Nafasi ya kazi ya Usimamizi "Manager" wa kiwanda kidogo

Abdul Ghafur

JF-Expert Member
Sep 18, 2017
610
733
Abraar Bricks Nyumba kwa wote.

Katika kiwanda chetu cha uzalishaji vifaa vya ujenzi wa kisasa kwa kutumia saruji (precast) tunatafuta msimamizi "manager" wa kiwanda.

Kiwanda kina uwezo wa kuwa na wafanyakazi wa uzalishaji 21 na wasio wazalishaji 3 kwa shift moja. Tunataraji kifikie uwezo wa kufanya kazi shifts tatu kila siku.

Kiwanda kina uwezo wa kuunda bidhaa zaidi ya aina 50 tofauti.

Kwa uchache awe na sifa zifatazo:

-Awe ni mtu wa kujituma na sio wa kutumwa.

-Awe na ufahamu na uelewa wa mambo ya ujenzi.

- Awe na uwezo wa kuandika na kutunza records kwa kutumia computer.

- Awe na uwezo wa kusimamia kazi kwa kuzingatia ubora wa bidhaa na nidhamu za kazi.

- Awe na ubunifu na anaependa kujifunza mambo mapya daima.

Malipo yatategemea uwezo na uzalishaji wake (Performance and production based earnings).

Ukiwa unahisi una sifa hizo au ukiwa unahisi ukifundishwa utaweza basi wasiliana kwa Whatsapp na Abdul Ghafur 0625249605. Tafadhali usitume cv.

Sisi tunaitwa Madrassatul Abraar. Maana yake ni madarasa ya Waja Wema. Mobile No. 0625249605. tuna programne yetu inaitwa Abraar Bricks Nyumba kwa wote.

Tupo mtaa wa Vitendo, kata ya Misugusugu, wilaya ya Kibaha,mkoa wa pwani.

Stendi inaitwa Miyomboni Shule au Misugusugu Shule ya msingi.

Wasambazie na wengine.
 
Ofisi zenu ziko wapi?

♻️♻️♻️♻️

Abraar Bricks Nyumba kwa wote

Inakuletea fursa kwenye darasa lake la kiwanda kidogo cha vifaa vya ujenzi.

Kunahitajika wanafunzi wa kuunda na uzalishaji wa vifaa vya ujenzi kwa vitendo (practical).

Kwa kuanzia tutafundishwa kuunda aina 8 mpaka 13 za vifaa vya ujenzi na ataependa kujiendelea atakua na fursa ya kuendelea kujifunza vifaa vingine aina 50 na pia kutakua na fursa ya kujiendeleza zaidi kwa kujifunza ujenzi.

Mafunzo yetu yote ni 95% kwa Vitendo (practical).

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Abdul Ghafur 0625249605.

Tafadhali sambazia na wengine.
 
Jiunge hapo kupata update za nafasi za ajira, Tenda na vibarua Tanzania

Asante.
 
Hii fursa haijajazwa.

Wamekuja candidates watatu kufanya orientation, wote wamemaliza orientation ya wiki mbili vyema kabisa lakini ilipofikia kuanza "probation" wote wameshindwa kuhimili u manager.

Hapa kwetu, tuna mpango wa "orientation", kwa maana ya mtu kupata muelekeo kabla hajaanza "probation" ya kisheria. Kupata muelekeo imelenga anaetafuta ajira aelewe mazingira na namna ya kufanya kazi zenye viwango vya ubora.

Baada ya orientation ya nafasi hii ya u manager wa kiwanda kidogo, wote walijibaini kuwa hawana vigezo stahiki vya kuwa manager. Kwa kujitambua kuwa hawana vigezo na baada ya kuwashauri wawe "apprentice", yaani wanafunzi wa kazi kwa vitendo, kama kawaida ya Watanzania walio wengi, fursa ikawatupa mkono, "wakaingia mitini" kwa visingizio mbali mbali.

Bado fursa ipo wazi kwa wenye uzoefu na kwa kuwa wanafunzi wa hii kazi kwa wataopenda kujifunza na kujiendeleza.

Kazi hii ya u manager wa kiwanda hiki kidogo, ni ngumu sana, kwa kuwa vifaa vinavyoundwa vinatakiwa vizingatie ubora na kuna namna za ku report.

Tunashauri kila atakeihitaji nafasi hii, ajisomee kwa uchache kwenye mitandao kuhusu "concrete blocks factory management). Kiwanda ni kidogo tu kinachoweza kuajiri mpaka watu 100 kwa siku kikifanya kazi kwa uwezo wake kamili.

Kwa maelezo au maswali yoyote kabla haujaja, tuma whatsapp 0625249605. Kama hauwezi kuhimili shinikizo (pressure) za kazi ya manager usijisumbue kuihitaji hii kazi.
 
Abraar Bricks Nyumba kwa wote.

Katika kiwanda chetu cha uzalishaji vifaa vya ujenzi wa kisasa kwa kutumia saruji (precast) tunatafuta msimamizi "manager" wa kiwanda.

Kiwanda kina uwezo wa kuwa na wafanyakazi wa uzalishaji 21 na wasio wazalishaji 3 kwa shift moja. Tunataraji kifikie uwezo wa kufanya kazi shifts tatu kila siku.

Kiwanda kina uwezo wa kuunda bidhaa zaidi ya aina 50 tofauti.

Kwa uchache awe na sifa zifatazo:

-Awe ni mtu wa kujituma na sio wa kutumwa.

-Awe na ufahamu na uelewa wa mambo ya ujenzi.

- Awe na uwezo wa kuandika na kutunza records kwa kutumia computer.

- Awe na uwezo wa kusimamia kazi kwa kuzingatia ubora wa bidhaa na nidhamu za kazi.

- Awe na ubunifu na anaependa kujifunza mambo mapya daima.

Malipo yatategemea uwezo na uzalishaji wake (Performance and production based earnings).

Ukiwa unahisi una sifa hizo au ukiwa unahisi ukifundishwa utaweza basi wasiliana kwa Whatsapp na Abdul Ghafur 0625249605.

Sisi tunaitwa Madrassatul Abraar. Maana yake ni madarasa ya Waja Wema. Mobile No. 0625249605. tuna programne yetu inaitwa Abraar Bricks Nyumba kwa wote.

Tupo mtaa wa Vitendo, kata ya Misugusugu, wilaya ya Kibaha,mkoa wa pwani.

Stendi inaitwa Miyomboni Shule au Misugusugu Shule ya msingi.

Wasambazie na wengine.
Hii nafasi ya kazi bado ipo, walikuja candidates wawili watatu wakidhani ni kazi ya mchezo mchezo, standards na quality ya utendaji wetu zikawashinda walifikiri kuna mteremko wa kitonga uliozoeleka Tanzania

Kama hauna ubora na standards za kazi za Kimataifa (kujituma, kujisimamia na kusimamia wengine) usijisumbue kutaka kazi hii, ni highly demanding.
 
😂😂😂 wakakimbia. Watz tumezoea kazi kishkaji
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom