Nahau za Nape: Mkulima, nyani na mahindi

Nahau za Nape: Mkulima, nyani na mahindi

Kukataa teuzi inakuwa kama dharau kwa mh ,mtukufu rais.halileti picha nzuri
Hivi barua ya kusitishiwa uteuzi wa uwaziri wa Sanaa na Habari ilitoka? Nakumbuka ya kuteuliwa tu ambayo hata haikutaja kama mteuliwa mpya amekuja kujaza nafasi ya mtenguliwa.

Anyway, kwanini kila waziri anayetenguliwa husema sasa ana nafasi ya kuwatumikia wanajimbo wake vizuri?

Kwanini hua wanakubali teuzi ikiwa wanajua watashindwa kuwatumikia wanajimbo vizuri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao nyani watatafuta mashamba mengine huko vijijini, kwani mkulima yupo mmoja tu?.

Jamaa ana vinyongo tangu agundue kwamba RC wa Dar ana ushawishi katika awamu hii kuliko yeye aliyelala porini wakati wa kampeni.
 
Hapa wengi mnapaogopa kwanini?
Nape ni ccm damu tena ile inayowaita wafadhili wa miradi mbalimbali na bajeti mabeberu lakini yeye leo kawabatiza na kuwaita wakulima.
Wananchi mliokuwa mnaifaidi misaada ya wafadhili walioitwa mabeberu na kisha wakulima sasa wana jina jipya ambalo ni nyani!
Sasa wafadhili ( mabeberu/ wakulima) wameondoa michango na misaada yao kwenye bajeti na miradi ambayo leo imeitwa mahindi na kilichofuata ni wananchi/ nyani kufa njaa na kutambua umuhimu wa wafadhili/ wakulima!
Upo sahihi Nape kwani wananchi/nyani njaa hii ikiendelea hivi kwa miezi sita ijayo ule mkanda wa mwl. Nyerere wa mwaka 1979-80s haukwepeki lazima tuufunge na kuukaza sana hadi utukate kiuno!
Mkulima=Mfadhili
Nyani=Watendaji wanaoamini wafadhili Ni Mabeberu
Mahindi=Fedha za Miradi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkulima alikuwa na faida gani kwa nyani kama mahindi yake walikuwa wanafukuzwa wasile?

Nape amechemka.
Wewe ndio hujui fasihi kabisa bora urudi shule ukasome. Hapa anamaanisha nyani walikua wajinga kushangilia kifo cha mkulima aligekua akiwafukuza wakila mahindi kwa kuibia sasa kufa kwake hata hayo mahindi ya kuiba hakuna tena. Nyani walimuona mkulima kama adui kumbe walikua wananufaika wao na sio mkulima
 
nape nae aache utotoo,yeye kila siku kuandika viji nahau tuuu.kama anajiaamini aache kujificha kwenye hivyo vinahau nahau.

kwanza watu wenyewe wa kutafakari nahau zake wako wapi?.
 
hapana, nyani hawezi kulima, lakini hata wakati mkulima analima mahindi hayakuwa na manufaa yeyote kwa nyani, yalikuwa yanalindwa na mwenyewe.

Kwenye reading comprehension hutakiwi kuongeza ya kwako kutoka kichwani. Tumeambiwa nyani walikuwa wanafukuzwa!

Mkulima kafa, na afe, what difference does it make? We weren’t getting the corn anyhow.
They always get some, they wanted it all.
 
Kama walikuwa wanakula mahindi mkulima alipokufa basi hakukuwa na njaa, na hakuna nahau wala somo lolote hapo...
Nyani wanakula mahindi! Somo ni wao kufanya sherehe kwa kifo kile bila kujuwa ndipo wanapopata mlo.
 
nyani walikua wajinga kushangilia kifo cha mkulima aligekua akiwafukuza wakila mahindi kwa kuibia


Wapi imesemwa nyani walikuwa wanakula mahindi?


Kinyume na hivyo, nyani walikuwa wanafukuzwa!
 
Kwenu,

Mh. Nape, mbunge wa Mtama ametoa nahau inayofikirisha watu wengi, hasa viongozi,mara baada ya kujiuzulu uenyekiti kwenye kamati nyeti ya Maiasili na Utalii.

Nahau ni hii, "Nyani waliposikia aliyekuwa akiwafukuza wasile mahindi amekufa, walishangilia Sana. Mwaka uliofuata walipata njaa kali maana hakukuwa na mahindi. Ndipo walipogundua kuwa mtu aliyekufa alikuwa mkulima.

Nani ni nyani? Nani Mkulima? Mahindi ni nini?

TS.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haaa mhe nape umeona hili, wakati ulikuwa kada wa ccm hukujua hili, lakini naona uko sawa maana sasa usakuwa na akili, hongera sana
 
Ziliponunuliwa bombardier wapiga kura walimuuliza wao zitawasaidia nini..vipi baada ya kununua dreamliner na air bus na ujenxi wa stieglars gorge na SGR..hawajauliza tena?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom