Nahisi hii ni moja ya sababu ya sisi vijana kulalamika kuhusu ugumu wa maisha humu mtandaoni

AlphaMale

JF-Expert Member
Oct 26, 2019
621
1,000
Nina imani wengi wetu humu JamiiForums tumetoka kwenye familia za kawaida, nikimaanisha kuwa tumeishi na wazazi wetu kwenye nyumba za tofali hata kama zilikua za kupanga, tumekua tukiwa na uhakika wa Milo mitatu kwa siku, kila siku, na ada ya shule haikusumbua sana wazazi.

Vijana wengi tumeishi hivyo (kula na kulala bure) tangu tulipozaliwa hadi tumefikisha miaka 23 au 29 ndo tunamaliza chuo, bado hatukuwahi kujitegemea hata siku moja, hivyo ubongo wetu unafikiri labda maisha yatakuja kirahisi rahisi.

Vijana wengi wa kisasa tunaanza kujitegemea tukiwa na miaka 29, wakati wazazi wetu walianza mapema zaidi kujitegemea, kwamfano baba yangu mzazi alianza kujitegemea akiwa na miaka 12, alivofikisha miaka 12 alitoroka nyumbani kwa wazazi wake akaenda kufanya kazi, akilipwa anajisomesha mpaka akaja kupata kazi nzuri.

Nahisi vijana wengi hatuna uzoefu na suruba za maisha ndo maana tunalalamikia ugumu wa maisha na kukosa kazi humu mtandaoni, wakati wazazi wetu washazoea huo ugumu wa maisha tangu wakiwa na miaka tisa. Wazazi wetu ilikua kushinda na kulala njaa siku 3 mfululizo ni jambo la kawaida.

Kwa wazazi wetu kufanya umachinga wa kutembeza vitu barabarani ilikua jambo la kawaida, kuwa na nguo mbili tu za mtumba ilikuwa ni kawaida kwa wazazi wetu, wakati sisi vijana ikitutokea hivyo tunahisi tumelogwa na tuna bahati mbaya, tunataka tuvae kisharobaro tupendeze, kumbe wakati mwingine ndo maisha yalivyo.

Huu ni mtazamo wangu tu wa asubuhi ya leo.
 

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
29,395
2,000
Lakini zamani wazaz wetu walikua na population ndogo. Pia walikua wakitoka shule direct kwa Ajira. Sasa hivi kila kitu unachotaka kufanya wenzako walishakifanya zaman. .changamoto ni nyingi zaidi. Wenye nacho wanazidi kuwa nacho. Maskini tunazidi kudidimizwa.

Utandawazi nao umeharibu, tukiona watu wamepost lavish life tunatamani na sisi tuwe hivyo.

All in all maisha ni magumu! Lakini ukiamua kutoka moyoni kwako sio magumu.
 

tang'ana

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
9,259
2,000
Nakumbuka nilianza kujaza magunia ya pamba nikiwa na miaka 12 kipindi hicho ukijaza unapewa 100 najaza magunia yangu 5 nanunua sabuni flani zilikuwa zinaiywa B29
Umenikumbusha mbali sana mkuu. Nakumbuka hiyo ilikuwa mwaka 1995 nikiwa na miaka 7 hapo, ilikuwa bariadi huko, tulikuwa na watoto wenzangu tunashirikiana kujaza kila gunia tunapewa sh 100/=.
 

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
6,240
2,000
Umesema ukweli aa kiwango cha juu sana.

Imagine leo na hizi fursa zote za kutoboa ila tunataka kukaa kwenye ofisi kupigwa kipupwe hata kama mtu analipwa 200,000
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom