Nafasi anayocheza Samatta pale Taifa Stars awe anawekwa Kibu Denis

Execute

JF-Expert Member
Sep 21, 2022
3,000
7,285
Japo Kibu hana akili ya mpira lakini anakupatia kitu kinaitwa work rate. Yaani akiwepo uwanjani anakuwa na pilikapilika nyingi ambazo zinaweza kuleta matokeo chanya.

Huyu Samatta ameshapitwa na wakati.. hana chochote anachoiongezea timu awapo uwanjani.. Kibu anaweza kufanya link ya viungo wakabaji na washambuliaji.. kitu ambacho kinakosekana kabisa pale stars.
 
Japo Kibu hana akili ya mpira lakini anakupatia kitu kinaitwa work rate. Yaani akiwepo uwanjani anakuwa na pilikapilika nyingi ambazo zinaweza kuleta matokeo chanya...
Huyo ametukosesha magoli mawili ya wazi Kwa ubinafsi wake wa kutaka kufunga yeye mwenyewe wakati hayupo katika nafasi nzuri
 
Hali ya Taifa Stars baada ya kichapo toka kwa Uganda.

JamiiForums-1387865150.jpg

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Huyo ametukosesha magoli mawili ya wazi Kwa ubinafsi wake wa kutaka kufunga yeye mwenyewe wakati hayupo katika nafasi nzuri
Kwa hiyo unataka kibu acheze namba 9?
Je huko simba huwa mnamchezesha namba 9??

Acha kuongea ushabiki nakuanza kumlaumu mtu kiufupi timu bovu lile mzee hakuna namba kumi mzuri aliyekua analisha mipira

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Baada ya Samatta kutolewa tu ndo tumepigwa, jamaa akiwepo tu uwanjani hata kama hachezi,anasababisha wachezaji watatu wa timu pinzani kumkaba yeye hivyo wachezaji wetu wengine hupata upenyo!

Namuheshimu sana SAMATTA,asivunjike moyo mashabiki wa Tanzania hatujui mpira bali ni makelele tuuu,Kwa hiyo atuvumilie
 
Kwa hiyo unataka kibu acheze namba 9?
Je huko simba huwa mnamchezesha namba 9??

Acha kuongea ushabiki nakuanza kumlaumu mtu kiufupi timu bovu lile mzee hakuna namba kumi mzuri aliyekua analisha mipira

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Tangu game ya kwanza mimi nilikuwa nalia na kukosekana kiungo mchezeshaji kwa sababi viungo waliopo ni viungo wakabji-mudathiri, himid, mzamiru. Pale alitakiwa awepo mtu kama sure boy ili hao kina Samata na Msuva wapate mipira
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom