Nahisi maisha yamenipiga vibaya mno hadi naona aibu

James Hadley Chase

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
1,565
2,638
Mpaka sasa nina miaka 25 ndio kwanza nipo Diploma mwaka wa kwanza Semester ya 2 inaanza tarehe 4 Aprili 2022. Bado nakaa na kaka yangu japo naye ana familia yake.

Najihisi kama nimechelewa kuanza maisha vile, nimesoma kwa kuungaunga tu, washkaji na rafiki zangu niliomaliza nao sekondari mwaka 2014 wengi wao wameoa, wengine washaolewa.

Yaani nikionana nao au kupishana nao njiani ni aibu tu, bora tuishie kuchati tu kupitia aidha sms, WhatsApp, Facebook. Nipo tu kama digidigi vile sina hili wala lile.

Hata akiba sina, siugui ovyoovyo. Siku nikitimuliwa home sijui itakuwaje. Japo Sir God analinda ile mbaya.
 
Kwny maisha hakuna kuchelewa wala kuwahi bro. Siku zote maendeleo ni hatua moja kwnda nyngne kiakil.kimwil na kiroho na si kujicompare na watu wengine.

Kuwa karibu na Mungu wako wekeza katika akili yako kila siku na kuwa boraa ww kama ww jiwekee malengo mafup SMART objective zipambanie uzifanikishe.
 
Kwny maisha hakuna kuchelewa wala kuwahi bro. Siku zote maendeleo ni hatua moja kwnda nyngne kiakil.kimwil na kiroho na si kujicompare na watu wengine...kuwa karibu na Mungu wako wekeza katika akili yako kila siku na kuwa boraa ww kama ww jiwekee malengo mafup SMART objective zipambanie uzifanikishe
 
Usikate tamaa...life start at 40

Robertson beki wa Liverpool alikata tamaa kipindi flani lakini sasa hivi anamafanikio makubwa
Screenshot_20220322-124719.jpg
 
Mpaka sasa nina miaka 25 ndio kwanza nipo Diploma mwaka wa kwanza semester ya 2 inaanza tarehe 4 Aprili 2022. Bado nakaa na kaka yangu japo nae ana familia yake.

Najihisi kama nimechelewa kuanza maisha vile, nimesoma kwa kuungaunga tu, washkaji na rafiki zangu niliomaliza nao sekondari mwaka 2014 wengi wao wameoa, wengine washaolewa.

Yaani nikionana nao au kupishana nao njiani ni aibu tu, bora tuishie kuchati tu kupitia aidha sms, WhatsApp, Facebook. Nipo tu kama digidigi vile sina hili wala lile.

Hata akiba sina, siugui ovyoovyo. Siku nikitimuliwa home sijui itakuwaje. Japo Sir God analinda ile mbaya.
Kwenye Maisha Hilo ni jambo la kawaida sana, muhimu kuwa na subra tu, utakuja kusahau yote hayo.

Mimi nimeanza maisha late sana (35yrs) ndio niliajiriwa. Japo Nilikuwa hvyo hvyo kusoma kwa kuunga Unga.

Lakini Sasa hivi (38yrs) Nina watoto wawili Ke/Me nafurahia maisha kama hakijatokea kitu.

Mke wangu Ana (31yrs) ni Graduate since (2015) BA Ed, no ajira no Biashara, yuko home analea kwa Aman. Alhamdulillah
 
25 ndo unapata presha? Mjomba wengine ghorofa ya tatu tushaingia na bado ramani imeloa.

Natamani nikupe moyo, lakini bora ukweli tu. Ukweli ni kua, huko mbeleni ndo unaeza kukutana na magumu zaidi ya sasa ukajikuta unadata kabisa.

So inshort, don't worry about the future, focus na ulichonacho saa hii, perfect it in every way you can. Hakuna blueprint ya life. Inatokea inavotaka. Find pleasure and happiness in the little things.

Never ever compare yourself na hao wengine, because hujui wanachopitia. Ungepewa maswaibu yao inaezekana tungekukuta Mirembe.

Angalizo: ukiuza "jicho" hakuna pasi ya kunyoosha marinda tena. Kaa chonjo
 
Back
Top Bottom