Nahau za Nape: Mkulima, nyani na mahindi

Toosweet

JF-Expert Member
May 27, 2012
2,141
1,982
Kwenu,

Mh. Nape, mbunge wa Mtama ametoa nahau inayofikirisha watu wengi, hasa viongozi,mara baada ya kujiuzulu uenyekiti kwenye kamati nyeti ya Maiasili na Utalii.

Nahau ni hii, "Nyani waliposikia aliyekuwa akiwafukuza wasile mahindi amekufa, walishangilia Sana. Mwaka uliofuata walipata njaa kali maana hakukuwa na mahindi. Ndipo walipogundua kuwa mtu aliyekufa alikuwa mkulima.

Nani ni nyani? Nani Mkulima? Mahindi ni nini?

TS.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajuaje mkulima alikuwa halindi shamba usiku?

Mkulima marehemu au hai yote sawa kwa Nyani kwa vile mahindi yenyewe walikuwa hawayali anyhow.

Nape kajichanganya.
Let other things remain constant akuna jinsi ya kulinda shamba ata iwe 24 hrs nyani hasiibe ata hindi moja.
 
Unajuaje mkulima alikuwa halindi shamba usiku?

Mkulima marehemu au hai yote sawa kwa Nyani kwa vile mahindi yenyewe walikuwa hawayali anyhow.

Nape kajichanganya.
Waliyala mkulima alipokufa. Wewe ndo unajichanganya.
 
Hivi barua ya kusitishiwa uteuzi wa uwaziri wa Sanaa na Habari ilitoka? Nakumbuka ya kuteuliwa tu ambayo hata haikutaja kama mteuliwa mpya amekuja kujaza nafasi ya mtenguliwa.

Anyway, kwanini kila waziri anayetenguliwa husema sasa ana nafasi ya kuwatumikia wanajimbo wake vizuri?

Kwanini hua wanakubali teuzi ikiwa wanajua watashindwa kuwatumikia wanajimbo vizuri?
 
Back
Top Bottom