shaks001
JF-Expert Member
- Feb 6, 2014
- 1,246
- 1,070
Heshima kwenu wakuu,
Naamini JF kuna wajuzi wa mambo ambao wanaweza kusaidia kushauri na mengine mengi tu.Kwa miaka mingi sana nimekuwa nasumbuliwa na hisia mbaya kichwani mwangu ambazo kwa kweli zinanikosesha raha na amani.Nimekuwa kila nikikaa mahali nahisi kama kuna mtu anakuja na silaha(bastola),anani-shoot na kuondoka.
Hali hii huwa inanitokea hata nikiwa nyumbani peke yangu nikisikia kitu kimegonga mlango au kimedondoka basi haraka hushtuka na kuanza "kunyata"kuelekea mlio ulipotokea kwa umakini mkubwa kujiridhisha kama kuna usalama
Hali hii imenifanya nisiweze kukaa milango wazi hata mchana huwa nikiwa nyumbani najifungia milango yote.Nimevumila kwa muda mrefu lakini nimeona leo nifunguke kwa wataalamu wa mambo hapa JF nikiamini naweza kupata msaada wa mawazo,maana inawezekana ikawa najitabiria kifo changu(Japokuwa sina imani hiyo).
NB:Sina ugomvi wala uadui na mtu,na ni raia safi tu!