Nahisi kama nimefikia hatua ya Kukata Tamaa kiwango cha Mwisho. Naomba msaada wenu Ndugu zanguni

Status
Not open for further replies.

std7

JF-Expert Member
May 6, 2011
694
1,000
Hebu linganisha thread yako na thread za nyuma? Mmojawapo ya mshangao ni Ile hread uliomba Ushauri wa jinsi ya kufanya threesome na wake zako watatu. Kabla hamjapost utapeli inabidi tutafakari sana. Watu kama sisi wazoezi wa upekuzi tumeshafanya kazi yetu. Nimekupekua sana toka nilipoona hii thread ya kutoa nyoka pangoni. Ingefaa ukaifuta thread haraka.
Lile neno la utaukumiwa kwa maneno yako ndiyo hilo sasa.
 

gidlameck

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
611
500
dunia haijawahi kuwa fair pole kwa madhila unayopitia hakuna dhoruba isio na mwisho
 

April26

JF-Expert Member
Jul 14, 2020
935
1,000
Mwacheni jamani haya ni mapito, hizo zilikuwa nyakati na sasa ni wakati.
 

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
3,267
2,000
Screenshot_20201204-084229.jpg
 

Shamkware

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
1,502
2,000
Pole mwanaume mwenzetu haya ni mapito wenye nia njema na wewe watakusaidia utapata walau conection pole sana sana usichoke mkuu endelea kutafuta ajira ila wakati huo mimi nakushauri uza hilo gari ununue hata bajaji ya biashara itakayokuingizia 20 kwa siku na utafute hata nyumba ya chumba na sebule ukae mjini ndivyo palivyo nia pagumu mno sometimes mambo yanaenda tofauti kubaliana na yote mkuu
 

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,690
2,000
Binadamu tunapitia magumu mengi. Unaweza kuona yako mazito na hayabebeki kumbe kuna mwenzako ana mazito zaidi yako. Pole sana mkuu....
 

Karucee

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
16,832
2,000
You will be fine young man. Hang on there. Stay firm.in your Belief and do not at any point indulge in substance abuse.

Don't be afraid to start anywhere. And be grateful to God for each day.
 

Vera ginger

JF-Expert Member
Dec 25, 2016
1,305
2,000
" Mimi ni member wa Jamiiforums kwa kipindi kirefu kidogo. Nimekuwa nikishirikiana na kushirikishana nanyi mambo mbalimbali ya maisha na pia ya burudani. Nimewaza kwa muda mrefu sana kabla sijaamua kuandika thread hii.

Nlikuwa nmeajiriwa na Kampuni moja ya Mambo ya IT na usafirishaji pia toka mwaka 2015. Nikifanya kazi katika nafasi mbalimbali Kama Operation Manager, Public Relation Manager na pia nikisaidiana na Managers mbalimbali katika majukumu yao niki coordinate Projects mbalimbali za Kampuni.

Mwaka 2017 Kampuni yetu ilianza kuyumba. Tuliyumba sana kutokana na mambo mbalimbali ya Soko (Wateja wetu wakubwa walikuwa ni kutoka Serikalini na Makampuni Makubwa)

Tukawa kama mtu aliyepata ulemavu wa mguu mmoja. Tulijitahidi sana kupambana na kuzoea hali hiyo ya kutumia mguu mmoja. Hali iliendelea kuwa mbaya. Bahati mbaya mpaka kufika katikati ya mwaka 2019 tukawa hatuwezi hata lipana mishahara.

Tukawa tunapeana posho na hatimaye ikafika hatua hata posho ikawa ngumu. Tuliendelea kujitahidi kupambana hadi ikafikia hatukuwa na uwezo wa kulipwa kitu kabisa. Hivyo mwaka huo kuanzia mwezi wa 9 hatukuwa tunapokea anything in terms of money.na hatimaye Kampuni ikatuomba sisi wengine tuandike barua ya ku resign au tufukuzwe kazi. Binafsi nliona hali ilivyokuwa.sababu before that pia CEO alituomba tuwe free kuacha kazi.

Mimi nlikuwa katika watu wachache ambao niliamini tungepambana tukashinda hali ile.nikaomba niendelee. Nikawa natumia pesa yangu na hatimaye akiba yangu yote kwisha. Nikauza gari moja nipate pesa ya nauli na matumizi nyumbani.

Mke wangu hakuwa kazini. Nilimpa pesa Mil 6. Akafanye biashara. Bahati mbaya sana akapoteza hizo pesa zote katka biashara akichangiwa hasa na Haya makampuni ya GNLD na Q-Net. Mtaji ukaisha.

Tukaamua tena kuuza gari nyingine ili watoto waende shule na pia tujitahidi kumalizia ujenzi. Hapo tulipokuwa tunaishi pia ilibidi tulipe kodi. Hatukukamilisha ujenzi.

Nifupishe habari. Toka mwaka jana mwezi wa 9 nmepambana sana kutafuta kazi.lakini sikufanikiwa pesa hizo nlizokuwa nazo ilibidi pia niingize kwenye matibabu kwa sababu ya ugonjwa nliokuwa nao mguu wa kulia una tatizo la maumivu makali kwenye mfupa na kushoto kiasi.

Nimehangaika sana Aga Khan, Hindu Mandal na Moi. Walinipa ushauri wa kupunguza uzito na kutotembea sana (Ugonjwa unaitwa Heel Spurs) so ikabidi pia nibakize gari moja liwe ndo la kutembelea.so nikabaki na gari dogo.

Maisha yalizidi kuwa magumu na hatimaye kodi ikawa ngumu kulipa.ikapita miezi 2 mwenye nyumba akashindwa kutuvumilia. Akaja tukatoa vitu nje. Watoto wangu wawili walikuwa wanasoma Elimu ya Msingi(mmoja hajaanza bado nina watoto watatu) wakarudishwa nyumbani.

Siku tunalazimika kutoa vitu nje it was a very humiliating day. Mimi, mke,dada wa kazi na watoto wetu watatu.Mke akaamua kuita gari lije chukua vyombo kupeleka kwao. Siwezi sahau siku hiyo.Ndo siku ya mwisho kumwona mke wangu mpaka leo hii hatujaonana tena.

Vitu vilipakiwa kwenye gari ikawa inatakiwa kulipia tsh 150,000 mke wangu akataka nitoe pesa, sikuwa nayo. Wife akapiga simu kwa mdogo wake akamtumia. They left mimi nikiwa sielewi nifanye nini.

Nlitoka na gari nikaenda park sehemu nikakaa mpaka usingizi uliponipitia nlikuja shtuka saa 2 usiku sina pa kwenda kulala.mfukoni nina tsh 7000 tu. Nlitumia 1000 kununua mihogo na 6000 nikaweka kama balance. 1000 nilienda lipia wanapolaza magari.nami nikashusha kiti nikalala kwenye gari mpaka asubuhi.

Kwa siku 3 nlikuwa nahangaika sina cha kufanya. Nilipata wazo la kuwasiliana na rafiki yangu wa shule ya msingi. Nlimweleza tatizo langu akanishauri niende kwake ana chumba cha wageni nikaishi naye.

Kiukweli kwa umri wangu wa miaka 30+ nlijisikia vibaya sana.nlienda ishi naye.sikuwa na namna.

Nashukuru kuna marafiki wachache ambao hawakunitupa ktk jambo hili hata kwa kunitia moyo na mwingine kunisaidia hata pesa ya voucher au usafiri.

Katika kipindi hiki nimepoteza sana marafiki. Wengi walikata mawasiliano kabisa.hata napopiga kuwasalimia.(si kuomba pesa) wamekuwa hawapokei simu zangu.

Nmekuwa hata natuma texts kuwasalimia na sometimes kuwaomba wanikumbuke zinapotokea nafasi za ajira. Wameacha kujibu.

Binafsi nilikuwa ni mtu ninayeshirikiana na kila mtu.sikuwahi bagua mtu au mtendea mtu ubaya. Maisha yangu sikuwahi kunywa pombe au kuvuta sigara.

Nimekuwa na majonzi hasa kutengwa na familia yangu. Mke wangu amekuwa si wa mawasiliano ya karibu nami. Ni kama amesusa. Watoto kila napoongea nao wanalia na kutaka turudi kuishi pamoja. Mmoja ameamua kabisa kutoongea nami hata napoomba kumsalimia.Hataki.

Nashindwa kwenda kwa wakwe kuisalimia familia yangu. Lakini nashindwa zaidi kwenda mikono mitupu kuonana na familia yangu. Wakwe zangu hawakuwahi nisemesha lolote hata baada ya kuona mke amerudi kwao. Nimewaelewa pia kwa hilo.

Mke wangu alifanikiwa kupata kazi sehemu. Lakini bado amekuwa akitaka nimtumie pesa za matumizi hata ndogo ndogo ambazo angeweza saidia mwenyewe.nafahamu anafanya hivi kuniumiza zaidi au kuonesha kuwa ni mwanaume irresponsible.

Naumia sababu wazazi wangu ambao nlipaswa niwe nawasaidia wao ndo wanatuma pesa kiasi wapatacho kuisaidia familia yangu. (Wao wanaishi Mwanza) Baba yangu alishastaafu.hana kazi.mama yangu pia anafanya tu ufugaji mdogo mdogo.

Naishi kwa fadhila za wadogo zangu na rafiki yangu huyu ambaye namwonea huruma pia. Nina Elimu ya Degree (naomba nisitaje ya nini/nisitoe details nyingi isipokuwa kwa mtu ambaye tutawasiliana inbox privately ikiwa atakuwa na namna ya kunisaidia)

Leo nimeandika kwa majonzi thread hii baada ya kutumiwa tsh 5000 kwenye simu na msichana ambaye alikuwa housemaid wetu akiwa huko aliko na wife. Yeye ananikumbuka.

Nmeumia kwa alichoandika (baba najua unaumia huko uliko pokea hiyo hata ya vocha mimi nakuombea ufanikiwe) nmejaribu kumrudishia hiyo pesa ametuma zaidi 7000 na kutaka nitumie.

Juzi nlipata simu kwa mtu ambaye nikiwa kazini aliwahi patwa na tatizo la kikazi alipokuwa ameenda kikazi Kampuni flani na kushawishika kuiba kitu flani. Nikiwa PR nlienda shughulikia jambo hilo.bahati mbaya ushahidi ww CCTV Camera ulimwonesha yule bwna mdogo akitenda jambo hilo. Muda huo akiwa amewekwa chini ya ulinzi na gari ya Kampuni imezuiliwa. Nlimsaidia akatolewa na siku mreport kazini zaidi ya kumwonya na kumshauri.

Alionekana kujutia kosa lake sana. Mwaka na nusu umepita juzi kanikumbuka nikiwa sina hata tsh 500. Mfukoni akanitumia tsh 30,000. Nlishamsahau.akanambia tu "Boss nimekuumbuka naomba hiyo uweke mafuta" nlimshukuru sana. Hajui kama sina kazi.

Haya mambo yananiumiza zaidi na kuona nina deni zaidi kwa familia yangu,rafiki zangu na wanaonizunguka.

Ndugu zanguni. Nipo katika msongo wa mawazo. Naona i have failed my family. I have failed my parents and relatives. Nliwaza kumeza dawa nyingi sana kukatisha maisha yangu. Mara kadhaa yananijia hayo mawazo.

Nashindwa nifanye nini. Nahangaika kuomba kazi na kutafuta kazi.tatizo langu la miguu halinipi nafasi ya kufanya kazi ambayo ntasimama sana, au ntatembea sana.

Nmetengwa nimebaki peke yangu.najiona mzigo kwa huyu rafiki yangu na familia yake.naona pia nmekuwa so humiliated.

Naombeni msaada wa kazi. Kazi katika upande wa kusimamia projects,kusimamia hata madereva pia naweza kuwa dereva wa mtu(gari ndogo) gari nayotumia haiwezekani kuwa Uber najua kuna mtu anaweza nishauri hivyo.ilikataliwa kwa namna ilivyo.

Pia nina uzoefu katika kufundisha ngazi za certificates na diploma masomo ya management, customer care, social skills,communication skills, development studies.

Ni mzuri katika kuongea na kuandika pia english and swahili ( do not consider this article it is informal)

Najua watu wengine wata kebehi,watanidharau na kunikashifu.nitayapokea yote. Kwa mtu ambaye atakuwa radhi kujadiliana nami jambo hili in person nipo radhi. Nahitaji kazi niweze saidia wengine pia. Si vyema nikaendelea pokea misaada toka kwa watu wengine. Nahitaji pia kuishi na familia yangu.

Nipo Dar Es Salaam kwa sasa naishi Bunju. Asanteni"
Daahpole sana,mpk nimeumia moyo,Mungu akupe hitaji la moyo wako
Endelea kumuomba Mungu akukumbuke anapowagusa wengine
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom