Nahisi kuachwa msaada wa mawazo tafadhali

Nahisi kuachwa msaada wa mawazo tafadhali

mmmmh kiongozi usijaribu kumwacha msichana kama unampenda huwa watu wakiwa mbali mambo kama hayo niya kawaida sana, chakufanya zidisha kumpenda na kumsumbua kwenye mawasiliano atajifunza tu na uwe unakusanya mkwanja na kwenda kumtembelea mara kwa mara na ruhusa unamwomba yeye then umueleze unavyoteseka kwa yeye kuwa mbali na wewe. Simu utaimba sana ila hali itajirudia tu udhaifu wa hawa viumbe ni ana kwa ana tu na unamweleza huku ukiwa unamwangalia kwenye macho you will know kweli kama huyu still anakupenda au vipi. Ikishindikana usimwambie chochote na wewe kata mawasiliano akiwa kimya au kutokulalamikia ujue atakuwa keshapata wa kumweka bussy.

Mimi ni mwanamek lakini huu ushauri wako nina upinga
 
Kama nakuona vile maumivu unayoyapata, hasa pale unapompigia simu asipokee au unakuta iko bize halafu ukimpigia baadae hapokei...

Kweli ni ngumu kusemea moyo wa mtu, lakini sio mbaya nikukuacha na machache yatakayo kupa muongozo, kama hayatakusidia wewe basi yatamsaidia mwingine.

Kwanza kabisa katika maisha yako usimtegemee binadamu mwenzako,kama ni mapenzi hayakuanzia kwako.
Kisha yakupasa kuelewa kwamba hauwezi kumlidhisha binadamu mwenzako kwa kila kitu.
Usisahau kwamba yule ni binti anakumbana na changamoto mbali mbali kutokana na mazingira anayokwenda.
Safari yenu ya mahusiano ilianzia chuoni wakati huo mkiwa na yale mawazo ya kianafunzi, usisahau akili na mitazamo hubadilika kutoka na muda unavyosongea, ulikuwa unafaa sana wakati ule mko chuo je, katika wakati huu wa maisha ya kiraia bado thamani yako iko pale pale? hilo ni swali kwako.

Nakupa na kisa kidogo kilicho wahi kunikuta.

Kunabinti mmoja nilikuwanae katika mahusiano ndani ya miaka mitano.
Wakati wa masomo yake ya chuo nilikuwa namsupport wakati huo tayari nilikuwa na ajira, hivyo kuna majukumu kadhaa nilijitwisha.
Baada ya masomo likaja swala la kazi hilo pia nikalisimamia, alipopata kazi ikawa nimateso tena kwangu, visa vikawa havikatiki, unajifanya yuko bize kuliko hata ubize wenyewe, kupokea simu nitabu,kuonana ni kama mshahara wa mlinzi ktk kampuni mwezi huu mtaonana na mwezi mwingine unapita, baada ya uchunguzi nikagundua kuna mtu natokanae pale kazini, nikarudia msemo mmoja wa wahenga kwamba tenda wema nenda zako, nikaamua kumuacha maada ya maumivu ya muda mrefu, kilicho kujakumpata ni aibu ya mwaka, mpaka leo katika maisha yake hato ni sahau, alitamani kuwa na mimi tena lakini ndiyo hivyo nafasi ikawa ilishapotea...

Kila jambo linalotokea linakuwa na sababu ya kulifanya litokee!
Hivyo hata huyo shemeji yetu anachokitenda sasa hivi kinasababu nyuma yake.

Anaekupenda katika maisha yako niyule aliekubeba tumboni miezi tisa, kisha akakuleta duniani kwa njia ya maungo yake. alietesaka na kuvuja damu nyingi kwaajili yako.!

Nashukuru kwa maneno yako mkuu kiukweli nimepata relief ya Ajabu
 
likuepukalo lina kheri kwako. Hii nimeipenda" na Sio kila unachokiona kinakupendeza ukajua ni heri kwako. Ila mi kuna nilichopenda zaidi. Labda kitakuwa ni heri kwangu( ushungi kwenye avatar)

Hahahahaaaa haya mkuu
 
miezi miwili hamkuwasiliana asije akawa keshapata replacement


Apate mara ngapi tena?hapo ni kutafuta sababu ya kuridhia tu
 
Mapenzi bana ni mambo ya ajabu sana. Leo anakupenda kesho hakupendi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom