Kozi ipi nzuri kwenye soko la ajira?

mozeh

JF-Expert Member
Mar 13, 2022
494
952
Habari wana jukwaa..
Natumai mko poa, niende moja kwa moja kwenye dhumuni la uzi huu. mimi ni mwalimu niliyehitimu katika shahada ya ualimu mwaka 2015 katika masomo ya chemistry na mathematics ambae bado sijapata ajira.

Nahitaji kubadili fani kwenda kusomea kati ya kozi zifuatazo;
1. Diploma in clinical medicine(passion)
2. Diploma in marine and mechanical engineering
3. Diploma in radiography/radiology
4. Diploma in biomedical engineering
5. Masters of science in industrial chemistry

Naombeni ushauri wenu kozi ipi nzuri kwenye soko la ajira na malipo kati ya hizo tafadhali.
 
Mkuu me nakushauri uendelee kupambana tu, kusoma sana bila connection ni kupoteza muda unless uwe na Bahati.

Shahada uliyonayo ni kubwa sana. Lakini kama unataka kujiendeleza kusoma ili utimize ndoto zako kitaaluma (Sio kiuchumi) nakushauri ufuate passion yako CLINICAL MEDICINE
 
Pole kwa kuwa njia panda.
Nakushauri utambue kuwa tunahitaji kusoma ili tuelimike, na tukielimika tutaweza kufanya chochote.

Aliyeelimika atatizama mazingira na atajua cha kufanya kwa namna ya elimu yake.

Najua mtu aliyekuwa askari na hana cheti cha ualimu lakini anapenda sana Physics, Chemistry na Hesabu lakini ameacha Uaskari na kuanza kufundisha tuition.

Na sasa ana tuition center kubwa sana Ukonga na anaingiza pesa nyingi bila stress za kukamata mwizi wala kulinda banks.

Tafakari mazingira yako kisha tumia elimu yako kujikwamua.

(Tukisomea kazi tunapata tusivyotegemea mbeleni)
 
Back
Top Bottom