haina noma kaka lakini bado nampenda nilishajaribu kuchepuka lakin wapi still in my mind
Kama nakuona vile maumivu unayoyapata, hasa pale unapompigia simu asipokee au unakuta iko bize halafu ukimpigia baadae hapokei...
Kweli ni ngumu kusemea moyo wa mtu, lakini sio mbaya nikukuacha na machache yatakayo kupa muongozo, kama hayatakusidia wewe basi yatamsaidia mwingine.
Kwanza kabisa katika maisha yako usimtegemee binadamu mwenzako,kama ni mapenzi hayakuanzia kwako.
Kisha yakupasa kuelewa kwamba hauwezi kumlidhisha binadamu mwenzako kwa kila kitu.
Usisahau kwamba yule ni binti anakumbana na changamoto mbali mbali kutokana na mazingira anayokwenda.
Safari yenu ya mahusiano ilianzia chuoni wakati huo mkiwa na yale mawazo ya kianafunzi, usisahau akili na mitazamo hubadilika kutoka na muda unavyosongea, ulikuwa unafaa sana wakati ule mko chuo je, katika wakati huu wa maisha ya kiraia bado thamani yako iko pale pale? hilo ni swali kwako.
Nakupa na kisa kidogo kilicho wahi kunikuta.
Kunabinti mmoja nilikuwanae katika mahusiano ndani ya miaka mitano.
Wakati wa masomo yake ya chuo nilikuwa namsupport wakati huo tayari nilikuwa na ajira, hivyo kuna majukumu kadhaa nilijitwisha.
Baada ya masomo likaja swala la kazi hilo pia nikalisimamia, alipopata kazi ikawa nimateso tena kwangu, visa vikawa havikatiki, unajifanya yuko bize kuliko hata ubize wenyewe, kupokea simu nitabu,kuonana ni kama mshahara wa mlinzi ktk kampuni mwezi huu mtaonana na mwezi mwingine unapita, baada ya uchunguzi nikagundua kuna mtu natokanae pale kazini, nikarudia msemo mmoja wa wahenga kwamba tenda wema nenda zako, nikaamua kumuacha maada ya maumivu ya muda mrefu, kilicho kujakumpata ni aibu ya mwaka, mpaka leo katika maisha yake hato ni sahau, alitamani kuwa na mimi tena lakini ndiyo hivyo nafasi ikawa ilishapotea...
Kila jambo linalotokea linakuwa na sababu ya kulifanya litokee!
Hivyo hata huyo shemeji yetu anachokitenda sasa hivi kinasababu nyuma yake.
Anaekupenda katika maisha yako niyule aliekubeba tumboni miezi tisa, kisha akakuleta duniani kwa njia ya maungo yake. alietesaka na kuvuja damu nyingi kwaajili yako.!