana walimu wana muda mwingi tu kufanya yao.
Then akimaliza anaenda kubadili muundo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…