Nahisi maisha yamenipiga vibaya mno hadi naona aibu

ameen
 
Acha kufatilia maisha ya hao marafiki zao na rika lako kwa ujumla.

Kwa kuacha kuangalia what's up status zao.(HAPA UNAWEZA KU MUTE AU UKASAVE NAMBA ZAO PEMBENI)

Kuacha kuulizia kuhusu maisha yao.

Kuacha au kupunguza kutumia mitandao ya kijamii itakayo fanya kukutana na post zao au kuona pia mfano Facebook na Instagram.

HAPO UTAKUTA MTU ANA POST YUKO KWENYE DUALIS caption Ina someka way to TANGA for weekend halafu akifika ana post nyingine akiwa kwenye restaurant Kali akipiga launch akiwa na mtoto mkali wa kidigo ana kwambia amefika salama.Muda huo wewe unapigana na shemeji akuachie ukoko wa wali siku nyingi ume umiss
. Lazima u frustrate!!!

Focus kwenye maisha yako,maisha yako Sasa hivi ni kusoma.Hakikisha una pigana kweli kweli Kwa kupata marks nzuri kuepukana na supp zisizo za msingi ma Repeat module yasiyo na lazima hata ku disco pia na mwisho upate GPA nzuri Umalize diploma Yako fresh.

Usiache kabisa ila punguza kuwasiliana nao kama hakuna ulazima acha kabisa kuwasiliana nao,Hii itaepusha kuambiwa mipango Yao ambayo wewe itakutoa kwenye reli na kukuongezea stress zaidi.Mfano jamaa akupigie simu ana enda Dodoma kuangalia Nyumba anayo taka kununua milion 78, ana mashamba Morogoro karibia ekari 30,ana mpango wa kuongeza gari jingine mwezi wa 10 maana kluger v kaichoka na vingine vingi.

Heshimu kila mtu si mkubwa siyo mdogo na kuwa mwaminifu pia,Hii itakutengenezea kesho yako nzuri especially Kwa kupata connection Kwa future Yako mbeleni.

Wakati wa likizo ndefu unaweza kutafuta kitu Cha kukuongezea ujuzi zaidi nje ya fani unayo somea Yote ni Kwa ajiri ya kesho yako na kuacha kushinda kwenye social media kufatilia maisha ya watu Ingali ya kwako ameyashika shemeji Yako.

Epuka kumpa ujauzito mwanamke yeyote kuepusha mzigo maana wewe hapo ulipo ni mzigo Kwa kaka Yako.

Usimwamini mtu yeyote Kwa kumwambia mambo yako au mipango Yako kama hakuna ulazima wowotee wa kufanya hivyoo,Bora mnyama kuliko mtu.


kubwa kuliko ni MAOMBI,SALA NA DUA.

Lakini Kaa ukijua maisha haya formula,
 
25yrs unalialia watu wamegonga 40yrs na bado hawaoni Njia your still younger bado una muda mwingi mno
 
Mkuu umenena vema sana
 
Point mzee wengi wanadaiwa kodi washenzi kuleta inferior complex kwa wenzao
 
ushauri murua sana huu.
 
Umeongea point sna mkuu nimekukubali una akili mno
 
Life start at 40.
Nani kakwambia kuna kuwahi au kuchelewa kwenye maisha.Maisha sio mashindano,maisha yana mipangilio yake sisi tunafata vile ambavyo inatakiwa tuwe na sio vile tunataka tuwe.
 
Tatizo lako unajilinganisha na wengine..hapo ndipo shida inapoanza..kua wewe..simama katika malengo yako na usiache kumuomba Mungu
 
Mkuu tupo wengi umri huo huo sema umenizidi elimu, nami nimepigika na maisha mkuu hali ninayokutana nayo da!?
Tafuta maarifa zaidi kuhusu maisha na jinsi ya kujinasua na ugumu,au shida zozote utafanikiwa.
 
Ameen
asante kwa ushauri
 
Angalia malengo yako. Usijilinganishe na wengine, kila mmoja na safari yake.
Stay strong.
 
Run your own race .kujicompare na watu kulinifanya niloose Kila kitu n direction
 
Mwanangu sikia maisha hayapo hivyo kabisa yan futa kichwan mwako kama umechelewa.bado upo ndani ya muda kabisa unga unga aisee ipo siku unatoboa.! Usijilinganishe utajipa stress bureeeee huenda unaejilinganisha nae na yeye ana stress bora hata wewe .usione mtu kapendeza ukaona kakuzidi maisha sio kweli mazeee.mfano kuna rafiki zangu ni wafanyakazi ila kina wabeba ile tittle tu ni wafanyakazi ila maisha yao ya kawaida mno.Nimejifunza kuwa kazi na rizki ni tofauti mzeeee ww tulia unatoboa one day yes..........
 
Tofauti ya mtu anayejiamini na mtu asiyejiamini:

Mtu asiyejiamini anaishi kwa kuangalia watu wanasemaje kuhusu yeye, lakini mtu anayejiamini anaishi kwa kuangalia mambo yake, hajali watu wanasemaje kuhusu yeye!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…