kisemvule8080
Member
- Dec 23, 2016
- 18
- 12
daah uz mzuri sana ila wa tanzania tunakosa majibu sahihi ya kujibu mahara sahihi, inakuwa ni kutishana kuongopeana na si kutoa fact.Nafarijika sana Ninaposikia kauli ya ahadi ya mh.Rais wetu kuhusu kutoa nafasi za ajira kwa vijana wa kitanzania katika jeshi letu imara (Jwtz) na kutoa kipaumbele kwa vijana ambao wamepitia mafunzo ya jkt.
Ajira hizi ni wazi kuwa japo hazitomaliza lakini kwa kiasi fulani zitapunguza tatizo la ajira katika nchi.
Ninaimani na mchakato wa upatikanaji wa vijana wanaohitajika maana jeshi letu limeundwa na watu wenye nidhamu na moyo wa uzalendo tofauti na baadhi ya taasisi nyingine za serekali ambazo kwa kiasi Fulani bado kuna changamoto ya ukosefu wa uadilifu kwa baadhi ya watendaji wa taasisi hizo ambao mh.Rais na serekali yake makini amekua akipambananao kila siku.
Hivyo naona kuwa hii itakua ni fursa kubwa sana hasa kwa vijana ambao pengine waliwahi kujikatia tamaa ya kupata ajira kutokana na ile imani na mazoea tuliyojijengea miongoni mwetu kuwa hauwezi kupata ajira serekalini kama hauna mtu wa kukushika mkono.
Ombi kwa wahusika
Kuna vijana wengi na wazalendo kwa nchi yetu pendwa Tanzania, ambao wapo tayari na wanatamani kulitumikia taifa letu kupita Jwtz na walipitia mafunzo ya JKT KWA MUJIBU WA SHERIA na sasa wamemaliza vyuo na wapo tu mtaani.
Ninaimani Serekali yetu ni sikivu na masikio yake yapo kila mahali ivo huwenda wazo hili ambalo ni tumaini la vijana waliowengi waliopitia jkt kwa mujibu wa sheria likiwapendeza wahusika basi vijana hawa watapata nafasi ya kulitumikia taifa letu.
Sio Jwtz tu hata majeshi mengine kama magereza,polisi,migration na mengine amabayo sijayataja kuna vijana ambao wamepitia jkt kwa mujibu wa sheria wapo tayari kupiga kazi kwani askari na mzalendo wa kweli hachagui kazi bali anafata amri na kutekeleza majukumu.
Hayo ndio mawazo yangu Mimi kutokana na upeo wangu nilionao.Naamini hatulingani katika upeo na namna ya kupambanua mambo, kama kuna mwenye wazo,ushauri,marekebisho nipo tayari kupokea.
PIA : kwa yeyote mwenye updates zozote kuhusiana na ajira hizi 3000 au nyingine za majeshi kama polisi,magereza,TANAPA na migration tunaweza kupeana updates kupitia Uzi huu. Lugha ya MATUSI sio mahala pake.
Asanteni.