Nahisi kama nimefikia hatua ya Kukata Tamaa kiwango cha Mwisho. Naomba msaada wenu Ndugu zanguni

Status
Not open for further replies.
Pole sana mkuu, madam bado una uhai mshukuru Mungu. Keep the faith . Don't say never until it is all over. Kwa sasa hivi Pambana uendelee kuishi.
 
HATA WANAOKUPA POLE WANAKUPUMBAZA UNAJIONA UNA TATIZO KUBWA SANA KULIKO UWEZO WAKO MPAKA UNALIALIA ILA UKWELI HUNA TATIZO KUBWA KAMA UNAVYOLINADI BALI UFAHAMU WAKO NA AKILI YAKO INAKUAMINISHA HIVYO, NAOMBA NENDA MUHIMBILI HOSPITAL UKITOKA HAPO NENDA MAHAKAMANI UKITOKA HAPO NENDA KUTEMBELEA WAFUNGWA GEREZA LOLOTE KISHA RUDI KAAA KWA HUYO RAFIKI YAKO UJIULIZE WEWE NA WALE ULIOKWENDA KUWAONA KWENYE MAJENGO YA SERIKALI NANI ANA MATATIZO KISHA UJE ULETE HAKO KAHADITHI KAKO HAPA JF. TENA MARA MIA USINGESEMA UNA ELIMU KIWANGO CHA DEGREE NINGEKUELEWA LAKINI KAMA WASOMI NDIYO MNAKUWA WAJINGA KIASI HIKI HAKUNA SABABU YA KUSOMESHA WATOTO BORA WACHUNGE MBUZI NA KONDOO WATAKUWA BRIGHT KULIKO KUWA NANGA KAMA WEWE NATUMIA LUGHA KALI ILI NIKU PROVOKE UCHUKIE UTOKE KWA RAFIKI YAKO UNAMTILIA KIWINGU NAYE KWA UJINGA ANAFIKIRI ANAKUSAIDIA KUMBE ANAAKUPUMBAZA. WASOMI WA LEO SIYO CREATIVE MMEKAA NA KUAAMINI KAZI ZA KITUMWA KUJIAJIRI HAMUWEZI ETI MAPA UNAFIKIRIA KUJIUA HAPO NDIYO UMETHIBITISHA KUWA ELIMU ULIYO NAYO HAINA MANUFAA KWA JAMII WALA KWAKO NA FAMILIA YAKO MAANA YA ELIMU NI KUPAMBANUA MAMBO MAGUMU YOTE NA KUYAPATIA MAJIBU NA SIYO KULIALIA MKE ANAPOTEZA FEDHA WEWE UNAKENUA SASA KWA TAARIFA YAKO HUKO ALIKO ANA BWANA MWINGINE NA HANA MUDA NA WEWE NA WAKWEZO WAKO UPANDE WA YULE BWANA HASA MAMA MKWE WAKO. KAA UKILIALIA UTASHANGAA ANA MIMBA IT IS MATTER OF TIME NDIYO UTAJITUNDIKA NA MCHEZO UISHE. MIMI DARASA LA SABA POKEA USHAURI WANGU UZA KIGARI CHAKO NUNUA PIKIPIKI KAMA NI LAZIMA UWE NA USAFIRI KWA SABABU YA MGUU CHENJI IKIBAKI PAUA CHUMBA KIMOJA WEKA GENGE LA NYANYA NA MIHOGO YA KUKAANGA UTOKE KWA RAFIKIO TOFAUTI NA HIVYO UNATAKA KUGOMBANA NA RAFIKI YAKO. NDHANI UTAKUWA UMESOMA ENGLISH MIDIUM WEWE PRODUCT AMBAYO HATA MENDEA AKIINGIA NDANI UNAMUITA JIRANI AJE KUMTOA "TPX JIHADHALI'' "TPX NAFUTIKA'' BADO MMOJA
Aiseee umemkamia kweli kweli. Lakini umempa.ushauri mzuri akae kwake apunguze makali atafute pesa ya kula.
 
" Mimi ni member wa Jamiiforums kwa kipindi kirefu kidogo. Nimekuwa nikishirikiana na kushirikishana nanyi mambo mbalimbali ya maisha na pia ya burudani. Nimewaza kwa muda mrefu sana kabla sijaamua kuandika thread hii.

Nlikuwa nmeajiriwa na Kampuni moja ya Mambo ya IT na usafirishaji pia toka mwaka 2015. Nikifanya kazi katika nafasi mbalimbali Kama Operation Manager, Public Relation Manager na pia nikisaidiana na Managers mbalimbali katika majukumu yao niki coordinate Projects mbalimbali za Kampuni.

Mwaka 2017 Kampuni yetu ilianza kuyumba. Tuliyumba sana kutokana na mambo mbalimbali ya Soko (Wateja wetu wakubwa walikuwa ni kutoka Serikalini na Makampuni Makubwa)

Tukawa kama mtu aliyepata ulemavu wa mguu mmoja. Tulijitahidi sana kupambana na kuzoea hali hiyo ya kutumia mguu mmoja. Hali iliendelea kuwa mbaya. Bahati mbaya mpaka kufika katikati ya mwaka 2019 tukawa hatuwezi hata lipana mishahara.

Tukawa tunapeana posho na hatimaye ikafika hatua hata posho ikawa ngumu. Tuliendelea kujitahidi kupambana hadi ikafikia hatukuwa na uwezo wa kulipwa kitu kabisa. Hivyo mwaka huo kuanzia mwezi wa 9 hatukuwa tunapokea anything in terms of money.na hatimaye Kampuni ikatuomba sisi wengine tuandike barua ya ku resign au tufukuzwe kazi. Binafsi nliona hali ilivyokuwa.sababu before that pia CEO alituomba tuwe free kuacha kazi.

Mimi nlikuwa katika watu wachache ambao niliamini tungepambana tukashinda hali ile.nikaomba niendelee. Nikawa natumia pesa yangu na hatimaye akiba yangu yote kwisha. Nikauza gari moja nipate pesa ya nauli na matumizi nyumbani.

Mke wangu hakuwa kazini. Nilimpa pesa Mil 6. Akafanye biashara. Bahati mbaya sana akapoteza hizo pesa zote katka biashara akichangiwa hasa na Haya makampuni ya GNLD na Q-Net. Mtaji ukaisha.

Tukaamua tena kuuza gari nyingine ili watoto waende shule na pia tujitahidi kumalizia ujenzi. Hapo tulipokuwa tunaishi pia ilibidi tulipe kodi. Hatukukamilisha ujenzi.

Nifupishe habari. Toka mwaka jana mwezi wa 9 nmepambana sana kutafuta kazi.lakini sikufanikiwa pesa hizo nlizokuwa nazo ilibidi pia niingize kwenye matibabu kwa sababu ya ugonjwa nliokuwa nao mguu wa kulia una tatizo la maumivu makali kwenye mfupa na kushoto kiasi.

Nimehangaika sana Aga Khan, Hindu Mandal na Moi. Walinipa ushauri wa kupunguza uzito na kutotembea sana (Ugonjwa unaitwa Heel Spurs) so ikabidi pia nibakize gari moja liwe ndo la kutembelea.so nikabaki na gari dogo.

Maisha yalizidi kuwa magumu na hatimaye kodi ikawa ngumu kulipa.ikapita miezi 2 mwenye nyumba akashindwa kutuvumilia. Akaja tukatoa vitu nje. Watoto wangu wawili walikuwa wanasoma Elimu ya Msingi(mmoja hajaanza bado nina watoto watatu) wakarudishwa nyumbani.

Siku tunalazimika kutoa vitu nje it was a very humiliating day. Mimi, mke,dada wa kazi na watoto wetu watatu.Mke akaamua kuita gari lije chukua vyombo kupeleka kwao. Siwezi sahau siku hiyo.Ndo siku ya mwisho kumwona mke wangu mpaka leo hii hatujaonana tena.

Vitu vilipakiwa kwenye gari ikawa inatakiwa kulipia tsh 150,000 mke wangu akataka nitoe pesa, sikuwa nayo. Wife akapiga simu kwa mdogo wake akamtumia. They left mimi nikiwa sielewi nifanye nini.

Nlitoka na gari nikaenda park sehemu nikakaa mpaka usingizi uliponipitia nlikuja shtuka saa 2 usiku sina pa kwenda kulala.mfukoni nina tsh 7000 tu. Nlitumia 1000 kununua mihogo na 6000 nikaweka kama balance. 1000 nilienda lipia wanapolaza magari.nami nikashusha kiti nikalala kwenye gari mpaka asubuhi.

Kwa siku 3 nlikuwa nahangaika sina cha kufanya. Nilipata wazo la kuwasiliana na rafiki yangu wa shule ya msingi. Nlimweleza tatizo langu akanishauri niende kwake ana chumba cha wageni nikaishi naye.

Kiukweli kwa umri wangu wa miaka 30+ nlijisikia vibaya sana.nlienda ishi naye.sikuwa na namna.

Nashukuru kuna marafiki wachache ambao hawakunitupa ktk jambo hili hata kwa kunitia moyo na mwingine kunisaidia hata pesa ya voucher au usafiri.

Katika kipindi hiki nimepoteza sana marafiki. Wengi walikata mawasiliano kabisa.hata napopiga kuwasalimia.(si kuomba pesa) wamekuwa hawapokei simu zangu.

Nmekuwa hata natuma texts kuwasalimia na sometimes kuwaomba wanikumbuke zinapotokea nafasi za ajira. Wameacha kujibu.

Binafsi nilikuwa ni mtu ninayeshirikiana na kila mtu.sikuwahi bagua mtu au mtendea mtu ubaya. Maisha yangu sikuwahi kunywa pombe au kuvuta sigara.

Nimekuwa na majonzi hasa kutengwa na familia yangu. Mke wangu amekuwa si wa mawasiliano ya karibu nami. Ni kama amesusa. Watoto kila napoongea nao wanalia na kutaka turudi kuishi pamoja. Mmoja ameamua kabisa kutoongea nami hata napoomba kumsalimia.Hataki.

Nashindwa kwenda kwa wakwe kuisalimia familia yangu. Lakini nashindwa zaidi kwenda mikono mitupu kuonana na familia yangu. Wakwe zangu hawakuwahi nisemesha lolote hata baada ya kuona mke amerudi kwao. Nimewaelewa pia kwa hilo.

Mke wangu alifanikiwa kupata kazi sehemu. Lakini bado amekuwa akitaka nimtumie pesa za matumizi hata ndogo ndogo ambazo angeweza saidia mwenyewe.nafahamu anafanya hivi kuniumiza zaidi au kuonesha kuwa ni mwanaume irresponsible.

Naumia sababu wazazi wangu ambao nlipaswa niwe nawasaidia wao ndo wanatuma pesa kiasi wapatacho kuisaidia familia yangu. (Wao wanaishi Mwanza) Baba yangu alishastaafu.hana kazi.mama yangu pia anafanya tu ufugaji mdogo mdogo.

Naishi kwa fadhila za wadogo zangu na rafiki yangu huyu ambaye namwonea huruma pia. Nina Elimu ya Degree (naomba nisitaje ya nini/nisitoe details nyingi isipokuwa kwa mtu ambaye tutawasiliana inbox privately ikiwa atakuwa na namna ya kunisaidia)

Leo nimeandika kwa majonzi thread hii baada ya kutumiwa tsh 5000 kwenye simu na msichana ambaye alikuwa housemaid wetu akiwa huko aliko na wife. Yeye ananikumbuka.

Nmeumia kwa alichoandika (baba najua unaumia huko uliko pokea hiyo hata ya vocha mimi nakuombea ufanikiwe) nmejaribu kumrudishia hiyo pesa ametuma zaidi 7000 na kutaka nitumie.

Juzi nlipata simu kwa mtu ambaye nikiwa kazini aliwahi patwa na tatizo la kikazi alipokuwa ameenda kikazi Kampuni flani na kushawishika kuiba kitu flani. Nikiwa PR nlienda shughulikia jambo hilo.bahati mbaya ushahidi ww CCTV Camera ulimwonesha yule bwna mdogo akitenda jambo hilo. Muda huo akiwa amewekwa chini ya ulinzi na gari ya Kampuni imezuiliwa. Nlimsaidia akatolewa na siku mreport kazini zaidi ya kumwonya na kumshauri.

Alionekana kujutia kosa lake sana. Mwaka na nusu umepita juzi kanikumbuka nikiwa sina hata tsh 500. Mfukoni akanitumia tsh 30,000. Nlishamsahau.akanambia tu "Boss nimekuumbuka naomba hiyo uweke mafuta" nlimshukuru sana. Hajui kama sina kazi.

Haya mambo yananiumiza zaidi na kuona nina deni zaidi kwa familia yangu,rafiki zangu na wanaonizunguka.

Ndugu zanguni. Nipo katika msongo wa mawazo. Naona i have failed my family. I have failed my parents and relatives. Nliwaza kumeza dawa nyingi sana kukatisha maisha yangu. Mara kadhaa yananijia hayo mawazo.

Nashindwa nifanye nini. Nahangaika kuomba kazi na kutafuta kazi.tatizo langu la miguu halinipi nafasi ya kufanya kazi ambayo ntasimama sana, au ntatembea sana.

Nmetengwa nimebaki peke yangu.najiona mzigo kwa huyu rafiki yangu na familia yake.naona pia nmekuwa so humiliated.

Naombeni msaada wa kazi. Kazi katika upande wa kusimamia projects,kusimamia hata madereva pia naweza kuwa dereva wa mtu(gari ndogo) gari nayotumia haiwezekani kuwa Uber najua kuna mtu anaweza nishauri hivyo.ilikataliwa kwa namna ilivyo.

Pia nina uzoefu katika kufundisha ngazi za certificates na diploma masomo ya management, customer care, social skills,communication skills, development studies.

Ni mzuri katika kuongea na kuandika pia english and swahili ( do not consider this article it is informal)

Najua watu wengine wata kebehi,watanidharau na kunikashifu.nitayapokea yote. Kwa mtu ambaye atakuwa radhi kujadiliana nami jambo hili in person nipo radhi. Nahitaji kazi niweze saidia wengine pia. Si vyema nikaendelea pokea misaada toka kwa watu wengine. Nahitaji pia kuishi na familia yangu.

Nipo Dar Es Salaam kwa sasa naishi Bunju. Asanteni"
Uza hiyo nyumba tufungue mgahawa ili tupate kazi
 
Una gari, una nyumba haijakamilika una degree bado unafikiria kujiua kweli wasomi waleo ni afadhali ya darasa la saba hivi huyu mlemavu hana nyumba hana gari wala elimu kama yako bado anaishi wewe una raslimali zote hizo eti unafikiria kujiua kweli akili yako ni ndogo tofauti na elimu uliyonayo. Msomi mwenye kiwango cha degree hawezi babaika kama unavyohaha wewe wewe. Uza hicho kigari chako nunua pikipiki uingie uba uishi chenji malizia chumba kimoja hilo pagale lako hamia toka kwa rafiki yako unakuwa mzigo. Changamoto kidogo unababaika kama hukusoma na ukizubaa kweli kwa ujinga wako utajiua na mimi nasema kufa tu na ujinga wako elimu uliyo nayo haijakusaidia wewe wala familia yako unatesa watu bure NASEMA TENA SIUNGI MKONO HOJA YA WEWE KUJIUA ILA KAMA UTATHIBITISHA KUWA WEWE NI FALA HAPO JIUE LAKINI KAMA UNA AKILI TIMAMU HAYO MAWAZO TUPA CHOONI SONGAMBELE TPX JIHADHALI TPX NAFUTIKA BADO MMOJA
Kiwango cha elimu na hali halisi ya maisha ni vitu viwili tofauti! Alichokisimulia kama ni kweli basi ni jambo linaloweza kumtokea mtu yeyote bila kujali kiwango chake cha elimu!
 
Mke wangu alinisumbua sana kwa hali kama hiyo, wanawake ni wachache duniani. Muamin Mungu ipo siku utasimama tena. Usiiwaze sana familia, kama wanakula wanalala we pambana taratibu mtangulize Mungu tu.
 
Yaliyokutokea yanatokana na aidha mambo makuu mawili, kwanza ni issue ya utawala wa awamu ya tano, hii nasema iwapo kampuni uliyokuwa unafanya kazi mlikuwa mnanufaika kiujanja ujanja, baada kuthibitia vilivyo njia za ujanja ujanja, basi hakuna namna, hayo ndo matokeo yake!
Pili, huenda ukawa na tatizo la kiroho! Hapa elimu kidogo inahitakijka! Kwa kifupi ni kuwa, ktk maisha ya kiroho, kuna roho kadhaa nyingi hulandalanda kutafuta hifadhi ktk viumbe vyenye mwili na nyama, binadamu ni sehemu ya viumbe hao! Roho hawa wakikuingia, huuendesha mwili kwa matamanio yao! Wapo roho wa umasikini na utajiri, umoja wengine wa mafarakano, roho wa mauti, roho wa zinaa, roho wa ufukara, roho wa kila aina wapo na tunaishi nao! Huenda sasa umeingiwa na roho ya ufukara, roho ya kukataliwa, roho ya mafarakano, na nyinginezo kadri ya uyapitiayo!
Kama ndivyo, nakushauri kwa imani yako anza kuondoa roho hizo na kila kitu kutakaa sawa! Achana na dhihaka za watu, wengine bado wanakushauri ili iwe fursa kwa roho wabaya kuendelea kukudhoofisha!
Ahsante na nikutakie kila LA kheri!
 
Kuna wakati unaweza ukamlilia Mungu sababu ya shida zako ila ukisikia ya wengine utajiona unakufuru
Pole sana mkuu, Mungu akupitishe katika hilo.

Jamani muwe wema na muwatende mema wake zenu mnapokuwa katika nyakati nzuri ili wasiwatenge katika nyakati mbaya pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu uwe unasoma uzi wote..wapi aliposema amemtendea ubaya mke wake?amempa mtaji mil 6 amezitapanya zote na ukute hata alihonga kwa Serengeti boy au alizificha na ndio hizo anaendeshea maisha baada ya kumkimbia mumewe.
INAUMA.
 
Kaka uza gari , chukua boda yako faster anza kupiga mishe. Pia paua chumba kimoja then hamia kwako. Pole sana brother
 
Kweli Kabisa, hata mimi hapo kanishangaza sana, magari yote hayo kwenye nyumba ya kupanga ya nini?
Hisia zangu zinaniambia chanzo ni huyo mwanamke..kuna wanaume tunapenda vibaya na kuendeshwa na kushikiwa akili na Hawa viumbe..Ila mimi simo kwenye hilo kundi.
 
" Mimi ni member wa Jamiiforums kwa kipindi kirefu kidogo. Nimekuwa nikishirikiana na kushirikishana nanyi mambo mbalimbali ya maisha na pia ya burudani. Nimewaza kwa muda mrefu sana kabla sijaamua kuandika thread hii.

Nlikuwa nmeajiriwa na Kampuni moja ya Mambo ya IT na usafirishaji pia toka mwaka 2015. Nikifanya kazi katika nafasi mbalimbali Kama Operation Manager, Public Relation Manager na pia nikisaidiana na Managers mbalimbali katika majukumu yao niki coordinate Projects mbalimbali za Kampuni.

Mwaka 2017 Kampuni yetu ilianza kuyumba. Tuliyumba sana kutokana na mambo mbalimbali ya Soko (Wateja wetu wakubwa walikuwa ni kutoka Serikalini na Makampuni Makubwa)

Tukawa kama mtu aliyepata ulemavu wa mguu mmoja. Tulijitahidi sana kupambana na kuzoea hali hiyo ya kutumia mguu mmoja. Hali iliendelea kuwa mbaya. Bahati mbaya mpaka kufika katikati ya mwaka 2019 tukawa hatuwezi hata lipana mishahara.

Tukawa tunapeana posho na hatimaye ikafika hatua hata posho ikawa ngumu. Tuliendelea kujitahidi kupambana hadi ikafikia hatukuwa na uwezo wa kulipwa kitu kabisa. Hivyo mwaka huo kuanzia mwezi wa 9 hatukuwa tunapokea anything in terms of money.na hatimaye Kampuni ikatuomba sisi wengine tuandike barua ya ku resign au tufukuzwe kazi. Binafsi nliona hali ilivyokuwa.sababu before that pia CEO alituomba tuwe free kuacha kazi.

Mimi nlikuwa katika watu wachache ambao niliamini tungepambana tukashinda hali ile.nikaomba niendelee. Nikawa natumia pesa yangu na hatimaye akiba yangu yote kwisha. Nikauza gari moja nipate pesa ya nauli na matumizi nyumbani.

Mke wangu hakuwa kazini. Nilimpa pesa Mil 6. Akafanye biashara. Bahati mbaya sana akapoteza hizo pesa zote katka biashara akichangiwa hasa na Haya makampuni ya GNLD na Q-Net. Mtaji ukaisha.

Tukaamua tena kuuza gari nyingine ili watoto waende shule na pia tujitahidi kumalizia ujenzi. Hapo tulipokuwa tunaishi pia ilibidi tulipe kodi. Hatukukamilisha ujenzi.

Nifupishe habari. Toka mwaka jana mwezi wa 9 nmepambana sana kutafuta kazi.lakini sikufanikiwa pesa hizo nlizokuwa nazo ilibidi pia niingize kwenye matibabu kwa sababu ya ugonjwa nliokuwa nao mguu wa kulia una tatizo la maumivu makali kwenye mfupa na kushoto kiasi.

Nimehangaika sana Aga Khan, Hindu Mandal na Moi. Walinipa ushauri wa kupunguza uzito na kutotembea sana (Ugonjwa unaitwa Heel Spurs) so ikabidi pia nibakize gari moja liwe ndo la kutembelea.so nikabaki na gari dogo.

Maisha yalizidi kuwa magumu na hatimaye kodi ikawa ngumu kulipa.ikapita miezi 2 mwenye nyumba akashindwa kutuvumilia. Akaja tukatoa vitu nje. Watoto wangu wawili walikuwa wanasoma Elimu ya Msingi(mmoja hajaanza bado nina watoto watatu) wakarudishwa nyumbani.

Siku tunalazimika kutoa vitu nje it was a very humiliating day. Mimi, mke,dada wa kazi na watoto wetu watatu.Mke akaamua kuita gari lije chukua vyombo kupeleka kwao. Siwezi sahau siku hiyo.Ndo siku ya mwisho kumwona mke wangu mpaka leo hii hatujaonana tena.

Vitu vilipakiwa kwenye gari ikawa inatakiwa kulipia tsh 150,000 mke wangu akataka nitoe pesa, sikuwa nayo. Wife akapiga simu kwa mdogo wake akamtumia. They left mimi nikiwa sielewi nifanye nini.

Nlitoka na gari nikaenda park sehemu nikakaa mpaka usingizi uliponipitia nlikuja shtuka saa 2 usiku sina pa kwenda kulala.mfukoni nina tsh 7000 tu. Nlitumia 1000 kununua mihogo na 6000 nikaweka kama balance. 1000 nilienda lipia wanapolaza magari.nami nikashusha kiti nikalala kwenye gari mpaka asubuhi.

Kwa siku 3 nlikuwa nahangaika sina cha kufanya. Nilipata wazo la kuwasiliana na rafiki yangu wa shule ya msingi. Nlimweleza tatizo langu akanishauri niende kwake ana chumba cha wageni nikaishi naye.

Kiukweli kwa umri wangu wa miaka 30+ nlijisikia vibaya sana.nlienda ishi naye.sikuwa na namna.

Nashukuru kuna marafiki wachache ambao hawakunitupa ktk jambo hili hata kwa kunitia moyo na mwingine kunisaidia hata pesa ya voucher au usafiri.

Katika kipindi hiki nimepoteza sana marafiki. Wengi walikata mawasiliano kabisa.hata napopiga kuwasalimia.(si kuomba pesa) wamekuwa hawapokei simu zangu.

Nmekuwa hata natuma texts kuwasalimia na sometimes kuwaomba wanikumbuke zinapotokea nafasi za ajira. Wameacha kujibu.

Binafsi nilikuwa ni mtu ninayeshirikiana na kila mtu.sikuwahi bagua mtu au mtendea mtu ubaya. Maisha yangu sikuwahi kunywa pombe au kuvuta sigara.

Nimekuwa na majonzi hasa kutengwa na familia yangu. Mke wangu amekuwa si wa mawasiliano ya karibu nami. Ni kama amesusa. Watoto kila napoongea nao wanalia na kutaka turudi kuishi pamoja. Mmoja ameamua kabisa kutoongea nami hata napoomba kumsalimia.Hataki.

Nashindwa kwenda kwa wakwe kuisalimia familia yangu. Lakini nashindwa zaidi kwenda mikono mitupu kuonana na familia yangu. Wakwe zangu hawakuwahi nisemesha lolote hata baada ya kuona mke amerudi kwao. Nimewaelewa pia kwa hilo.

Mke wangu alifanikiwa kupata kazi sehemu. Lakini bado amekuwa akitaka nimtumie pesa za matumizi hata ndogo ndogo ambazo angeweza saidia mwenyewe.nafahamu anafanya hivi kuniumiza zaidi au kuonesha kuwa ni mwanaume irresponsible.

Naumia sababu wazazi wangu ambao nlipaswa niwe nawasaidia wao ndo wanatuma pesa kiasi wapatacho kuisaidia familia yangu. (Wao wanaishi Mwanza) Baba yangu alishastaafu.hana kazi.mama yangu pia anafanya tu ufugaji mdogo mdogo.

Naishi kwa fadhila za wadogo zangu na rafiki yangu huyu ambaye namwonea huruma pia. Nina Elimu ya Degree (naomba nisitaje ya nini/nisitoe details nyingi isipokuwa kwa mtu ambaye tutawasiliana inbox privately ikiwa atakuwa na namna ya kunisaidia)

Leo nimeandika kwa majonzi thread hii baada ya kutumiwa tsh 5000 kwenye simu na msichana ambaye alikuwa housemaid wetu akiwa huko aliko na wife. Yeye ananikumbuka.

Nmeumia kwa alichoandika (baba najua unaumia huko uliko pokea hiyo hata ya vocha mimi nakuombea ufanikiwe) nmejaribu kumrudishia hiyo pesa ametuma zaidi 7000 na kutaka nitumie.

Juzi nlipata simu kwa mtu ambaye nikiwa kazini aliwahi patwa na tatizo la kikazi alipokuwa ameenda kikazi Kampuni flani na kushawishika kuiba kitu flani. Nikiwa PR nlienda shughulikia jambo hilo.bahati mbaya ushahidi ww CCTV Camera ulimwonesha yule bwna mdogo akitenda jambo hilo. Muda huo akiwa amewekwa chini ya ulinzi na gari ya Kampuni imezuiliwa. Nlimsaidia akatolewa na siku mreport kazini zaidi ya kumwonya na kumshauri.

Alionekana kujutia kosa lake sana. Mwaka na nusu umepita juzi kanikumbuka nikiwa sina hata tsh 500. Mfukoni akanitumia tsh 30,000. Nlishamsahau.akanambia tu "Boss nimekuumbuka naomba hiyo uweke mafuta" nlimshukuru sana. Hajui kama sina kazi.

Haya mambo yananiumiza zaidi na kuona nina deni zaidi kwa familia yangu,rafiki zangu na wanaonizunguka.

Ndugu zanguni. Nipo katika msongo wa mawazo. Naona i have failed my family. I have failed my parents and relatives. Nliwaza kumeza dawa nyingi sana kukatisha maisha yangu. Mara kadhaa yananijia hayo mawazo.

Nashindwa nifanye nini. Nahangaika kuomba kazi na kutafuta kazi.tatizo langu la miguu halinipi nafasi ya kufanya kazi ambayo ntasimama sana, au ntatembea sana.

Nmetengwa nimebaki peke yangu.najiona mzigo kwa huyu rafiki yangu na familia yake.naona pia nmekuwa so humiliated.

Naombeni msaada wa kazi. Kazi katika upande wa kusimamia projects,kusimamia hata madereva pia naweza kuwa dereva wa mtu(gari ndogo) gari nayotumia haiwezekani kuwa Uber najua kuna mtu anaweza nishauri hivyo.ilikataliwa kwa namna ilivyo.

Pia nina uzoefu katika kufundisha ngazi za certificates na diploma masomo ya management, customer care, social skills,communication skills, development studies.

Ni mzuri katika kuongea na kuandika pia english and swahili ( do not consider this article it is informal)

Najua watu wengine wata kebehi,watanidharau na kunikashifu.nitayapokea yote. Kwa mtu ambaye atakuwa radhi kujadiliana nami jambo hili in person nipo radhi. Nahitaji kazi niweze saidia wengine pia. Si vyema nikaendelea pokea misaada toka kwa watu wengine. Nahitaji pia kuishi na familia yangu.

Nipo Dar Es Salaam kwa sasa naishi Bunju. Asanteni"
Hebu linganisha thread yako na thread za nyuma? Mmojawapo ya mshangao ni Ile hread uliomba Ushauri wa jinsi ya kufanya threesome na wake zako watatu. Kabla hamjapost utapeli inabidi tutafakari sana. Watu kama sisi wazoezi wa upekuzi tumeshafanya kazi yetu. Nimekupekua sana toka nilipoona hii thread ya kutoa nyoka pangoni. Ingefaa ukaifuta thread haraka.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom