Nafasi 3000 za JWTZ na waliopita JKT kwa Mujibu wa sheria.

Wakisema mtu aliyepita JKT wanamaanisha Yale mafunzo ya Kujitolea Mdogo wangu.
Ndo nashangaa huyu anadhani wanaonhelewa wale wa mujibu wa sheria(miez mi3) ambao hata namba nadhani hawana.

JKT kwa kujitolea wapo vijana kibao kambini,mtaani kwenye makampuni ya ulinzi nk. Ambao hawa kozi yao ni ndefu na deep zaidi kuliko wale Form six leavers wanaoenda kwa lazima
 
Ndo nashangaa huyu anadhani wanaonhelewa wale wa mujibu wa sheria(miez mi3) ambao hata namba nadhani hawana.

JKT kwa kujitolea wapo vijana kibao kambini,mtaani kwenye makampuni ya ulinzi nk. Ambao hawa kozi yao ni ndefu na deep zaidi kuliko wale Form six leavers wanaoenda kwa lazima
Hiyo ni opinion yako au ndio agizo la rais?
 
Kuna mbunge qliwahi kusema eti jeshi sio ajira , Ila huyo mbunge baba take nae no mbunge ... Embu bahatisha kumtambua
 
TATIZO WATU HAWATAKI KUELEWA. .YAAN KWA USAWA HUU KUTOKA KITAA KWENDA JW NI NGUMU. .LABDA ITOKEE WATAFUTE WATU MAALUMU WA PROFESSIONAL FULANI NDO WANAWEZA CHUKUA MTAAN NA HASA KAMA UMEPITA HYO YA MUJIBU. .AU KAMA UNA CHANNEL INAYOELEWEKA HUKO MAJUU. .LA SIVYO PAMBANA KITAA UTATOKA TUU. .HYO YA KUSUBIRIA LABDA WATAKUJA KUFANYA USAILI KITAA HYO KWA %KUBWA TUSAHAU. .HUKO MAKAMBINI KUNA WA KUJITOLEA JKT WENGINE MWAKA WA NNE HUU WAKIJITOLEA. .AFU WAKUCHUKUE KITAA KIZEMBE ZEMBE TU..JESHI LA WAPI HILO? ?
 
Nikisikia ajira za JWTZ,moyo hunienda mbio,nakumbuka,miaka kadhaa nyuma,zilotoka nafasi 72,kwa mkoa wa Dar,kila wilaya watu 24,kwenye usahili pale wilayani kinondoni,kupitia kwa jamaa yangu,was karibu,alinipereka moja kwa moja,kwa maofisa waliokuwa wanaofanya usahili,kipindi hicho nirikuwa mwili jumba,Gym sana,yule officer,akaniangaliaaa,then akaniambia,kijana sifa unazo,lakini hapo nje mpo zaidi ya 200,majina yakifika hapa,wanaangalia,huyu mtoto wa Mani,anapitishwa,he wewe una jamaa ngazi za juu,?nikaishiwa nguvu kabisa,
Mara ya pili nirienda pale Mlalakuwa JKT,nikauliza nafasi vipi,maana zilitangazwa,nirichoambulia nikuulizwa jina langu LA ubini,na kupigwa tarehe,
Nikarudi kitaa kujipanga upya,nikaamua kurudi Shule,kutafuta shahada,ni miaka kadhaa sasa,nipo sekta binafsi napiga kazi,kwa wadogo zangu ni rahisi kuingia jeshini,ukitokea mikoani,kuliko kwenye majiji makubwa kama dar,arusha,mwanza,
 
Alisema anataka jeshi liwe na wataalam...unauhakika waliopo jkt saizi wanatosheleza idadi ya watu 3000 wenye professional?Na alisema kipaumbele kitakua kwa ambao wamepitia mafunzo ya jkt lakini hakusema kama kwa kujitolea au kwa mujibu wa sheria.Acha kupotosha watu.
Wewe hujitambui, hebu sikiliza audio au tazama video fupi utasikia akisema hao elfu tatu ni maofisa au maaskari. Kasema hao 3,000 ni junior officers na askari. Alisema hatuwezi kuwa na maafisa tupu katika jeshi na ndipo akaangushia kwenye suala la ajira 3,000.
Hutaki maelezo yangu kaa na kaa uzisubiri hizi ajira utashtuka bajeti ya 2018/19 ikisomwa na still uko home.
Pia usijidanganye kuwa jkt wa kujitolea wote ni lasaba na form four, wengi wana vyeti vyao vizuri.
Ungekuwa umepitia mujibu operetion Miaka 50 ya JKT awamu ya kwanza ungeamini hili. Wenye barchelors ,diploma na astashahada wengi tulipiga nao kozi. Mimi nilipiga mujibu RUVU 2013 ambapo miezi miwili na nusu ya kwanza tulianza na wakujitolea na kisha kutenganishwa.
 
Hilo la mujibu ni la kwako. Ujue wengi wamejitolea na degree zao. Wa mujibu ni maform six.
 
Nafarijika sana Ninaposikia kauli ya ahadi ya mh.Rais wetu kuhusu kutoa nafasi za ajira kwa vijana wa kitanzania katika jeshi letu imara (Jwtz) na kutoa kipaumbele kwa vijana ambao wamepitia mafunzo ya jkt.

Ajira hizi ni wazi kuwa japo hazitomaliza lakini kwa kiasi fulani zitapunguza tatizo la ajira katika nchi.

Ninaimani na mchakato wa upatikanaji wa vijana wanaohitajika maana jeshi letu limeundwa na watu wenye nidhamu na moyo wa uzalendo tofauti na baadhi ya taasisi nyingine za serekali ambazo kwa kiasi Fulani bado kuna changamoto ya ukosefu wa uadilifu kwa baadhi ya watendaji wa taasisi hizo ambao mh.Rais na serekali yake makini amekua akipambananao kila siku.

Hivyo naona kuwa hii itakua ni fursa kubwa sana hasa kwa vijana ambao pengine waliwahi kujikatia tamaa ya kupata ajira kutokana na ile imani na mazoea tuliyojijengea miongoni mwetu kuwa hauwezi kupata ajira serekalini kama hauna mtu wa kukushika mkono.

Ombi kwa wahusika

Kuna vijana wengi na wazalendo kwa nchi yetu pendwa Tanzania, ambao wapo tayari na wanatamani kulitumikia taifa letu kupita Jwtz na walipitia mafunzo ya JKT KWA MUJIBU WA SHERIA na sasa wamemaliza vyuo na wapo tu mtaani.

Ninaimani Serekali yetu ni sikivu na masikio yake yapo kila mahali ivo huwenda wazo hili ambalo ni tumaini la vijana waliowengi waliopitia jkt kwa mujibu wa sheria likiwapendeza wahusika basi vijana hawa watapata nafasi ya kulitumikia taifa letu.

Sio Jwtz tu hata majeshi mengine kama magereza,polisi,migration na mengine amabayo sijayataja kuna vijana ambao wamepitia jkt kwa mujibu wa sheria wapo tayari kupiga kazi kwani askari na mzalendo wa kweli hachagui kazi bali anafata amri na kutekeleza majukumu.

Hayo ndio mawazo yangu Mimi kutokana na upeo wangu nilionao.Naamini hatulingani katika upeo na namna ya kupambanua mambo, kama kuna mwenye wazo,ushauri,marekebisho nipo tayari kupokea.

PIA : kwa yeyote mwenye updates zozote kuhusiana na ajira hizi 3000 au nyingine za majeshi kama polisi,magereza,TANAPA na migration tunaweza kupeana updates kupitia Uzi huu. Lugha ya MATUSI sio mahala pake.

Asanteni.





Itasaidia kiasi flani.
 
Vijana wenzangu wa bongo sometimes nawahurumia sana. Uwezo wao wa kuchuja mambo ni mdogo. TPDF wana mfumo wao rasmi wa kuajiri ambao uko wazi.
Huchukua vijana waliomo makambini(JKT) na kuwapa mafunzo mafupi ya miezi mitatu au minne kisha kuwa askari. Na kwa maofisa mfumo uko wazi pia.
Hivi leo wahangaike kutafuta vijana mtaani ilhali wanaohitajika ni 3000 na waliomo makambini ni zaidi ya elfu tano.How!
Kuna intakes ngapi wamemaliza mafunzo mpaka sasa?
Nafasi kwaajili ya mujibu wa sheria zinatolewa wakimaliza kozi tu .
Sisi huku tunamaliza kozi 2013 kwa mujibu tulioomba kuendelea na TPDF walitupigia simu hasa waliosoma sayansi na hata maartists walipiga usaili. Waliotaka walikwenda kufanya usaili wengine walikuwa washamba wa chuo kikuu huku wakidanganyana tutakwenda tukimaliza degree.
Kama ulipita mujibu wa sheria na ukarudi nyumbani na kama hukusomea udaktari, uhandisi au urubani sahau kuhusu JWTZ labda itokee vita.
JKT ina watu wa kila kada wamemaliza kozi wanasubiri fursa na wengine mkataba wa miaka miwili washamaliza wameongezewa mkataba. Itakuwa ajabu leo wasake vijana mtaani kwa gharama kubwa huku makambini wako wengi. Alichotaja jana Magufuli ni idadi tu yaani kama kibali ambacho kila mwaka hutolewa na si kwamba kutaja hadharani ndio mfumo wa uandikishaji utabadilika.
sorry kiongoz ivi kwa udaktari hata wa technician certificate & diploma wanapokelewa?
 
Ile miezi mitatu ya kuweka chenja nayo unajiita umepita JKT?

National Service Compulsory Program ilianzishwa kisiasa na ndio maana hata mtaala wa mujibu haufanani na wa kujitolea (except pilot intake ya 2013 ya wanafunzi 5000 ambao mujibu na wa kujitolea walichanganywa)

Hivyo basi,wanapozungumzia vijana waliopita JKT ,hawawazungumzii nyie maselule wa miezi mitatu
 
Ile miezi mitatu ya kuweka chenja nayo unajiita umepita JKT?

National Service Compulsory Program ilianzishwa kisiasa na ndio maana hata mtaala wa mujibu haufanani na wa kujitolea (except pilot intake ya 2013 ya wanafunzi 5000 ambao mujibu na wa kujitolea walichanganywa)

Hivyo basi,wanapozungumzia vijana waliopita JKT ,hawawazungumzii nyie maselule wa miezi mitatu
 
Ile miezi mitatu ya kuweka chenja nayo unajiita umepita JKT?

National Service Compulsory Program ilianzishwa kisiasa na ndio maana hata mtaala wa mujibu haufanani na wa kujitolea (except pilot intake ya 2013 ya wanafunzi 5000 ambao mujibu na wa kujitolea walichanganywa)

Hivyo basi,wanapozungumzia vijana waliopita JKT ,hawawazungumzii nyie maselule wa miezi mitatu
Mkuu mie sijipigii debe,mie nilipita jeshini mwaka 2001 pale Mafinga kwa Meja Stephano aka Mlaiberia,kisha nikalitema jeshi 2004 na mshahara wangu wa mwisho ulikua 128,000. now nimejiajiri na ata sipo huko TZ so kuwa na Amani tu mkuu!
 
Back
Top Bottom