Simbamteme
JF-Expert Member
- Sep 10, 2011
- 808
- 2,169
Miaka hiyo muigizaji Sylvester stallon "RAMBO" alipitia msoto wa kufa mtu katika maisha yake,alifulia vibaya mno hadi kufikia hatua ya kuiba mkufu wa mke wake na kwenda kuuza..kama hiyo haitoshi ilifikia hatua alishindwa kumlisha mbwa wake aliyekuwa anampenda sana na kuamua kwenda kumuuza kwa dola 25 tu na kwa maelezo yake baada ya kumuuza aliondoka huku analia..mambo yaliendelea kuwa magumu,alishindwa kulipa kodi ya pango hivyo ikamlazimu alale siku 3 kweye kituo cha mabasi cha New York
FAST FORWARD, wiki mbili baadaye aliona mechi ya BOXING kati ya Muhamed Ally na Chuck Wepner..Mechi hiyo ilimpa hamasa ya kuandika Script ya movie ambayo ilikuja kuwa 'Famous' sana ya 'ROCKY'
Unaambiwa aliiandika script ya movies hiyo kwa masaa 20..alijaribu kwenda kwenye makampuni ya kutengeneza filamu kwa ajili ya kuiuza na akabahatika kupata ofa ya dola 125000 ..lakini yeye alikuwa na OMBI moja tu..awe STERLING kwenye movie hiyo,bahati mbaya kampuni ikamkatalia,kampuni ilitaka "The real star",kumbuka kipindi hicho rambo alikuwa ni underground tu..je,ingekuwa wewe ungeiachia hela iende hivihivi wakati shida zimekuzidi?
Rambo aliwakatalia na kusepa na Script yake,wiki chache mbele studio ile ile ikampigia simu na kumpa ofa ya dola 250000 kwa script lakini akakataa,msimamo wake ulikuwa uleule,yeye awe STERLING..wakamuongezea ofa ya dola 350000 lakini jamaa bado akashikilia msimamo wake
Baada ya muda kidogo kupita studio ikakubali ombi lake na kumpa ofa ya dola 35000 tu..embu fikiria kutoka dola 350000 mpaka dola 35000,ungekuwa wewe ungeweza?
Kilichofata ni historia..filamu ya "ROCKY" ilishinda tuzo kibao ikiwemo "best picture" "best directing" na "best film editing" na pia RAMBO alichaguliwa kugombea for BEST ACTOR..pia filamu hiyo iliingizwa kwenye "American National Film Registry" kama moja ya filamu bora sana kuwahi kutokea.
Jamaa baada ya kupewa ile dola 35000 alienda kumnunua mbwa wake aliyemuuza kwa dola 25..mbwa huyo yupo nae kwenye filamu hiyo!
Moral of the story: Hakuna mtu anayeweza kuamini uwezo wako zaidi ya wewe mwenyewe