Nafasi za kazi Qatar

Nafasi za kazi Qatar

Mtindo huo wa upendeleo haupo huku tu.Kuna viwanda hapa tz vinavyofanya mambo haya kinyemela.Kuna nafasi special kabisa kwa ajil ya watoto wa mama mdogo.Watoto wa mama mdogo wanapendelea kubebwa kama wabunge wa viti maalumu.Inshort wanataka vipaumbele kama wao ni kundi maalumu.M mwenyewe kwa mtindo huu naona heri ziwe sirekal 3.
 
Hahaha hiyo kweli sam hawafai hao,bora wangetangaza msikitini na kwenye mihadhara yao
 
Nilikuwa naunga mkono serekali mbili zenye maboresho.Lakini kutokana na tangazo nilolikuta katika JUKWAA LA NAFASI ZA KAZI NA TENDA.Likitangaza nafasi za kazi huko uarabuni ambako watakuwa wenyeji wa fainali za kombe la dunia miaka ijayo.
MLeta tangazo amesitiza nafasi ni kwa ajiri ya wanzanzibar tu tena waislamu peke yao,wazenj wakristo hawana sifa.Watu wa tanzani bara hatuna nafasi kabisa hata kama ni mwislamu mwenzao.Swali nalojiuliza mbona nafasi za kazi alizotangaza yule mmbunge wetu wa huku za kule uarabuni akuwalenga watanganyika tu peke yao bali watanzania wote.
Mi nadhani kama tumefikia hatua hii ya kubaguana sioni maana ya muungano au tuwe na serekali 3 na muungano uwe ni shirikisho tu la mambo mengine.
 
Ndugu yangu, waswahili wanamsemo wao usema, uliyekunyima dengu kakupunguzia ushu..z! Kukunyima kufanya kazi arabuni, kukupunguzia madhira yaliyowapata babu zetu waliopelekwa utumwani kwa karne mbili lakini hakuna hata mtu mweusi wa asilia kama ilivyo kwa amerika ya kusini na kaskazini. Usiniulize walikuwa wanafanyajwe hadi hakuna aliyeacha mbegu nyeusi kule.
 
Sultani na ndugu zake waarabu bado wanaitamani Zanzibar, na wanafanya mbinu za kila aina ili waipate tena!
 
Asalaam alaikum,

Nafasi za kazi Qatar Flour Mills,(QATAR) kwa Muslim tu.

Kwa niaba ya Qatar Flour Mills napenda kuwatangazia wazanzibar wenzangu waliopo hapa Qatar au Zanzibar nafasi za kazi kwa vijana wote,Kazi za Usindikaji,Usambazaji,upakiaji na nyingine nyingi,Mshahara ni mzuri sana na pia kuna makazi ya bure kwa wafanyakazi.

Masharti ya muombaji ni pamoja na;

.Awe na umri kati ya miaka 18 na usiozidi miaka 35.

.Awe na Elimu ya Msingi na kuendelea.

.Mwaminifu na upo tayari kujituma katika kazi.
.Hizi nafasi ni kwa Wazanzibar tu na Uwe ni Muslim.

Kwa Maelezo zaidi tuma CV yako kwa;

Qatar Flour Mills Co. P.O.Box: 1444, Doha, Qatar

Email: fatma@qualityservice.com

iMETOKA KATIKA UKURASA WA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU ZANZIBAR.
link : http://www.facebook.com/[color=red]UamshoJumuiyaYaMihadharaYaKiislamuZanzibar[/color]

"TISS PANDIKIZENI VIJANA WA KAZI"

la sivyo...!
 
‎ ‎: حركة الشباب المجاهدين‎
 
الشباب
 
200px-ShababAdmin.svg.png
 
Vipi kuhusu taasisi kama WORLD VISION mbona hutangaza kazi zao kwenye PUBLIC lakuni ni WAKRISTO tu ndio wanaopewa.......Hayo hamuyaoni au huo sio ubaguzi....Hiyo kazi imetangazwa kutoka kwenye taasisi ya kiislam tena ya Zanzibar kwa hiyo inawahusu tu wahusika...tena bora wao wameweka wazi ili kupunguzia watu usumbufu.
 
Back
Top Bottom