Nahisi sina bahati

Nahisi sina bahati

Pole my dear ... Naomba usifikirie hivyo labda uliokuwa nao before hawakuwa wako .. Subiri wako yuko njiani usiwe na haraka. Muda alioupanga aliye juu mbinguni ukifika hutajuta wala kuhisi hivyo unavyohisi.. pole sana mummy.. I feel your pain. . Jitahidi kutojiweka mpweke okay .. Thanks..
 
Angalia mwendendo wako.....
Angalia.pia aina ya wanaume unaochagua....unakua nao kwa kuwa umejiridhisha wanakupenda au kwa kuwa upo desparate kutafuta penzi... unachagua mwanaume mwema au bora liende....vigezo vipoje???
 
Pole my dear ... Naomba usifikirie hivyo labda uliokuwa nao before hawakuwa wako .. Subiri wako yuko njiani usiwe na haraka. Muda alioupanga aliye juu mbinguni ukifika hutajuta wala kuhisi hivyo unavyohisi.. pole sana mummy.. I feel your pain. . Jitahidi kutojiweka mpweke okay .. Thanks..

Hiyo yuko njiani unamtengenezea mazingira ya kuonjwa mwenzio
 
Kuwa makini na tabia zako, Usafi wako binafsi kimwili, Usiwe mtu wa kulia shida kilasiku kwa Mwanaume(Yule si baba ako), Now days wanaume hukinaishwa sana na mahusiano kutokana na Virungu. Usiwe muongeaji sana( Mropokaji/Maneno mengi) Hata kama ni mcheshi usipende kujichekesha kwa kila mtu hasa ukiwa na dushe lako pembeni.
 
Tatizo hili husababishwa na mambo haya;
1.Umejiona mpweke sana kiasi kwamba unatamani kila mtu ajue upweke wako,na wanaume wepesi wa kujua upweke wa mwanamke sio waoaji.Wakishakuonja wanasepa kutafuta mpweke mwingine.
2.Unajiheshimu au uliwahi kujiheshimu sana kwa sababu hiyo unakutana mwanaume ambao hawahitaji mke,akishakulala anakuonea aibu anakimbia.
3.Wewe ni perfectionist yaani unajiona umekamilika kila kitu,kiasi kwamba hata kuanzisha mahusiano huwa hutaki kujishauri mara mbili unaamini umekamilika.
Mimi nakushauri wewe na wengine wanaotaka kujifunza.Msichana ukishaamua kujiheshimu haijalishi umri wako utapata mume wako wa maisha.Kwa ulichosema hapo unasifiwa unajua mapenzi kwa msichana hiyo siyo sifa,ni sifa ya mwanamke aliyeolewa,kuwa mjuzi sana wanaume huamini kuwa unatoka na watu wengi hata kama huo ujuzi unamuonyesha yeye tuu.
Ondoa mawazo kuwa umri umeenda kwani hakuna umri sahihi wa kuolewa fuata mambo yako udhuria ibada heshimu watu wote usiwaze sana kuhusu why fulani ameolewa mimi bado utaangukia mikononi mwa mtu asiye sahihi hata kidogo.Be smart katika mambo yako utashangaa mume ankuja mwenyewe.
La mwisho unapokuwa kwenye uhusiano ishi kama girfriend not a wife.Tabia za kumpikia boyfriend,kumfulia na majukum mengine ya mke achana nayoo.Uatakuja kumpata ambae Mungu amekuandalia alafu utakuwa umechokaaaa.Pia usiamini huna bahati hii ni imani potofu ukiendelea kuamaini unavuta mambo ya mabaya katika maisha yako.
 
Poor good girls....sijui kwanini wanakuaga wanaumizwa na kutendwa kwenye mahusiano
pole mwaya
 
Ts not your problem ts theirs if they can't find the best in you.
 
Habarini wandugu. Mwenzenu nina tatizo ambalo linanikosesha raha kwa kweli kila ninapokuwa na mahusiano hayadumu kabisa na sielewi tatizo nini. Nikijitazama nipo mrembo, mcheshi na sina makuu. Na nasifiwa kwamba mapenzi nayajua lakini hakuna wa kunijali . Kunithamini wala kunipenda kama navyoona wenzangu, umri unasonga hakuna kinachoeleweka labda mnisaidie mawazo tatizo litakuwa nini wazalendo? Its serious problem i need help of advice
Wengine huwa mnadhani kwamba..
1. Urembo unapika
2. Urembo unafua na kufanya usafi
3. Urembo utakupa mwingine saa yoyote hivyo uliyenae akikuzingua unapiga chini
4. Urembo ndiyo uliokupatia uliye naye hence hata akiondoka mwingine atakuja
5. Uliye naye ana Bahati kuwa na wewe maana wewe ni mrembo sana
6. Urembo wako ndo kila kitu hence hubabaishwi na yeyote

Wengi mnababaishwa sana na urembo na matokeo yake urembo ukififia tu unaanza kuhangaika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom