Nape Nnauye ajiuzulu Uenyekiti wa Kamati ya Maliasili na Utalii

  • Thread starter Mwanahabari Huru
  • Start date

Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Messages
13,950
Likes
30,768
Points
280
Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2015
13,950 30,768 280
Mhe Nape amejiuzulu uenyekiti wa kamati ya mali asili baada ya kuwekwa kitimoto na chama. Habari zinasema ni baada ya kukataa kuondoa taarifa ya uchukuaji wa mashamba ya wawekezaji kinyume na sheria.

--------------

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amejiuzulu Uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili na Utalii. Kujiuzulu kwake, kunatokana kile kinachodaiwa ni “Kugoma kuondoa taarifa ya uchukuaji wa mashamba ya wawekezaji, kinyume na sheria.”

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii zinasema, Nape amejiuzulu baada ya kutofautiana na serikali kuhusu ripoti ya Kamati yake.

“Nape alitaka ripoti ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii, iliombe Bunge kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge ili kuchunguza utaratibu uliotumika wa kufuta mashamba ya watu,” ameeleza mjumbe mmoja wa kamati hiyo.

Ameongeza, “Serikali haitaki kuundwa kwa Kamati hiyo. Hivyo imeamua kuitumia Kamati ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumlazimisha Nape kujiuzulu.”

Taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii zinasema, tayari Nape amemuandikia barua rasmi ya Spika kumjulisha kujiuzulu kwake.

Nape alihuhutubia waandishi wa habari leo akiwa chini ya vyombo vya usalama na kutetea msimamo wake.

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja siku moja kabla ya Kamati yake kuwasilisha ripoti yake na zinaeleza kuwa Kamati hiyo ilikuwa inaleta mapendekezo ya kuundwa kwa Kamati Teule, jambo ambalo lilihofiwa kuwaumbua baadhi ya wakubwa.

Machi mwaka 2017, Nape aling’olewa kwenye nafasi ya uwaziri wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo.

Mbunge huyo wa Mtama mkoani Lindi, alivuliwa wadhifa wake siku moja baada ya kupokea ripoti ya Kamati ya uchunguzi juu ya tukio uvamizi wa kituo cha televisheni cha Clouds kwa kutumia silaha uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Ripoti ya kamati aliyoiunda Nape kuchunguza tukio hilo, ilithibitisha kuwa Makonda alivamia kituo hicho majira ya saa 5 usiku wa Ijumaa ya tarehe 17 Machi 2017 na alifanya uvamizi huo akitumia askari wenye silaha. Nape aliahidi kulifikisha ripoti yake kwa mamlaka ya juu yake. Haijajulikana mpaka sasa, ripoti hiyo amekabidhiwa nani.

Nape ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Idara ya Uenezi ya CCM, amesema atapata nafasi nzuri ya kutumikia wananchi wa jimboni wake baada ya kuachia nafasi hii.
 
jingalao

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Messages
28,307
Likes
19,071
Points
280
jingalao

jingalao

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2011
28,307 19,071 280
Mhe Nape amejiuzulu uenyekiti wa kamati ya mali asili baada ya kuwekwa kitimoto na chama. Habari zinasema ni baada ya kutaa kuondoa taarifa ya uchukuaji wa mashamba ya wawekezaji kinyume na sheria.
Kwa hiyo kawa mtetezi wa wawekezaji hewa?
 
Fullfilledtruth

Fullfilledtruth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2018
Messages
1,908
Likes
1,279
Points
280
Fullfilledtruth

Fullfilledtruth

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2018
1,908 1,279 280
Mmawia

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Messages
68,260
Likes
30,870
Points
280
Mmawia

Mmawia

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2013
68,260 30,870 280
Mhe Nape amejiuzulu uenyekiti wa kamati ya mali asili baada ya kuwekwa kitimoto na chama. Habari zinasema ni baada ya kukata kuondoa taarifa ya uchukuaji wa mashamba ya wawekezaji kinyume na sheria.
Mungu ibariki Tanzania

In God we Trust
 
FORTALEZA

FORTALEZA

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Messages
2,034
Likes
3,031
Points
280
FORTALEZA

FORTALEZA

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2017
2,034 3,031 280
Tulitegemea hilo siku nyingi。

Na sasa kinatafutwa kile kichwa cha mzee wa singeli, sidhani kama atapona mtego waliomuwekea.

Msinihoji wala kuniuliza maswali, muda ni mwalimu mzuri sana. Mtajionea.
 
Waziri wa Kaskazini

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2015
Messages
2,852
Likes
4,634
Points
280
Waziri wa Kaskazini

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2015
2,852 4,634 280
dah
 
Mmawia

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Messages
68,260
Likes
30,870
Points
280
Mmawia

Mmawia

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2013
68,260 30,870 280
Tulitegemea hilo siku nyingi。

Na sasa kinatafutwa kile kichwa cha mzee wa singeli, sidhani kama atapona mtego waliomuwekea.

Msinihoji wala kuniuliza maswali, muda ni mwalimu mzuri sana. Matajionea.
Yeyote yule anayejiona amesimama basi ategemee kudondoka wakati wowote ule

In God we Trust
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Messages
23,827
Likes
53,522
Points
280
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2015
23,827 53,522 280
Mhe Nape amejiuzulu uenyekiti wa kamati ya mali asili baada ya kuwekwa kitimoto na chama. Habari zinasema ni baada ya kukata kuondoa taarifa ya uchukuaji wa mashamba ya wawekezaji kinyume na sheria.
Bado kidogo wote ccm na upinzani tutajua umuhimu wa utawala bora
 
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
56,778
Likes
51,815
Points
280
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2012
56,778 51,815 280
Mhe Nape amejiuzulu uenyekiti wa kamati ya mali asili baada ya kuwekwa kitimoto na chama. Habari zinasema ni baada ya kukata kuondoa taarifa ya uchukuaji wa mashamba ya wawekezaji kinyume na sheria.
Shetani hana rafiki
 

Forum statistics

Threads 1,262,481
Members 485,588
Posts 30,123,421