Nahisi leo ndo nimeona chuma ulete live

Nahisi leo ndo nimeona chuma ulete live

Je ukizidishiwa chenji na huna hayo mambo ya chuma ulete ni ishara Gani?manake Kuna cku Niko Mafinga napanda bajaji za kwenda kinyanambo ni 800,kufika nampa elf mbili dreva katurudisha elf tisa mia mbili,nkamwambia umezidisha hataki kunielewa ,nkamwambia nlikupa elf mbili , ndo abiria alikua hajashuka akanisaidia kumuelewesha dereva kuwa ni kwel aliniona nkitoa elf mbili. Nkamrudishia chenji yake yote. ..
Alikua anafanya installation huyo kwenye wallet yako, si kwamba alijisahau😂😂. Usiamin kila unachokiona ukadhan ndivyo kilivyo..hil ndio somo nimejifunza kwenye maisha so far
 
Nimewahi msaidia mtu mlemavu ambaye alikuwa ombaomba Jijini Mwanza nikiwa kwenye mgahawa mmoja napata msosi akaja na kijana wakiwa wanaomba!

Nilitoa elfu 3 nikampa yule dogo akiwa na yule mlemavu,Sasa kumbe pale wanamfahamu na watu huwa hawawapi hela,ajabu ni jamaa hawakunishitua!

Hadi muda huo naingia hapo mgahawani kupata msosi mfukoni nilikuwa nina 360000/- baada ya kupiga msosi nimemaliza nachomoa pesa nilipe,kwanza nikahisi mfukoni kumekuwa kwepesi ghafla,ikabidi nitoe zile pesa Ili nifanye malipo ya Chakula!

Nilipo hesabu pesa nakuta elfu 80 haipo,nilihisi kuchanganyikiwa,ikabidi nihesabu upya lakini bado hiko kiasi kikawa hakipo!,baadae ndiyo watu wananishitua wananiambia yule jamaa mlemavu na yule dogo niliowasaidia huwa hayo ndiyo mambo Yao!,na raia wengi wanawafahamu hivyo huwa wanawaangalia tu hawawapi chochote!

Tangu siku hiyo nilijifunza kitu😁
Haya mambo yapo ila sisi wenye elimu ya kukariri maphysics na mabiology huwa ni wabishi sana

Ndo maana unapofanya biashara ni muhimu kwenda kwa waganga kuzuia mambo kama hayo
kuzuia tu au kuingia mzimamzima?
 
Chuma ukete ipo sanaa....kuna wazee ikifika saa 12 ....watu wanagoma kuwauzia chochote.....hasa mitaa Goba Msumi Mabwepande hadi Bunju.....wamejaa waswahili huko balaaa sanaaa....hata stand mbezi ma bus shamba....
 
Nimewahi msaidia mtu mlemavu ambaye alikuwa ombaomba Jijini Mwanza nikiwa kwenye mgahawa mmoja napata msosi akaja na kijana wakiwa wanaomba!

Nilitoa elfu 3 nikampa yule dogo akiwa na yule mlemavu,Sasa kumbe pale wanamfahamu na watu huwa hawawapi hela,ajabu ni jamaa hawakunishitua!

Hadi muda huo naingia hapo mgahawani kupata msosi mfukoni nilikuwa nina 360000/- baada ya kupiga msosi nimemaliza nachomoa pesa nilipe,kwanza nikahisi mfukoni kumekuwa kwepesi ghafla,ikabidi nitoe zile pesa Ili nifanye malipo ya Chakula!

Nilipo hesabu pesa nakuta elfu 80 haipo,nilihisi kuchanganyikiwa,ikabidi nihesabu upya lakini bado hiko kiasi kikawa hakipo!,baadae ndiyo watu wananishitua wananiambia yule jamaa mlemavu na yule dogo niliowasaidia huwa hayo ndiyo mambo Yao!,na raia wengi wanawafahamu hivyo huwa wanawaangalia tu hawawapi chochote!

Tangu siku hiyo nilijifunza kitu😁
Roho mbaya ni kinga

Wema wangu umeniponza sasa machungu ya Dunia nayaona-Ferooz
 
Yaani nineenda dukani (kutoa hela kwa wakala maana ni muuza duka na wakala hapo hapo.nimekuta anahudumia watu wengine ikabidi nikae pembeni kwanza amalizane nao, sasa wakati nimetulia pembeni akaja mbabu kavaa kote barakashia tena inechanika chanika nimemsalimia hajaitiika hata.akamwuliza yule muuza duka nitapata chenji?

Muuza duka akamwambia sina checji babu! Yule mzes akamwambia basi nipe juice nimpelee mjukuu wangu ananisumbua sana,babu akanitizama machoni huku anatoa hela mfuko wa koti ule wa ndani.

Yule jamaa akatoa juice ya box ile ndogo akampa babu na yule babu akatoa shilingi elfu 2 akampa jamaa muuza duka.

Mimi hapo kimoyomoyo niokajiulizaina maana amaekuja kuomba chenji ya ya 2000 tuujioni hii ya nini?nikatulia,wakati huo yule muuza duka kashapokea hela nikaona anarudisha chenji 9500 moyo wangu ukafanya paaa!!!

Babu kapokea vhenjiakamwambia jamaa asnantee!jamaa nae akasema sawa babu karibu tena,babu huyooo kaondaka,mi nikamwambia jamaa mbona babu kakupa elfu 2 wee unamrudishia chenji elfu 9500 kulikoni?jamaa wa dukani huwezi amini kakataa katu katu kasema elfu kumi yaani nimebishana nae mpaka watu wakatishangaa nikatoa hela yangu huyio jikatimka ila jamaa nimemwonea huruma sana.
Aise kumbe hii ishu ipo tuweni makani
Kuna mji fulani (sitaji jina) hapa Tanzania ukiomba chenji kwenye duka lolote hawakupi (hawatoi chenji). Siku hiyo nilihangaika sana kupata chenji ya Tshs elfu kumi.

Yaani nilipokuwa nikiomba chenji, kabla muuzaji hajanijibu kama chenji ipo au La! ananitazama usoni kama kwamba tuliwahi kuonana sehemu kisha anajibu; "bro sina chenji".

Mwenyeji wangu akaniambia; "mji ule ambaye angenipa chenji ni mgeni wa biashara katika eneo lile". Eneo hilo wanapeana chenji wafanyabiashara wenyewe, kwasababu wenyewe wanajuana fulani yukoje (ni mbaya au mzuri).

Uchawi upo!
 
Siku moja kibabu kilinunua panado za 1000, akatoa 2000, kidogo nirudishe 9000, nikamuuliza, babu umenipa ngapi, akadakia "si uliiona? Nikarudisha nikampa 1000, kakasonya na kuondoka. Haya mambo yapo, muwe macho. Kuna watu wanaishi kwa kazi hiyo. Kutwa nzima kucheza bao, jioni anazunguka madukani.
 
Je ukizidishiwa chenji na huna hayo mambo ya chuma ulete ni ishara Gani?manake Kuna cku Niko Mafinga napanda bajaji za kwenda kinyanambo ni 800,kufika nampa elf mbili dreva katurudisha elf tisa mia mbili,nkamwambia umezidisha hataki kunielewa ,nkamwambia nlikupa elf mbili , ndo abiria alikua hajashuka akanisaidia kumuelewesha dereva kuwa ni kwel aliniona nkitoa elf mbili. Nkamrudishia chenji yake yote. ..
We mchamungu sana ila sirudishagi maana wenyewe makonda wanatuibia sana chenji zetu kwa makusudi kabisa.
 
Je ukizidishiwa chenji na huna hayo mambo ya chuma ulete ni ishara Gani?manake Kuna cku Niko Mafinga napanda bajaji za kwenda kinyanambo ni 800,kufika nampa elf mbili dreva katurudisha elf tisa mia mbili,nkamwambia umezidisha hataki kunielewa ,nkamwambia nlikupa elf mbili , ndo abiria alikua hajashuka akanisaidia kumuelewesha dereva kuwa ni kwel aliniona nkitoa elf mbili. Nkamrudishia chenji yake yote. ..
Daah Kinyanambo kitambo sana iyo kipindi iko bajaji 500 to mafinga
 
Ulikuwaje ukaona ile ni elfu mbili wakati wenzio wanaona ni liteni?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom