Habari!
Napenda nitoe shukrani zangu kwa wale wote walioamua kuchukua jukumu la kufuatilia ili kujua zaidi kuhusu nafasi tajwa! Baada ya majibu yenu nimefuatilia na kujua kuwa nimewahi kutoa taarifa kabla ya taarifa rasmi kufika ngazi za chini kabisa yani kwa washauri wa migambo wilaya na watendaji! Kwa mfumo wa taarifu nilijua kuwa kwa sasa zitakuwa zipo huko tayari, lakini la hasha! Kwa taarifa nilizofuatilia jioni hii ni kuwa kwenye meza za washauri wa migambo wa wilaya bado taarifa hizi hazijawafikia rasmi, mpaka jumatatu! Samahani kwa hilo!
Cha msingi ni kwamba kwa ngazi za juu inafahamika! Nadhani pamoja na kuwahi kutoa taarifa bila kuzingatia kama zimefika ngazi ya chini ama la (nimeshaomba radhi kwa hilo) pia kuna manufaa! Hii inamanisha wewe uliyekuwa na lengo la kujiunga na JKT usikae mbali na ofisi za mkuu wa wilaya ama mtendaji wako wa kata.
Nimefurahi kuona kumbe sio wote wanaopenda kukaa kwenye mitandao na kubishana bila kuthibitisha jambo, hiyo ndio akili!
Nimejaribu kujibu maswali kadri ya uwezo na uelewa wangu, kwa yule ambaye anaona sijamtendea haki ama kumjibu ipasavyo samahani! Kwa walioni-PM nao vile vile nimejitahidi kuwasaidia!
Kwa uchambuzi wangu wa haraka haraka nimegundua hili:
HOFU YA AJIRA! Kwa wanaotaka kujiunga JKT. Pamoja na replies zangu na wadau wengine hapo juu naomba nijibu swali hili kwa ujumla
Kwanza sio kweli kama ilivyodaiwa na mdau mmoja hapo juu eti taasisi kama TAKUKURU, JWTZ ama MAGEREZA hawachukui wahitimu wa JKT wenye degree, huo ni uzushi! Elimu inapewa kipaumbele kuliko kitu chochote kwa sasa! Wanazingatia sana elimu.
Pili: napenda kuweka wazi kuwa ni kweli kuna watu wana degree lakini baada ya kuhitimu hawajachukuliwa, ila ebu waulize wana-proffesional gani? Napenda nirudie kauli yangu ya awali "probability ya ajira kwa proffesional is higher lakini pia itategemea umesomea nini"! Je sikujibu hivyo? Mulize alieachwa kasomea nini? Wewe ni mhitimu una B.A mfano ya MicroFinance Institution Management alafu unandika barua ya kuomba JWTZ! Jeshi halina taasisi ndogo za fedha za kutoa mikopp, kuna vyama ambavyo ni vichache sanaa! Sasa hata wewe ungekuwa recruiter, ungemchukua huyo mtu? Nani mwenye B.A ya Account, ama Procurement ama Public admistration ambae baada ya kuhitimu JKT ameomba JWTZ na akaachwa? Kama yupo ni-PM nambie yupo kambi gani!
Napenda kusema mengi lakini kwa sasa inatosha!
Nawatakia majadiliano mema, sintekuwepo kuendelea kujibu maswali yenu, lakini unaweza ni-PM na pindi nitakaporudi nitajibu,
Ahsante..
Mimi ni Mtanzania, wajibu wangu ni kua mtiifu, muadirifu na muwajibikaji, wewe je?