Nahisi kufa kufa; unapata wapi nguvu ya kumwacha umpendae?

Nahisi kufa kufa; unapata wapi nguvu ya kumwacha umpendae?

asante ilanaumia sana...sijawahi hata mcheat...nilimpa moyo wangu woooteeee...nayeye nlimwamini sana...bora hata angekua muhuni...ila kinachoniuma hajawahi nionesha hata dalili...
Hilo ndo kosa kubwa sana huwa mnafanya usijaribu kumpa mtu moyo ndo maana mnalizwa kila Leo hebu jaribu kumpa akili tu tena robo
 
wewe unaonekana mjuaji sana. hakuna mwanaume ambaye anapenda kulekebishwa lekebishwa sana yaonekana ww ulikuwa unataka awe perfect, kajaribu kuwa hivyo kwa kipindi hiko chote ila sasa kaona imetosha kuigiza tena basi. mwanaume wa wapi eti hanywi, havuti afu siyo mzinzi labda yesu.kachoka kuwa unavyotaka wewe, sasa anataka kuwa yeye mwache kijana wawatu awe huru
 
Binti yangu Pole Sana. Umefanikiwa kufanya kwa sehemu yako, acha nature ichukue mkondo wake but hakikisha you remain true to yourself!! The greatest love of all is learning to love yourself by Whitney Houston
 
kuna kitu amekuficha kuna mahali hapakuwa sawa na huenda alikuwa msiri sn cha kukusaidia kwanza 1. jithamini sana kwamba wewe ni kila kitu 2.acha kukaa peke yako .3 ingia internet usome vitu muhimu ambavyo huwa unapanga ktk maisha yko .4 usijiingize kwenye uhus
iano mwingne kimapenzi ktk kipindi hiki .5 kama utanawajua
rafiki zke wa krb huyo bf wko jaribu kuwauliza ni kwanini mpnz wko ameamua kukuacha.6 fanya mazoezi ya kutosha ili kupata usingizi mzuri

mwisho pole sn mapenzi ndvyo yalivyo hakuna ambaye hajawahi kuumizwa ktk mapenzi ila ndo kujifunza
 
Afuu kama hunaa Helaa girl wakoo anakupa Akili na mipango ya kufanya mishee lakini sasa Mfukoo hauruhusuu..
Ukiwa kidume ni kidume tu mambo ya kuwa huna kitu hafu demu anacho nitamshiiiti kistaili yaani kutumia hela ya demu kbs huwa najisikia kukosa nguvu ya kiume


Ila nikitoa kitu najiamin balaa naweza shuka milima na mabonde mpk aseme baaaaaas
 
pole sana.Ila usijilaumu sana wala kujiuliza maswali mengi.
Tatizo sio wewe,tatizo ni yeye.
Kuachwa ndio ukubwa.Utampata mwingine utampenda zaidi ya huyo.
Usijitese kwa kuombolezea penzi,utaumwa mwenzio anaendelea na maisha yake.
Just Let It Go,wala usikufuru!
 
kuna kitu amekuficha kuna mahali hapakuwa sawa na huenda alikuwa msiri sn cha kukusaidia kwanza 1. jithamini sana kwamba wewe ni kila kitu 2.acha kukaa peke yako .3 ingia internet usome vitu muhimu ambavyo huwa unapanga ktk maisha yko .4 usijiingize kwenye uhus
iano mwingne kimapenzi ktk kipindi hiki .5 kama utanawajua
rafiki zke wa krb huyo bf wko jaribu kuwauliza ni kwanini mpnz wko ameamua kukuacha.6 fanya mazoezi ya kutosha ili kupata usingizi mzuri

mwisho pole sn mapenzi ndvyo yalivyo hakuna ambaye hajawahi kuumizwa ktk mapenzi ila ndo kujifunza
Mie sijawahi kuumizwa
 
Ukiwa kidume ni kidume tu mambo ya kuwa huna kitu hafu demu anacho nitamshiiiti kistaili yaani kutumia hela ya demu kbs huwa najisikia kukosa nguvu ya kiume


Ila nikitoa kitu najiamin balaa naweza shuka milima na mabonde mpk aseme baaaaaas
Haa ha ha...!! Ofcoz kama huna pesaa ni msalaa
 
You are not his cup of tea. Amekutana na ampandae zaidi. Pole sana
 
habari zenu jf...
kwanza kabisa mimi ni KE msishange hii ID...(ni jina lilonijia kwa haraka...mana aliekua mpenzi wangu ni Leo sign)
Am heart broken mwenzenu...mpenzi wangu KANIACHA
nimedumu naye kwa mwaka mmoja na nusu...

Jamani alinipenda sana na hajawahi kuonesha hata dalili za kucheat...mda wote simu yake nashika plus matendo yake kabisa yanaonesha he is honest...yani tangu siku ya kwanza kaniona akanitongoza yani mpaka mwisho wetu everything was too real yani...

Nilimpenda pia tena sana...nashangaa tu from nowhere ananiambia hatuwez kua pamoja tena...nkimuliza why anasema hataki kuoa kwa sasa...namwambia am okay with that hata usiponioa nataka tu niwe na wewe mana ndo furaha yangu...anasema hataki kunipotezea mda...akaniblock kote kote...kwa madai itanisaidia mm kumove on...

Dadangu alimpigia simu akamjibu kua hata ye inamuuma ila anataka kua single kwa sasa kuna vitu anataka atimize kwenye maisha yake so inamuhitaji awe single...nililia sana hadi hapa naandika nalia...naumia sana...

Hana kazi tumemaliza wote chuo...kuna mda alikua anasema kuna vitu natamani nikupe ila sina uwezo inaniuma...namwambiaga you know me better...nakuelewa na pesa sio kikwazo tutatafuta tutapata tu...hua nampa moyo hata matangazo ya kazi namtumia...plan za biashara pia hua tunaongelea...

Najiuliza maswali mengi sana kwa upendo mkubwa alonionesha amepataje nguvu ya kuniacha[emoji24][emoji24][emoji24]...na kuniumiza mimi...alisema me ndo furaha yake...sasa why aniache...he was so honest..loving...sio muhuni...hanywi..havuti...yani tuliendana sanaaa..yani kuna mda pia nilikua nasema this is too good to be true...

Guys niambieni how many heartbreaks does it take mpaka kupata the right one...huyu ni mwanaume wangu wa pili but nilimpenda sana kuliko wa kwanza we were just too perfect yani...kinachouma zaidi hatukugombana kusema kwamba ndo aniache...hata hakuna kosa nlilofanya...

Nawaomba msinikejeli please...niko katika wakati mgumu...nahitaji faraja zenu...
Pole sana dear, ila kuna kitu lazima ukielewe, yaweza kuwa ndiyo alikuwa na upendo kwako na sasa kapata mwingine ambaye anamuona anafaa na kuona wewe humfai tena.

Iliwahi kunitokea pia, yaani from no where mtu anakuuliza "nikikuacha utaumia"? Na anakwambia sababu ya kufanya hivyo anataka akamilishe mipango yake ya kimaisha ikiwa ni pamoja na kujiendeleza zaidi kielimu.
Na kudai kwa muda huo hana uwezo wa kutoa mahali, nikamtia moyo kuwa kuhusu mahali asijali mie ntawapanga home fresh[emoji2] [emoji2] ni vile nilikuwa nampenda sana. Kumbe alikuwa kaishapata kitu kipya bwana.

Hivyo usikiamini sana anachokwambia, yote yanawezekana.
 
Kuna jambo niliwahi kufanya Kama hilo, tulikua UDSM mwaka wa nne, nikiwa semester ya pili mwaka wa tatu nikapata Mdada, akanipenda saana, na Mimi Kama binadamu Nikaanza pia kumpenda, aliishi Hall three then mwaka wa nne akawa Mabibo Hostel. Penzi letu likakua saana, Lazima Jumapili anisubiri Tuingie wote Ibadani tulikua wote CCT. Tukitoka Tunakwenda Room kwangu Hall Six. Tunanunua vitafunwa tunakwenda tunashinda Room hadi jioni, namsindikiza! Yalikua maisha mazuri sana ila watu wa Karibu walisisitiza kuwa, Elli huyu mtu hakufai!! Hali hii ilipenya taratibu na bahati mbaya na Mimi nilikua na mtu wangu wa miaka na miaka!

Naumia Sana maana nilimuumiza sanaa Sana!! Niliumia kumuacha ila sikua na namna! Pole binti, sasa Hivi sisi tumebaki kuwa Marafiki na kila tunapokumbushia mapenzi yetu kwa simu, maumivu huanza upya! Please Popote ulipo naomba Nisamehe saaana!
 
Pole sn mpnz kwa maumivu,lkn usihamaki sn embu tulia umskilizie kwanza huenda anakutega ili auone msimamo wako au ana sababu nyingine tofauti na hiyo alokueleza ispokuq anahitaji muda.
Hayo ndio Mapenzi bhn alafu anakuacha kwenye tar mbaya namna hii[emoji36][emoji36]Mungu anamuona wallah
 
Back
Top Bottom