Nahisi kama nimefikia hatua ya Kukata Tamaa kiwango cha Mwisho. Naomba msaada wenu Ndugu zanguni

Status
Not open for further replies.
Uza gari iliyobaki fungua biashara ndogo inayoweza kukuingizia kipato kidogo na kukuweka bize utafanikiwa.trust me.

N.B usiwekeze hela yote kwenye hiyo biashara.
 
" Mimi ni member wa Jamiiforums kwa kipindi kirefu kidogo. Nimekuwa nikishirikiana na kushirikishana nanyi mambo mbalimbali ya maisha na pia ya burudani. Nimewaza kwa muda mrefu sana kabla sijaamua kuandika thread hii.

Nlikuwa nmeajiriwa na Kampuni moja ya Mambo ya IT na usafirishaji pia toka mwaka 2015. Nikifanya kazi katika nafasi mbalimbali Kama Operation Manager, Public Relation Manager na pia nikisaidiana na Managers mbalimbali katika majukumu yao niki coordinate Projects mbalimbali za Kampuni.

Mwaka 2017 Kampuni yetu ilianza kuyumba. Tuliyumba sana kutokana na mambo mbalimbali ya Soko (Wateja wetu wakubwa walikuwa ni kutoka Serikalini na Makampuni Makubwa)

Tukawa kama mtu aliyepata ulemavu wa mguu mmoja. Tulijitahidi sana kupambana na kuzoea hali hiyo ya kutumia mguu mmoja. Hali iliendelea kuwa mbaya. Bahati mbaya mpaka kufika katikati ya mwaka 2019 tukawa hatuwezi hata lipana mishahara.

Tukawa tunapeana posho na hatimaye ikafika hatua hata posho ikawa ngumu. Tuliendelea kujitahidi kupambana hadi ikafikia hatukuwa na uwezo wa kulipwa kitu kabisa. Hivyo mwaka huo kuanzia mwezi wa 9 hatukuwa tunapokea anything in terms of money.na hatimaye Kampuni ikatuomba sisi wengine tuandike barua ya ku resign au tufukuzwe kazi. Binafsi nliona hali ilivyokuwa.sababu before that pia CEO alituomba tuwe free kuacha kazi.

Mimi nlikuwa katika watu wachache ambao niliamini tungepambana tukashinda hali ile.nikaomba niendelee. Nikawa natumia pesa yangu na hatimaye akiba yangu yote kwisha. Nikauza gari moja nipate pesa ya nauli na matumizi nyumbani.

Mke wangu hakuwa kazini. Nilimpa pesa Mil 6. Akafanye biashara. Bahati mbaya sana akapoteza hizo pesa zote katka biashara akichangiwa hasa na Haya makampuni ya GNLD na Q-Net. Mtaji ukaisha.

Tukaamua tena kuuza gari nyingine ili watoto waende shule na pia tujitahidi kumalizia ujenzi. Hapo tulipokuwa tunaishi pia ilibidi tulipe kodi. Hatukukamilisha ujenzi.

Nifupishe habari. Toka mwaka jana mwezi wa 9 nmepambana sana kutafuta kazi.lakini sikufanikiwa pesa hizo nlizokuwa nazo ilibidi pia niingize kwenye matibabu kwa sababu ya ugonjwa nliokuwa nao mguu wa kulia una tatizo la maumivu makali kwenye mfupa na kushoto kiasi.

Nimehangaika sana Aga Khan, Hindu Mandal na Moi. Walinipa ushauri wa kupunguza uzito na kutotembea sana (Ugonjwa unaitwa Heel Spurs) so ikabidi pia nibakize gari moja liwe ndo la kutembelea.so nikabaki na gari dogo.

Maisha yalizidi kuwa magumu na hatimaye kodi ikawa ngumu kulipa.ikapita miezi 2 mwenye nyumba akashindwa kutuvumilia. Akaja tukatoa vitu nje. Watoto wangu wawili walikuwa wanasoma Elimu ya Msingi(mmoja hajaanza bado nina watoto watatu) wakarudishwa nyumbani.

Siku tunalazimika kutoa vitu nje it was a very humiliating day. Mimi, mke,dada wa kazi na watoto wetu watatu.Mke akaamua kuita gari lije chukua vyombo kupeleka kwao. Siwezi sahau siku hiyo.Ndo siku ya mwisho kumwona mke wangu mpaka leo hii hatujaonana tena.

Vitu vilipakiwa kwenye gari ikawa inatakiwa kulipia tsh 150,000 mke wangu akataka nitoe pesa, sikuwa nayo. Wife akapiga simu kwa mdogo wake akamtumia. They left mimi nikiwa sielewi nifanye nini.

Nlitoka na gari nikaenda park sehemu nikakaa mpaka usingizi uliponipitia nlikuja shtuka saa 2 usiku sina pa kwenda kulala.mfukoni nina tsh 7000 tu. Nlitumia 1000 kununua mihogo na 6000 nikaweka kama balance. 1000 nilienda lipia wanapolaza magari.nami nikashusha kiti nikalala kwenye gari mpaka asubuhi.

Kwa siku 3 nlikuwa nahangaika sina cha kufanya. Nilipata wazo la kuwasiliana na rafiki yangu wa shule ya msingi. Nlimweleza tatizo langu akanishauri niende kwake ana chumba cha wageni nikaishi naye.

Kiukweli kwa umri wangu wa miaka 30+ nlijisikia vibaya sana.nlienda ishi naye.sikuwa na namna.

Nashukuru kuna marafiki wachache ambao hawakunitupa ktk jambo hili hata kwa kunitia moyo na mwingine kunisaidia hata pesa ya voucher au usafiri.

Katika kipindi hiki nimepoteza sana marafiki. Wengi walikata mawasiliano kabisa.hata napopiga kuwasalimia.(si kuomba pesa) wamekuwa hawapokei simu zangu.

Nmekuwa hata natuma texts kuwasalimia na sometimes kuwaomba wanikumbuke zinapotokea nafasi za ajira. Wameacha kujibu.

Binafsi nilikuwa ni mtu ninayeshirikiana na kila mtu.sikuwahi bagua mtu au mtendea mtu ubaya. Maisha yangu sikuwahi kunywa pombe au kuvuta sigara.

Nimekuwa na majonzi hasa kutengwa na familia yangu. Mke wangu amekuwa si wa mawasiliano ya karibu nami. Ni kama amesusa. Watoto kila napoongea nao wanalia na kutaka turudi kuishi pamoja. Mmoja ameamua kabisa kutoongea nami hata napoomba kumsalimia.Hataki.

Nashindwa kwenda kwa wakwe kuisalimia familia yangu. Lakini nashindwa zaidi kwenda mikono mitupu kuonana na familia yangu. Wakwe zangu hawakuwahi nisemesha lolote hata baada ya kuona mke amerudi kwao. Nimewaelewa pia kwa hilo.

Mke wangu alifanikiwa kupata kazi sehemu. Lakini bado amekuwa akitaka nimtumie pesa za matumizi hata ndogo ndogo ambazo angeweza saidia mwenyewe.nafahamu anafanya hivi kuniumiza zaidi au kuonesha kuwa ni mwanaume irresponsible.

Naumia sababu wazazi wangu ambao nlipaswa niwe nawasaidia wao ndo wanatuma pesa kiasi wapatacho kuisaidia familia yangu. (Wao wanaishi Mwanza) Baba yangu alishastaafu.hana kazi.mama yangu pia anafanya tu ufugaji mdogo mdogo.

Naishi kwa fadhila za wadogo zangu na rafiki yangu huyu ambaye namwonea huruma pia. Nina Elimu ya Degree (naomba nisitaje ya nini/nisitoe details nyingi isipokuwa kwa mtu ambaye tutawasiliana inbox privately ikiwa atakuwa na namna ya kunisaidia)

Leo nimeandika kwa majonzi thread hii baada ya kutumiwa tsh 5000 kwenye simu na msichana ambaye alikuwa housemaid wetu akiwa huko aliko na wife. Yeye ananikumbuka.

Nmeumia kwa alichoandika (baba najua unaumia huko uliko pokea hiyo hata ya vocha mimi nakuombea ufanikiwe) nmejaribu kumrudishia hiyo pesa ametuma zaidi 7000 na kutaka nitumie.

Juzi nlipata simu kwa mtu ambaye nikiwa kazini aliwahi patwa na tatizo la kikazi alipokuwa ameenda kikazi Kampuni flani na kushawishika kuiba kitu flani. Nikiwa PR nlienda shughulikia jambo hilo.bahati mbaya ushahidi ww CCTV Camera ulimwonesha yule bwna mdogo akitenda jambo hilo. Muda huo akiwa amewekwa chini ya ulinzi na gari ya Kampuni imezuiliwa. Nlimsaidia akatolewa na siku mreport kazini zaidi ya kumwonya na kumshauri.

Alionekana kujutia kosa lake sana. Mwaka na nusu umepita juzi kanikumbuka nikiwa sina hata tsh 500. Mfukoni akanitumia tsh 30,000. Nlishamsahau.akanambia tu "Boss nimekuumbuka naomba hiyo uweke mafuta" nlimshukuru sana. Hajui kama sina kazi.

Haya mambo yananiumiza zaidi na kuona nina deni zaidi kwa familia yangu,rafiki zangu na wanaonizunguka.

Ndugu zanguni. Nipo katika msongo wa mawazo. Naona i have failed my family. I have failed my parents and relatives. Nliwaza kumeza dawa nyingi sana kukatisha maisha yangu. Mara kadhaa yananijia hayo mawazo.

Nashindwa nifanye nini. Nahangaika kuomba kazi na kutafuta kazi.tatizo langu la miguu halinipi nafasi ya kufanya kazi ambayo ntasimama sana, au ntatembea sana.

Nmetengwa nimebaki peke yangu.najiona mzigo kwa huyu rafiki yangu na familia yake.naona pia nmekuwa so humiliated.

Naombeni msaada wa kazi. Kazi katika upande wa kusimamia projects,kusimamia hata madereva pia naweza kuwa dereva wa mtu(gari ndogo) gari nayotumia haiwezekani kuwa Uber najua kuna mtu anaweza nishauri hivyo.ilikataliwa kwa namna ilivyo.

Pia nina uzoefu katika kufundisha ngazi za certificates na diploma masomo ya management, customer care, social skills,communication skills, development studies.

Ni mzuri katika kuongea na kuandika pia english and swahili ( do not consider this article it is informal)

Najua watu wengine wata kebehi,watanidharau na kunikashifu.nitayapokea yote. Kwa mtu ambaye atakuwa radhi kujadiliana nami jambo hili in person nipo radhi. Nahitaji kazi niweze saidia wengine pia. Si vyema nikaendelea pokea misaada toka kwa watu wengine. Nahitaji pia kuishi na familia yangu.

Nipo Dar Es Salaam kwa sasa naishi Bunju. Asanteni"
Mungu wangu!

Acha kwanza kushughulikia langu, mshughulikie huyu Kaka.

Hakika ukiona lako zito Kuna watu Wana mazito zaidi.

Mungu akutie nguvu, Ipo siku itabaki hadithi.

Nisisahau........Mungu ukishambariki huyu Kaka, akiweza kuhudumia wanae, nakuomba mlipe huyo mkewe sawasawa na anachostahili
 
Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi ndugu, wandugu tusimlaumu huyu ndugu yetu kwamba kwanini hakuwekeza katika biashara kipindi akiwa katika comfort zone, mapito yanatofautiana, historia zinatofautiana na jinsi ya kujifunza kitu pia huja tofauti, i’m sure baada ya hili atakuwa amejifunza na atajipanga vizuri siku akikaa sawa.

Anayeweza kumsaidia huyu ndugu tafadhali amsaidie avuke hili au hata asogee kidogo, hii ni hali mbaya sana hasa kwa mwanaume, mimi sina cha kukusaidia ndugu, zaidi sana ninakuombea.
 
Na Hili litapita

Nianze KWA kusema wewe si wa Kwanza kupitia hii Hali ,wewe si wa Kwanza kupitia kipindi kigumu
Tena wewe una nafuu kubwa Sana
Una
Gari
Una nyumba

Uza hilo gari hata KWA Bei chee ,tafuta frem weka biashara unayoiweza pesa nyingine tafuta nyumba ndogo maximum vyumba viwili tu
 
Kuna suala moja la kujifunza kwenye mkasa wa huyu bwana,jamani tusidanganyane ukipata nafasi ya kushika hela jenga hata ka nyumba ka chumba na sebule ili likitokea la kutokea uwe na sehemu iitwayo kwako.Nimeshangaa sana ndugu yangu huyu ana gari tatu ila anaishi kwenye nyumba ya kupanga HII NI AIBU KUBWA SANA!!!! Na asilimia kubwa ya vijana ndio aina ya maisha yetu TUNAPENDA TUONEKANE TUNA DRIVE MA NDINGA HUKU UMEPANGA CHUMBA NA SEBULE kibaya zaidi una familia,my friend mambo yakibadilika familia haiwezi kuishi kwenye gari NDIO MAANA MKE ALIAMUA KUKIMBIA NA FAMILIA KWA KUWA ALIONA BABA HANA SEHEMU YA KUISHI NA KWENYE NYUMBA KAFUKUZWA!!!
 
Pole sana kwa hilo. Naomba usinywe dawa ya aina yeyote au pombe kwa ajili ya kudhuru maisha yako (kujitoa uhai) kisa ugumu wa maisha. Marafiki wa kweli utawajua nyakati za shida. Marafiki wengi ni feki,maana wanakupenda pale unapokuwa una kitu mfukoni lakini jambo baya likikupata hautamwona hata mmoja wapo wanakukimbia na kukuogopa wanafikiria unapowapigia utawapiga mzinga. Pamoja na ugumu huo tuliza kichwa hangaika naamini ipo siku unaweza kuokota na kupata kitu. Ukipata tena utashangaa marafiki walewale waliokukimbia watakuja tena. Najua hayo mambo magumu unayoyapitia nami pia nilipitia na nikaona tabia za marafiki na baadhi ya ndugu jinsi wanavyofanya. Pole mkuu mimi nimeielewa hiyo hali.
 
Pole sana kaka , Mungu atasimama na wewe hakika. Niliwahi kucharara nkatengwa na Watu wangu nkapotea miaka 5 . Nkapotea kutafta nimerudi nimeokota Gold kubwa na wao wamerudi nawachora tu. Jikaze kiume, onesha uume wako yataisha na utarudi kwenye Form kama kawaida.
 
Mkuu,unamwamini Mungu...mimi nikikupa mkasa wangu,nilikuwa nafanya kazi bank hapohapo Dar,na nilikuwa naishi bunju A,hugo yako cha mtoto,nilipita miaka 7 kavu..kwenye situation hiyo ndio maana nauliza,unamwamini Mungu....
Umemuuliza swali ambalo nilitaka kumuuliza pia maana kama anamwamini Mungu aliye hai basi atamfanikisha. Naomba asome Isaya 43:1-3. Ni ujumbe mzuri sana kwako someni na uombe. Nina uhakika Mungu atakuvusha ukiwa mshindi. Hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea, kikubwa kaa magotini kwa Bwana. Mungu akufanikishe ktk jina la Yesu.
 
" Mimi ni member wa Jamiiforums kwa kipindi kirefu kidogo. Nimekuwa nikishirikiana na kushirikishana nanyi mambo mbalimbali ya maisha na pia ya burudani. Nimewaza kwa muda mrefu sana kabla sijaamua kuandika thread hii.

Nlikuwa nmeajiriwa na Kampuni moja ya Mambo ya IT na usafirishaji pia toka mwaka 2015. Nikifanya kazi katika nafasi mbalimbali Kama Operation Manager, Public Relation Manager na pia nikisaidiana na Managers mbalimbali katika majukumu yao niki coordinate Projects mbalimbali za Kampuni.

Mwaka 2017 Kampuni yetu ilianza kuyumba. Tuliyumba sana kutokana na mambo mbalimbali ya Soko (Wateja wetu wakubwa walikuwa ni kutoka Serikalini na Makampuni Makubwa)

Tukawa kama mtu aliyepata ulemavu wa mguu mmoja. Tulijitahidi sana kupambana na kuzoea hali hiyo ya kutumia mguu mmoja. Hali iliendelea kuwa mbaya. Bahati mbaya mpaka kufika katikati ya mwaka 2019 tukawa hatuwezi hata lipana mishahara.

Tukawa tunapeana posho na hatimaye ikafika hatua hata posho ikawa ngumu. Tuliendelea kujitahidi kupambana hadi ikafikia hatukuwa na uwezo wa kulipwa kitu kabisa. Hivyo mwaka huo kuanzia mwezi wa 9 hatukuwa tunapokea anything in terms of money.na hatimaye Kampuni ikatuomba sisi wengine tuandike barua ya ku resign au tufukuzwe kazi. Binafsi nliona hali ilivyokuwa.sababu before that pia CEO alituomba tuwe free kuacha kazi.

Mimi nlikuwa katika watu wachache ambao niliamini tungepambana tukashinda hali ile.nikaomba niendelee. Nikawa natumia pesa yangu na hatimaye akiba yangu yote kwisha. Nikauza gari moja nipate pesa ya nauli na matumizi nyumbani.

Mke wangu hakuwa kazini. Nilimpa pesa Mil 6. Akafanye biashara. Bahati mbaya sana akapoteza hizo pesa zote katka biashara akichangiwa hasa na Haya makampuni ya GNLD na Q-Net. Mtaji ukaisha.

Tukaamua tena kuuza gari nyingine ili watoto waende shule na pia tujitahidi kumalizia ujenzi. Hapo tulipokuwa tunaishi pia ilibidi tulipe kodi. Hatukukamilisha ujenzi.

Nifupishe habari. Toka mwaka jana mwezi wa 9 nmepambana sana kutafuta kazi.lakini sikufanikiwa pesa hizo nlizokuwa nazo ilibidi pia niingize kwenye matibabu kwa sababu ya ugonjwa nliokuwa nao mguu wa kulia una tatizo la maumivu makali kwenye mfupa na kushoto kiasi.

Nimehangaika sana Aga Khan, Hindu Mandal na Moi. Walinipa ushauri wa kupunguza uzito na kutotembea sana (Ugonjwa unaitwa Heel Spurs) so ikabidi pia nibakize gari moja liwe ndo la kutembelea.so nikabaki na gari dogo.

Maisha yalizidi kuwa magumu na hatimaye kodi ikawa ngumu kulipa.ikapita miezi 2 mwenye nyumba akashindwa kutuvumilia. Akaja tukatoa vitu nje. Watoto wangu wawili walikuwa wanasoma Elimu ya Msingi(mmoja hajaanza bado nina watoto watatu) wakarudishwa nyumbani.

Siku tunalazimika kutoa vitu nje it was a very humiliating day. Mimi, mke,dada wa kazi na watoto wetu watatu.Mke akaamua kuita gari lije chukua vyombo kupeleka kwao. Siwezi sahau siku hiyo.Ndo siku ya mwisho kumwona mke wangu mpaka leo hii hatujaonana tena.

Vitu vilipakiwa kwenye gari ikawa inatakiwa kulipia tsh 150,000 mke wangu akataka nitoe pesa, sikuwa nayo. Wife akapiga simu kwa mdogo wake akamtumia. They left mimi nikiwa sielewi nifanye nini.

Nlitoka na gari nikaenda park sehemu nikakaa mpaka usingizi uliponipitia nlikuja shtuka saa 2 usiku sina pa kwenda kulala.mfukoni nina tsh 7000 tu. Nlitumia 1000 kununua mihogo na 6000 nikaweka kama balance. 1000 nilienda lipia wanapolaza magari.nami nikashusha kiti nikalala kwenye gari mpaka asubuhi.

Kwa siku 3 nlikuwa nahangaika sina cha kufanya. Nilipata wazo la kuwasiliana na rafiki yangu wa shule ya msingi. Nlimweleza tatizo langu akanishauri niende kwake ana chumba cha wageni nikaishi naye.

Kiukweli kwa umri wangu wa miaka 30+ nlijisikia vibaya sana.nlienda ishi naye.sikuwa na namna.

Nashukuru kuna marafiki wachache ambao hawakunitupa ktk jambo hili hata kwa kunitia moyo na mwingine kunisaidia hata pesa ya voucher au usafiri.

Katika kipindi hiki nimepoteza sana marafiki. Wengi walikata mawasiliano kabisa.hata napopiga kuwasalimia.(si kuomba pesa) wamekuwa hawapokei simu zangu.

Nmekuwa hata natuma texts kuwasalimia na sometimes kuwaomba wanikumbuke zinapotokea nafasi za ajira. Wameacha kujibu.

Binafsi nilikuwa ni mtu ninayeshirikiana na kila mtu.sikuwahi bagua mtu au mtendea mtu ubaya. Maisha yangu sikuwahi kunywa pombe au kuvuta sigara.

Nimekuwa na majonzi hasa kutengwa na familia yangu. Mke wangu amekuwa si wa mawasiliano ya karibu nami. Ni kama amesusa. Watoto kila napoongea nao wanalia na kutaka turudi kuishi pamoja. Mmoja ameamua kabisa kutoongea nami hata napoomba kumsalimia.Hataki.

Nashindwa kwenda kwa wakwe kuisalimia familia yangu. Lakini nashindwa zaidi kwenda mikono mitupu kuonana na familia yangu. Wakwe zangu hawakuwahi nisemesha lolote hata baada ya kuona mke amerudi kwao. Nimewaelewa pia kwa hilo.

Mke wangu alifanikiwa kupata kazi sehemu. Lakini bado amekuwa akitaka nimtumie pesa za matumizi hata ndogo ndogo ambazo angeweza saidia mwenyewe.nafahamu anafanya hivi kuniumiza zaidi au kuonesha kuwa ni mwanaume irresponsible.

Naumia sababu wazazi wangu ambao nlipaswa niwe nawasaidia wao ndo wanatuma pesa kiasi wapatacho kuisaidia familia yangu. (Wao wanaishi Mwanza) Baba yangu alishastaafu.hana kazi.mama yangu pia anafanya tu ufugaji mdogo mdogo.

Naishi kwa fadhila za wadogo zangu na rafiki yangu huyu ambaye namwonea huruma pia. Nina Elimu ya Degree (naomba nisitaje ya nini/nisitoe details nyingi isipokuwa kwa mtu ambaye tutawasiliana inbox privately ikiwa atakuwa na namna ya kunisaidia)

Leo nimeandika kwa majonzi thread hii baada ya kutumiwa tsh 5000 kwenye simu na msichana ambaye alikuwa housemaid wetu akiwa huko aliko na wife. Yeye ananikumbuka.

Nmeumia kwa alichoandika (baba najua unaumia huko uliko pokea hiyo hata ya vocha mimi nakuombea ufanikiwe) nmejaribu kumrudishia hiyo pesa ametuma zaidi 7000 na kutaka nitumie.

Juzi nlipata simu kwa mtu ambaye nikiwa kazini aliwahi patwa na tatizo la kikazi alipokuwa ameenda kikazi Kampuni flani na kushawishika kuiba kitu flani. Nikiwa PR nlienda shughulikia jambo hilo.bahati mbaya ushahidi ww CCTV Camera ulimwonesha yule bwna mdogo akitenda jambo hilo. Muda huo akiwa amewekwa chini ya ulinzi na gari ya Kampuni imezuiliwa. Nlimsaidia akatolewa na siku mreport kazini zaidi ya kumwonya na kumshauri.

Alionekana kujutia kosa lake sana. Mwaka na nusu umepita juzi kanikumbuka nikiwa sina hata tsh 500. Mfukoni akanitumia tsh 30,000. Nlishamsahau.akanambia tu "Boss nimekuumbuka naomba hiyo uweke mafuta" nlimshukuru sana. Hajui kama sina kazi.

Haya mambo yananiumiza zaidi na kuona nina deni zaidi kwa familia yangu,rafiki zangu na wanaonizunguka.

Ndugu zanguni. Nipo katika msongo wa mawazo. Naona i have failed my family. I have failed my parents and relatives. Nliwaza kumeza dawa nyingi sana kukatisha maisha yangu. Mara kadhaa yananijia hayo mawazo.

Nashindwa nifanye nini. Nahangaika kuomba kazi na kutafuta kazi.tatizo langu la miguu halinipi nafasi ya kufanya kazi ambayo ntasimama sana, au ntatembea sana.

Nmetengwa nimebaki peke yangu.najiona mzigo kwa huyu rafiki yangu na familia yake.naona pia nmekuwa so humiliated.

Naombeni msaada wa kazi. Kazi katika upande wa kusimamia projects,kusimamia hata madereva pia naweza kuwa dereva wa mtu(gari ndogo) gari nayotumia haiwezekani kuwa Uber najua kuna mtu anaweza nishauri hivyo.ilikataliwa kwa namna ilivyo.

Pia nina uzoefu katika kufundisha ngazi za certificates na diploma masomo ya management, customer care, social skills,communication skills, development studies.

Ni mzuri katika kuongea na kuandika pia english and swahili ( do not consider this article it is informal)

Najua watu wengine wata kebehi,watanidharau na kunikashifu.nitayapokea yote. Kwa mtu ambaye atakuwa radhi kujadiliana nami jambo hili in person nipo radhi. Nahitaji kazi niweze saidia wengine pia. Si vyema nikaendelea pokea misaada toka kwa watu wengine. Nahitaji pia kuishi na familia yangu.

Nipo Dar Es Salaam kwa sasa naishi Bunju. Asanteni"
Pole ndugu yangu,naamini utapata msaada
 
Huu utawala wa awamu ya tano umesababisha kilio na maumivu mengi sana kwa watu walio wengi sana Kama si moja kwa moja Basi Ni kwa namna nyingine.

Maisha magumu hayajawahi kutokuwepo awali,au kuanguka na kuinuka sio kwamba hakujawahi kuwepo laa! Bali kipindi hiki kilio kimekua nikikubwa mno!

Lakini yote ya yote Mungu anajua mengi kuliko mwanadam yoyote.
Leo yetu,kesho yetu ipo juu ya uweza wake.

Hivyo ndugu mleta mada usivunjike moyo sana, Mungu yule alie idhinisha kuwepo kwako hapa duniani hatakuacha moja kwa moja.

Kwa umakini mkubwa niweza kusoma kisa chako hakika ni vigumu kustahimili,lakini kwa jana ilipita na ikafika leo na bado na uzima Basi hata kesho itafika haliyakua upo na uzima na furaha na Tumaini.

Kwenye kisa hiki siwezi kushangaa ya huyo mke wako kwa sababu Ni Mara chache sana mwanamke kufanya kinyume Cha huyo wako, wengi wa wanawake kwa kweli hufanya hivi.

Lakini huyo binti ndie alie nistaajabisha na kunipa Tumaini la kukuambia pale usipotegemea ndipo palipo na kuinuka kwako.

Kuna mfano katika kitabu chetu Cha dini, Biblia. Mtu mmoja alikua ni mkuu wa jeshi, zamani hizo kulikua na magonjwa makubwa na moja wapo Ni ukoma, huyu jamaa alitafuta tiba nyingi akakosa. Baadae binti yake wakazi akamwambia kwenye nchi yetu Kuna nabii wa Mungu anaweza kukusaidia.
Yule bwana hakudharua ushauri was binti wake wa kazi, alifunga safari akaenda kwa huyo nabii.
Lakini hakuonana nae bali wasaidizi wa huyo nabii na alipewa ujumbe kwamba ili apone akanawe mara sana katika mferi fulani.
Yule mkuu wa jeshi aliekua mgonjwa akadharau ujumbe huo akisema Kama kunawa nimenawa kwenye mji wetu Tena na maji masafi sijapona ndio nije niponee kwenye maji haya machafu ya mfereji?

Akaondoka kurudi kwao, alipokua njiani akashauriwa heri angetekeleza ujumbembe ule hata Kama asingepona si Neno!
Akakatashauri na akarejea kwenye ule mfereji na akanawa na akapona!

Nimetolea mfano huo japo sio kwa usahihi sana, lakini nataka kuegemea kwenye angle ya kwamba sehumu ulizo ziainisha kwenye kisa chako ukitazamia Kama ungepata kimojawapo kinge kuinua!
Mimi nadhani unaweza ukainuka hata kwa kidogo tuu, kwa mfano 30000 hio aliokutumia yule ndugu ulie msilaidia ingeweza kua mtaji wa kukuinua kiasi ambacho usingedhania.

Pia unaweza ukasaidiwa kuinuka, au Mungu anaweza kumtuma mtu akawa sababu ya wewe kuinuka Tena ila huyo mtu akawa Ni wa thamani ndogo sana lakini wewe usidhanie ya kua huyo ndie sababu ya kuinuka kwako , rejea huyo binti aliekutumia 5000 na Neno alilokupa. Kisha umrejelee yule binti wa mfano kwenye Biblia aliemshauri boss wake na kwa ushauri huo alulipouzingatia alipona.

Hii mada inaweza kua ndio mwanzo was kuinuka kwako.
Naomba uombe kwa Mungu msamaha,nawe ujisamehe, nawe usamehe. Ujivike nguvu, usijihesabie kwamba unaumwa, fanya chochote, usione aibu, kila safari ilinza na hatua moja. Na kuanguka sio ishu Bali kukaa pale pale ulipoangukia ndi ishu.

Mimi nakuombe Mungu ni mweme tena Ni mwema mno, tena hata kuacha total.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesema tangu ufukuzwe kwenye nyumba ya kupanga Wakwe zako hawajakupigia simu yoyote na ww uko kimya wala hujawahi fika..Unafikiri uko sahihi kufanya hivyo??unafikiri kwann wameamua kukaa kimya??una mshutumu mkeo kwa kukusaliti kwenye matatizo,ila ww kuwadharau wazazi wake ni sawa tu?kumbuka hao wazazi wake ndio wanaomsaidia sasa kulea watoto wako baada ya ww kushindwa kufanya hivyo..so kitendo cha kutokwenda kuonana nao na kuzungumza nao kuhusu situation unayopitia sasa ni dharau na ndio mana na wao wakaamua kukaa kimya ili waone mwisho wako..inaonekana ni MTU unaependa kuonekana wa hadhi ya juu tu so kitendo cha uchumi kuyumba kidogo unaona aibu kujitokeza kwa wakwe zako ndio maana umeweza kumiliki gari tatu za kutembelea ilihali uko ktk nyumba ya kupanga..na hata mwenye nyumba nadhani ameona unamletea dharau za kutomlipa kodi yake ilihali unarudi nyumbani na gari pengine anategemea hiyo kodi ikidhi basic needs zake..yaan kukosa kazi tu kunakufanya usiwe na uchungu hata wa kuwatembelea watoto wako ukweni kisa kipato kimeshuka??wewe ni baba wa aina gani,ndio mana huyo mtoto mwingine hataki kuongea na ww kwenye simu amehisi huna mapenzi nae..umeona ukaishi kwa rafiki ni bora kuliko kupata ushauri wowote kwa wakwe zako??come on buddy..Jaribu kujishusha haya maisha hayana mwamba ndio mana yakaitwa ni safari kuna kupanda na kushuka so usione soo... Am sorry brother sikua na nia ya kukukejeli kukudhihaki or sina maana sijaguswa na madhila yanayokusibu Ila nimejarbu kufikri kwa namna nyingine kwa lengo LA kujenga ni hayo tu unaweza fanyia kazi ukiona inafaa pole sana mkuu...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom