Nahisi kifo changu kitatokana na kupigwa risasi

Nahisi kifo changu kitatokana na kupigwa risasi

Obsessive-Compulsive Disorder (OCD) is a common, chronic and long-lasting disorder in which a person has uncontrollable, reoccurring thoughts (obsessions) and behaviors (compulsions) that he or she feels the urge to repeat over and over.

See a psychiatric specialist immediately.

Be blessed.
 
Acha kuangalia movies za kupigana/kivita zenye milio ya risasi kwa wingi,sikiliza slow jams kwa wingi au audio za kurelax mind,tuliza nafsi yako fanya maombi,jichanganye fanya issue zingine ukiamini utaishi maisha marefu,usipende kukaa na ukimya muda mrefu,
Hio ya kuogopa ukiwa ghorofani, fear of Heights wanayo wengi hata me sipendi kuangalia chini from a high building, ikinilazimu nafumba macho mf kwny lifti za kioo,..au I opt kutokwenda huko juu nk
 
2pac au!!?

Ukiisha kwa upanga utakufa kwa upanga mkuu.. Na mashaka na job yako mkuu, nadra sana kwa mkulima kufia baharini.
 
Heshima kwenu wakuu,

Naamini JF kuna wajuzi wa mambo ambao wanaweza kusaidia kushauri na mengine mengi tu.Kwa miaka mingi sana nimekuwa nasumbuliwa na hisia mbaya kichwani mwangu ambazo kwa kweli zinanikosesha raha na amani.Nimekuwa kila nikikaa mahali nahisi kama kuna mtu anakuja na silaha(bastola),anani-shoot na kuondoka.

Hali hii huwa inanitokea hata nikiwa nyumbani peke yangu nikisikia kitu kimegonga mlango au kimedondoka basi haraka hushtuka na kuanza "kunyata"kuelekea mlio ulipotokea kwa umakini mkubwa kujiridhisha kama kuna usalama

Hali hii imenifanya nisiweze kukaa milango wazi hata mchana huwa nikiwa nyumbani najifungia milango yote.Nimevumila kwa muda mrefu lakini nimeona leo nifunguke kwa wataalamu wa mambo hapa JF nikiamini naweza kupata msaada wa mawazo,maana inawezekana ikawa najitabiria kifo changu(Japokuwa sina imani hiyo).

NB:Sina ugomvi wala uadui na mtu,na ni raia safi tu!
Wengi tu tupe hivyo MI nikiangalia movies huwa Yale matukio ya KUOGOFYA yanabaki ubongoni mwangu nakuwa the km wewe
 
Kuna watu humu wameniuliza maswali yafuatayo,nitajibu ninayoyakumbuka:

1:Kuoa/kuolewa
-Nimeoa na nina mtoto mmoja.

2:Nishawahi kuua?
-Hapana wala sijafikiria.

3:Kazi gani nafanya?
-Mjasiliamali

4:Nina mali kiasi gani?
-Za kawaida,nimepanga japo ndio nipo kwenye ujenzi wa makazi yangu.

5:Umri wangu
-Miaka 35

Nadhani baadhi nimeyajibu.Kuna mmoja amenambia inawezekana nina ugonjwa/tatizo linaloitwa Phobia,ngoja ni Google nione maana kuna jambo lingine huwa mara nyingi hunitokea sana sana nikiwa kwenye majengo marefu juu huwa nahisi kama mwilini kuna vitu vinanitokea halafu nahisi mawazo ya kujirusha.Kuna jamaa alinieleza nina tatizo la hiyo phobia,sasa leo nimepata ushauri mwingine kuhusu hiyo kitu ngoja nicheck.Ahsanteni kwa wote mlionishauri!
Mkuu hayo ni maradhi ya kisaikolojia tu, unaweza kuyaondoa wewe mwenyewe.
 
You get what you wish or think about! Laws of attraction respond precisely as per your thought and wish!! Muone Dr Mauki atakusaidia na pia jenga tumaini la kuishi hata km Kifo kipo,soma neno la Mungu pia kwa sana
 
Kwanza alitakiwa ajitambulishe tumwelewe vizuri ndipo tumshauri. The way ninavyoweza mshauri machinga, dereva bodaboda, Mengi, Magufuli, mkulima mdogo, afisa usalama, kibaka, padre, Mwalimu, daktari, housegirl /houseboy, mpiga debe, mama wa nyumbani, polisi, jw n.k. ni tofauti tofauti. Toa sifa zako, kama ni gaidi Sawa "ukiua kwa risasi utakufa kwa risasi ".

Hahahahah una mikwara wewe.

Nishauri basi, mimi ndo Mengi.
 
Tafutaa hudumaa safii ya maombez ukombolewe kwa Damu takatifuu ya Yesu unasumbuliwa na kufuatwa na roho ya mautii. Ikemee kwa jina la Yesu lishindwe na lisikufuatee pia jarbuu kubadil life stail yakoo na punguza kukaa pekeakoo
 
Kuna kipindi flani nilikuwa naangalia sana series ya 'THE WALKING DEAD' ile ya mazombi...basi karibu kila siku nilikuwa naota mimi ndo starling nipo pamoja na wakina Rick, Daryl, Michonne tupo tunaua mazombie..
USHAURI: Acha kupenda maadui kwenye movie unazoangalia badala yake we mpende STELING utaona UTAKUWA UNAOTA WEWE NDO UNAWAFATA WATU NA BUNDUKI BADALA YA KUFATWA WEWE.
 
Hivi ni kweli huduma hiyo ni bure kuna uncle wangu nataka nimpeleke kama ni bure naomba ufafanuzi
Mkuu nenda tu Muhimbili pale kuna kitengo cha magonjwa ya akili.
Ugonjwa huu si kichaa bali unatokana na vitu mbali mbali kwa mfano mtu kuwa na wasi wasi mwingi sana au kujihisi kama mtu anataka kukuua, hilo ni tatizo la ugonjwa wa fahamu na si kichaa moja kwa moja.

Nina ndugu aliyeugua miaka mingi sikufahamu, baada ya kupata ushauri kama huu tulimwona daktari na anendelea vizuri kabisa.
 
Back
Top Bottom