Naepuka vipi magamba mikononi baada ya kutumia sabuni ya Unga?

Loweka sabuni inayotosha kwenye chombo e. g jagi kwa dak. 30-saa1 reference Mathabane. Wakati wa kufua mimina kiasi kwenye maji nakufua nguo zaps kama una tatizo kama la mleta mada.
Nyoosha kiswahili chako, wewe pia unatatizo la kiswahili unahitaji msaada.
 
Basi safi.mana kuna mtu wangu mmoja kaajiriwa sehemu kwa kazi hiyo akaniambia kwamba hizi mashine ni kwa nguo za kutoa jasho na sio zile zilizochafuka sanaa
.inakuwa ngumu mashine kupoint sehemu moja yenye uchafu na kufanya friction.sijui pana ukweli gani hapo
Hata mimi niliwahi kusikia hivyo kua kwenye makwapa na kola mashine haifui vizuri. Kua eti inafaa kufulia mashuka na mataulo but nguo zenye kona au mikunjo eti hazitakati, wajuzi watujuze
 
Unajua mkuu sio kama naleta ujuwaje hapana.
Kiukweli kabisa suala la kufua sikuwahi kufundishwa poppte kuna wadau wanasema ni sayansi kimu,lakini mimi sikumbuki kama nafua kupitia mafundisho ya darasani.

Staili yangu ya kufua nafua nguo mbili mbili tu.zikiisha naenda kuchukua zingine.hayo ndo maisha yangu.na hapo mpaka ziwe chafu nyingii ndo nafua.

Sasa nikisema niloweke nguo 20 kwa pamoja lwa kweli siwezi naona kama ntajifunga kifungo nifue zote.

Ufuaji wangu nafua tatu naanika nachukua zingine,nikichoka naacha kufua mpaka siku ingine.hapo nikisema niloweke mbili mbili kwa ufuaji wangu kweli itani kosti kwa namna fulani muda.

Lakini kama kwa ufuaji wenu inakuwa bora kufanya hivyo.
Usiwe mbishi una tatizo unashauriwa unaleta ujuwaji. Jaribu ushauri unaopewa uone.

Nguo utengwa kabla ya kufuliwa. Za rangi, nyeupe etc. Nguo kwa pamoja hulowekwa kimakundi na kifuliwa. Rejea somo la sayansi kimu shule ya msingi.
 
Unajua mkuu sio kama naleta ujuwaje hapana.
Kiukweli kabisa suala la kufua sikuwahi kufundishwa poppte kuna wadau wanasema ni sayansi kimu,lakini mimi sikumbuki kama nafua kupitia mafundisho ya
Lakini kama kwa ufuaji wenu inakuwa bora kufanya hivyo.
Mkuu, hii staili yako yakufua ndiyo inasababisha magamba (blisters) kwenye mikono.

Wadau walivyokuelekeza wako sahihi kabisa. Kwenye instructions juu ya mfuko wa Ariel, wameelekeza kwenye kufua na mikono:
1. Sort - Tenganisha nguo nyeupe na za rangi
2. Dose and Soak - Mwaga sabuni kwenye basin ya maji na lowesha nguo. Unapolowesha nguo ndiyo sabuni inapata fursa ya kushughulikia uchafu na madoa. Hata kwenye mashine ya kufulia pia kuna cycles, na mzunguko wa kulowesha ndio ndefu kabisa na sabuni inashughulikia mpaka sehemu za collar na mkwapa zinakuwa safi.
3. Wash - Fua

Ujue kwamba sabuni za kisasa zimewekewa makemikali na enzymes za kuondoa uchafu na madoa. Unapolewesha ndipo hizo kemikali zinayayuka kwenye maji na kushambulia uchafu. Ukifua bila kulowesha, kemikali ambayo hazijayayuka yanashambulia ngozi na kusababisha magamba.
 
Unajua mkuu sio kama naleta ujuwaje hapana.
Kiukweli kabisa suala la kufua sikuwahi kufundishwa poppte kuna wadau wanasema ni sayansi kimu,lakini mimi sikumbuki kama nafua kupitia mafundisho ya darasani.
Staili yangu ya kufua nafua nguo mbili mbili tu.zikiisha naenda kuchukua zingine.hayo ndo maisha yangu.na hapo mpaka ziwe chafu nyingii ndo nafua.
Sasa nikisema niloweke nguo 20 kwa pamoja lwa kweli siwezi naona kama ntajifunga kifungo nifue zote.
Ufuaji wangu nafua tatu naanika nachukua zingine,nikichoka naacha kufua mpaka siku ingine.hapo nikisema niloweke mbili mbili kwa ufuaji wangu kweli itani kosti kwa namna fulani muda.
Lakini kama kwa ufuaji wenu inakuwa bora kufanya hivyo.
Sabuni bora za unga zinamaelekezo kwa mfuaji, jaribu kufuata maelekezo hayo.
 
Mkuu, hii staili yako yakufua ndiyo inasababisha magamba (blisters) kwenye mikono.

Wadau walivyokuelekeza wako sahihi kabisa. Kwenye instructions juu ya mfuko wa Ariel, wameelekeza kwenye kufua na mikono:
1. Sort - Tenganisha nguo nyeupe na za rangi
2. Dose and Soak - Mwaga sabuni kwenye basin ya maji na lowesha nguo. Unapolowesha nguo ndiyo sabuni inapata fursa ya kushughulikia uchafu na madoa. Hata kwenye mashine ya kufulia pia kuna cycles, na mzunguko wa kulowesha ndio ndefu kabisa na sabuni inashughulikia mpaka sehemu za collar na mkwapa zinakuwa safi.
3. Wash - Fua

Ujue kwamba sabuni za kisasa zimewekewa makemikali na enzymes za kuondoa uchafu na madoa. Unapolewesha ndipo hizo kemikali zinayayuka kwenye maji na kushambulia uchafu. Ukifua bila kulowesha, kemikali ambayo hazijayayuka yanashambulia ngozi na kusababisha magamba.
Pamoja sana mkuu imesomeka vizuri kabisa
 
Daaha mie sabuni za unga karibia zote huwa zinanisumbua. Clean soft na sabuni fulani hivi kutoka Zanzibar ndio hazinisumbui.
 
Hyo sabuni fulani kutoka zanzibar ni ipi mkuu jina lake..?
 
Kabla ya kufulia sabuni ya unga iloweke kwenye maji muda wa chini sana iwe japo nusu saa.

Ukiweka kwenye maji nq kufulia hapohapo lazima mikono iungue. Haijalishi ni omo ama nini.

Jaribu kufanya hivyo afu lete mrejesho.
Nafikiri inategemea mtu na mtu, mie hata niloweke kwa masaa 10 bado omo,ariel,foma,sunlight zitanichubua tu.
 
Back
Top Bottom