Nafasi za kujitolea JKT kwa vijana

Nafasi za kujitolea JKT kwa vijana

Status
Not open for further replies.
Joined
Sep 10, 2013
Posts
76
Reaction score
21
Habari.

Napenda kuchukua nafasi hii kukutaarifu wewe kijana wa kitanzania kuwa nafasi za kujiunga na JKT (maarufu kama nafasi za kujitolea zimetoka)
Utaratibu upo kama ifuatavyo:

*Nafasi hizi zimetolewa kwa kila mkuu wa wilaya TZ
*Wakuu wa wilaya watazisambaza kwenye ofisi za kata wakitoa idadi elekezi kwa kila kata kama inavyohitajika
*Vijana wataomba kupitia kwa watendaji
Vigezo:

i) Uwe ni mtanzania
ii) Uwe na umri usiozidi miaka 23
iii) Uwe na afya njema
Kwa maelezo mengine fika katika ofisi ya mshauri wa mgambo wa wilaya ambayo inakuwaga ndani ya majengo ya ofisi za mkuu wa wilaya

JKT
Kwa uzalendo, Tujenge Taifa Letu

=============================

ONYO: HII HABARI SI YA KWELI NA IMEKANUSHWA NA JKT MAKAO MAKUU

mwenge1.jpg

​
TANGAZO
​

MAKAO MAKUU YA JESHI LA KUJENGA TAIFA LINAKANUSHA HABARI ILIYOTOLEWA NA MTANDAO WA JAMII FORUM KUWA NAFASI ZA VIJANA WA KUJITOLEA ZIMETANGAZWA.HABARI HIYO IMETUMWA NA MTU ANAYEJIITA MTANZA MWENYE NIA TAREHE 24 SEPTEMBA 2014.

UKWELI NI KWAMBA NAFASI HIZO HAZIJATOLEWA NA TAARIFA HIYO SI SAHIHI, HAKUNA KITU KAMA HICHO.AIDHA, IFAHAMIKE MATANGAZO YOTE YAHUSUYO JESHI LA KUJENGA TAIFA HUTANGANGAZWA KWENYE TOVUTI YA JKT AMBAYO NI WWW.JKT.GO.TZ.

AMA NA MKUU WA JKT KUPITIA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MAKAO MAKUU YA JKT TAREHE 25 SEPTEMBA 2014.
 
Samahani naomba unisaidie kujua kwamba wanajitolea alafu badae wanapata ajira au wakishajitolea mwisho wake ni upi
 
Ni swali zuri!
Mfumo wa JKT upo ivi, mafunzo ni miez 6 Kisha muda wa kuwa kambini ukijitolea ni miezi 3! Baada ya hapo, taasisi kadhaa za serikali ikiwemo JWTZ, TAKUKURU,UHAMIAJI, POLISI, MAGEREZA na ZIMA MOTO huja kwenye kambi za mafunzo kufanya recruitment kwa vijana wahitimu! Ukweli ni kwamba kwa mfumo wa sasa wa uajiri kama una ndoto ya kufanya kazi kwenye taasisi tajwa hapo juu, ni lazima upitie JKT. Kwa ufupi ni kwamba hakuna mwenye elimu ya kutosha (mf: certificate, diploma n.k) anaemaliza mafunzo ya awali JKT kisha anarudi mtaani. Am inside the system and that is my assurance.
 
Samahani mkuu hivi hapo kwenye umri watu wenye degree/shahada itakuaje?
 
Asante sana kwa ufafanuzi wenye kujitosheleza.
 
Unamaanisha mwenye certificate na diploma lazima aajiliwe au umemaanisha nini
 
hili zoezi hadi kukamilika hakika watu watakuwa wamejenga nyumba kwa rushwa.
 
haya mambo yapo ya watu kupoteza maisha japo hufanywa kuwa siri kubwa
 
Samahani mkuu hivi hapo kwenye umri watu wenye degree/shahada itakuaje?

Ki ukweli nafasi hizi ni za wenye umri chini ya miaka 23 hivyo bhasi kama una Bachelor degree and you meet age criteria apply! Ila itakupasa utumie cheti cha form six wakati wa kujiorodhesha! Hii ni kwa sababu maagizo waliyonayo watu wa chini ni kuchukua watu mpaka ordinary diploma tu! Ila ukichaguliwa ukifika kambin wakati wa particulars analyzation utaandika you hold Bachelor Degree
 
Unamaanisha mwenye certificate na diploma lazima aajiliwe au umemaanisha nini
Sijamaanisha ni lazima aajiriwe ila nnachokisema "employment probability for proffessional candidates is higher than 99%" Ingawaje pia itategemea una certificate/diploma ya nini!
 
nackia mafunzo ni magumu mpaka watu wengine wanakufa huko mafunzoni

Kabla ya kuanza mafunzo watahiniwa wote upimwa afya zao! JKT ni taasisi ya serikali, hakuna serikali inayoweza kuangalia raia wake wakiuwawa ama yenyewe kuendesha mauaj! Endapo watahiniwa wanafariki, Watahiniwa hawafi kwa sababu ya mafunzo, labda ni magonjwa n.k
 
Sijamaanisha ni lazima aajiriwe ila nnachokisema "employment probability for proffessional candidates is higher than 99%" Ingawaje pia itategemea una certificate/diploma ya nini!

Sawa sawa ila walio na degree na diploma wengi wako above 23, haya walio chini ya 23 wachangamkie fursa
 
Bwana
Mtanza Mwenye Nia
Nina ndugu yangu amefeli form four 2012, umri miaka 22.
je? na yeye anaruhusiwa kisheria

Maana sitaki aendelee kumbaki mtaani,
 
Last edited by a moderator:

Kwenda mafunzoni JKT kisha kujitolea hapo inawezekanaa. Lakini ajira itategemea kama kuna taasisi itayohitaji watu wenye vigezo kama vyake!
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom