Toa ngoma ipo Kigamboni kwahyo Unatakiwa kupanda gari inayokwenda Feri (Kivukoni) Yameandikwa T/Ngoma. Kigamboni ! Ukishuka hapo utavuka kutumia Kivuko mpaka upande wa Pili Panda mwendokasi ushukie kituo kinaitwa Ubungo maji! Ukiwa ndani ya basi ya mwendokasi omba msaada kwa abiria mwenzio akukumbushe kituo cha ubungo maji ushuke! Ukishashuka Panda Bodaboda (nauli buku) mwambie akupeleke chuo udsm! Au kama una mizigo mingi nakushauri siku ya kwanza nenda mikono mitupu kufanya uchunguzi upajue kwanza then baadae ufate mizigo yako ndo uende sio ubebe matranka na mabegi unaenda sehemu usiyoijua utapata tabu saana!
N.B: Nauli T/ngoma mpaka Kigamboni - 600
Nauli ya kivuko - 200
Nauli ya Mwendokasi - 650
BodaBoda kutoka ubungo maji mpaka udsm nauli - 1000
Nakutakia safari Njema
Umemshauri Vizuri Sana Kutoka T/Ngoma Mpaka UDSM.
Mimi Namuongezea Kwa Sehemu Ulioiacha.
• Kutoka TUNDUMA Mpaka UBUNGO (DAR) utafika SAA MBILI usiku au Zaidi.
• Ukishafika UBUNGO utaona Daraja (Flyover) watu Wanapanda Juu Kwahiyo Nawewe Panda Juu halafu Shukia Kwa Ndani Utakata Tiketi Ya Mwendo Kasi (Basi) Kwa Shilingi 650/=.. Lakini Kwa Muda Huwo Mabasi Yanajaa Nyomi Kwahiyo Likisimama tu Basi Kimbilia Uingie Hivyohivyo.
• Ukiwa Ndani Ya Mwendo Kasi Ukiangalia Kwa Dereva Kule Juu ya WindScreen Basi linasoma Vituo Vyote Linavyosimama.
Wewe Hakikisha Unashuka Kituo Cha Mwisho Kabisa Ambacho Basi Litasoma
Final Destination Ferri Terminal.
• Ukifika Ferri Shuka Utaona Watu Wanakoelekea Kutoka Hapo Stand, Then Elekea Upande Wa Pwani Utaona Bango Kubwa Hivi then Mbele Ya Hilo Bango ndiyo Utaelekea Kukata Tiketi Ya Kivuko Kwa Sh. 200/= Na Kuingia Jengo la Abiria.
Note: Tiketi Za Kivuko Kama Hujawahi Kuzitumia Zinaweza Zikakuzingua Wakati Wakuingia Kwenye Jengo la Abiria Kwani Zinasoma Kielectronic. Kwahiyo Zikikuzingua Basi Angalia Upande Wa Kushotoni Utakuta Kuna Uwazi Wewe Pita tu Kwanye Huo Uwazi, Haina Shida Wala Usijali.
• Lango la Jengo la Kusubiria Abiria Likifunguliwa tu Utaona Watu Wanakimbilia Kwenye Kivuko, Lakini Wewe Hata Usijilazimishe Kukimbilia Bali nenda Taratibu tu Mpaka Ndani Ya Kivuko.
• Kivuko Kikishafika Upande Wa Pili Abiria Nyote Mutashuka...
Ukishashuka Fuata Abiria Wenzio Wanakoelekea Mpaka Nje Ya Geti Utakutia Njia Panda;
Njia Moja imeelekea Kushoto Na Nyengine imeelekea Kulia. Hakikisha
Unaiacha Njia Ya Kushoto Usiifuate, Na hapo
Fuata Njia Ya Kulia.
Hiyo Njia Ya Kulia ifuate Moja Kwa Moja Bila Ya Kupinda Popote baada Ya Masafa Kama Ya Mita 150m hivi itakupeleka Mpaka Stand Kuu ya Kigamboni.
Njiani Kuelekea Stand Na Hapo Stand Wenyewe Muna Biashara Kibao za Vyakula, Vinywaji na Matunda Kama Una Ubao Basi Unaweza Ukajipendelea tu.
Hapo Stand Tafuta Gari iliyoandikwa
T/NGOMA - FERRI. Ukishapanda Gari ya Abiria Mpigie Simu Mwenyeji Wako Ushuke Gari Kituo Gani then Yeye atakusubiri Hapo.
Note: Hakikisha Usije Ukapanda Gari ya KIBADA - FERRI utaishia Njiani Kibada Stand.