Nafasi za Kazi: Afisa Mauzo na Meneja Masoko Mikoa Mbalimbali

Boreless

Member
Aug 25, 2009
61
39
Kampuni yetu inayojishughulisha na utengenezaji wa vinywaji vikali na wines inazo nafasi za kazi zilivyotajwa hapo juu katika mkoa wa Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi na Shinyanga, Simiyu na Geita.

Tunakaribisha maombi kutoka kwa watu wenye sifa zifuatazo:
  • Ubunifu wa mikakati ya kutafuta, kujenga, kuimarisha masoko na kudumisha wateja.
  • Uwezo wa kujieleza kwa ufasaha na stadi za kuwasilisha mada kwa kuendana na hadhira.
  • Uenyeji na utengamano mzuri na wadau wa vinywaji kama vile wauzaji vinywaji kwa jumla, rejareja, bar, hotel n.k
  • Tabia ya kuanza kazi kwa kuweka malengo na kuyafikia bila kutafuta sababu za kushindwa.
  • Uaminifu juu ya pesa, mali na asiye na historia ya wizi au dhuruma.
  • Asiye na kikwazo cha kiimani katika uuzaji wa bidhaa aina ya pombe.
  • Umri wa kuzaliwa usiozidi miaka 28.
Mwenye sifa zilizotajwa hapo juu anaweza kutuma maombi kwa kuandika barua pepe akieleza wasifu, uzoefu katika tasnia ya masoko na mauzo, na mkoa anaopenda kupangiwa. Pia aambatanishe na anwani yake kamili ikiwa na njia zote za mawasiliano.

Maombi yote yatumwe kupitia kwenda kwenye barua pepe: tanvanille@gmail.com na kutufikia kabla ya Jumatatu, tarehe 5/12/2016
 
Mimini dereva mwenye uzoefu usiyo pungua miaka sita nitafurai sanakama nitapata kazikwenu 0785837710
 
Nimetuma ngoja nisubilie majibu kama yakiwa chanya itakuwa jambo jema kwa kweli.
Kuchezea mtaa f.c si mchezo
 
Tangazo halipo clear,
Natamani ungeitaja Jina la kampuni, Anwani yake na Kazi zake!
Vinginevyo jitahidi kurekebisha!
 
Kampuni yetu inayojishughulisha na utengenezaji wa vinywaji vikali na wines inazo nafasi za kazi zilivyotajwa hapo juu katika mkoa wa Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi na Shinyanga, Simiyu na Geita.

Tunakaribisha maombi kutoka kwa watu wenye sifa zifuatazo:
  • Ubunifu wa mikakati ya kutafuta, kujenga, kuimarisha masoko na kudumisha wateja.
  • Uwezo wa kujieleza kwa ufasaha na stadi za kuwasilisha mada kwa kuendana na hadhira.
  • Uenyeji na utengamano mzuri na wadau wa vinywaji kama vile wauzaji vinywaji kwa jumla, rejareja, bar, hotel n.k
  • Tabia ya kuanza kazi kwa kuweka malengo na kuyafikia bila kutafuta sababu za kushindwa.
  • Uaminifu juu ya pesa, mali na asiye na historia ya wizi au dhuruma.
  • Asiye na kikwazo cha kiimani katika uuzaji wa bidhaa aina ya pombe.
  • Umri wa kuzaliwa usiozidi miaka 28.
Mwenye sifa zilizotajwa hapo juu anaweza kutuma maombi kwa kuandika barua pepe akieleza wasifu, uzoefu katika tasnia ya masoko na mauzo, na mkoa anaopenda kupangiwa. Pia aambatanishe na anwani yake kamili ikiwa na njia zote za mawasiliano.

Maombi yote yatumwe kupitia kwenda kwenye barua pepe: tanvanille@gmail.com na kutufikia kabla ya Jumatatu, tarehe 5/12/2016
Nimechelewa aiseee!
vipi mkuu naweza kutuma au wamepatikana wa kutosha?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom