Nafasi za JKT 2016 zitatoka lini?

Nafasi za JKT 2016 zitatoka lini?

Status
Not open for further replies.
Tatizo la watz wenzangu huwa hatutaki kuambiwa ukweli..me nimewaambia hii ishu ya jkt ni mpaka mwezi wa 6 au 7 baada ya budget,lakini nimeishia kutukanwa kwa kuitwa tapeli.poa,nyie endeleeni kupeana false hopes humu.ila ukweli ni kwamba operation magufuli itaanza kuchukua watu mwezi wa 6 au wa 7 mwanzoni.
 
Kuchukua una maana ya kufanya usaili au kureport makambini ni mwezi wa 6-7?
 
mchakato utaanza mwezi wa 4 ili mkaripoti makambini pamoja na vijana wa mujibu wa sheria.ila sasa vijana hamtaki kuambiwa ukweli.nawaambien tena,msipeane matumaini hewa vijana.hizi taarifa ninazoziandika hapa nina uhakika nazo 99.9%.
 
mwaka jana mchakato ulianza mwezi wa 12 na wameripoti wa 7...
 
mwaka juzi ulianza mwezi wa 12 na wakaripoti wa 4...
 
jeshi halina mtaala mda wowote wanaweza wakaamua lolote....
 
magufuri kasema nafasi hizo hamna hadi ipite miaka miwili uchumi ukitengamaa ndo wataanza kuwachukua.
 
TAARIFA KWA UMMA TANGAZO TOKA JKT
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), linapenda kuutaarifu umma, kuzipuuza taarifa potofu zinazosambazwa mitaani na katika mitandao ya kijamii kuwa, JKT limeanza kuandikisha vijana wa kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa Kujitolea kwa mwaka 2016.

Taarifa hizo siyo sahihi na wananchi wanatakiwa kupuuza upotoshaji huo wenye sura ya utapeli unaofanywa na kikundi kidogo cha watu. Aidha, yeyote anayedai kupewa fedha ili aweze kumuingiza kijana katika Jeshi la Kujenga Taifa aripotiwe mara moja Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa.

Katika hili unahitajika ushirikiano wa karibu sana ili kuweza kudhibiti udanganyifu na utapeli unaofanywa na watu wachache wanaojifanya wana uwezo wa kuwaingiza vijana JKT, na kudai watumiwe fedha kupitia mitandao ya simu za mikononi kama vile Tigo Pesa, M- Pesa, Airtel Money.

JKT linasisitiza kuwa, muda wa kuanza mchakato wa kuchukua vijana wa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea utakapowadia, wananchi watatangaziwa rasmi kupitia Mamlaka za Serikali zinazohusika pamoja na vyombo vya habari hapa nchini. Aidha inazidi kukumbushwa kuwa nafasi za vijana kujiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea hazipatikani kwa kununuliwa.

IMETOLEWA NA

KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO,

MAKAO MAKUU YA JESHI LA KUJENGA TAIFA,

LEO TAREHE 08 JANUARI 2016
 
kuweni makini,wahuni wanaweza kutumia hata hii thread kutapeli watu...
 
Back
Top Bottom