Nadharia 4 kuhusu kisa cha Mdude na dawa za kulevya

Nadharia 4 kuhusu kisa cha Mdude na dawa za kulevya

Kwa taarifa za siri nilizonazo, baada ya biashara ya madawa kuota nyasi Dares salaam baada mkuu wa mkoa kuwataja hadharani ,wakuu wa ufipa waliweka kikao na kuamua kuhamishia biashara yao nyanda za juu kusini na wakamteua rasmi Mdude kuwa agent wao.!

Angalia baada ya Mdude kukamatwa ,mwenyekiti akapanic balaa na kuamua kuita waandishi wa habari ili kutengeneza mazingira ya kwamba Chadema wanaonewa kwa kubambikwa kesi.



Sent using Jamii Forums mobile app
Angalia ulichoandika na kumbuka huyo Mdude yupo ndani na nibinadamu. Kama kweli unataharifa kama ulivyosema basi Mungu akubariki. Na kama umeamua kufurahia mateso ya mwanadamu mwenzako pia Mungu akubariki wewe na familia yako.

Ikumbuke siku ya Leo usije ukaisahau, kwani haitojirudia
 
Hii ndio kazi tiss yetu wanaiweza, kupambana na upinzani, ila wafanye wafanyavyo lazima mtalipa tu, that Son of Adam hataacha hivi hivi, na hii ni must.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DAAH MKUU TUNAPOELEKEA HII NCHI KUNA SIKU KITAWAKA,HASA AKIPATIKANA TENA RAISI AINA YA MKULU BAADA YA MKULU KUMALIZA MUDA WAKE
Jitihada zozote zitakazofanyika kujaribu kusimika utawala ujao kwa lengo la kuendeleza ushenzi unaofanyika sasa most likely utakutana na overwhelming resistance.

Kuna watu wamegoma kusafiri, lakini wataiaga hii dunia wakiwa wamejificha nje ya nchi.
 
Utawala wowote ambao hauna mission and vision huwa kazi yake kubwa ni kuhangaika na raia wake.
 
Na mimi nakujibu kwa Nadharia!!

Nadharia yako 2:
Kutokutumia bidhaa haimaanishi huwezi kuuza bidhaa hiyo. Morocco ni wauzaji wakubwa wa mvinyo pombe lakini hawanywi. Mdude kinadharia alikuwa anauza kama wauza wengine.

Nadharia yako 3
kinadharia waliomkamata walitumia muda mwingi kabla ya kumpeleka mahakamani lengo wahakikishe wanajua mtandao ambao alikuwa anatengeneza wa 'hiyo biashara haramu '.Kazi hiyo kinadharia haiwezi kufanywa siku moja ama masaa michache.

Nadharia yako 4:
Kinadharia unatuaminisha kuwa 'kisiki2014' ambaye alitoa taarifa naye anahusika katika mchezo huu! Kwamba kinadharia ndiye alimuandalia honeytrap na kumuunganisha kwa madrugs lords!?

=====
Acheni vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vifanye kazi yake kwa usahihi. Acha kuvuruga uchunguzi kwa makusudi mleta mada.
Toka mwanzoni mwa miaka ya 2000 mpaka leo, hili ndio tukio la polisi kukamata mtu kwa kujihusisha na madawa ya kulevya baada ya kukutwa na kiwango kidogo sana cha madawa husika.

Pia, ndio tukio linahusika na kumkamata mtu akiwa na madawa ya kulevya bila kukamata wahusika weka wenza.
 
Ukakasi ni huu kwa nini ukae na watuhumiwa siku 7 wakati umemshika redi hendedi kama Rais wetu anavyosema kila siku?

Yaani siku saba umekaa na muharifu wakati umemkamata na kete, siku 7 kweli
 
Huu ujuaji wenu ndiyo unawaponza kila siku haya tuambie wewe hapo alikuwa anamsema nani na huyo nani anahusika vipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
You can not point a confirmatory finger to anybody! Utahisi, lkn huwezi kuwa na irresistible inference kuwa anamsema fulani. Ndiyo maana wametafuta kumpachika madawa. Wangeliweza kupeleka tweet ile mahakamani, wanajua kuwa kuna mapungufu...
 
Lakini pia utawala wa awamu ya tano unapoanza kutolewa mifano ya namna watu kama pinochet waliongoza serikali zao kwa kweli inabidi ujitafakari, hasa magufuri inabidi ajitafakari sana, maneno yanaumba na lisemwalo lipo.
hapa ndio napata mashaka kama ataondoka madarakani hata 2025,ni ama alazimishe kubaki au ampe mtu kituko zaidi yake kumlinda. usidhani kama kina Mugabe walipenda kufia madarakani.hofu ilikuwa wakitoka itakuwaje
 
hapa ndio napata mashaka kama ataondoka madarakani hata 2025,ni ama alazimishe kubaki au ampe mtu kituko zaidi yake kumlinda. usidhani kama kina Mugabe walipenda kufia madarakani.hofu ilikuwa wakitoka itakuwaje
Watawala wa CCM hawajawahi fanikiwa kuweka mapandikizi yao wakati wanaondoka.only Nyerere have had such legitimacy.
 
Hizi nguvu mnazotumiaga kumnasua kwenye matokeo anayopata kwa nini msingezitumia kumshauri pindi awapo uraiani aishi kama RAIA mwema? Au ndo unafiki wenyewe huu! Hiyo njia kachagua mwenyewe maana yanaepukika hayo na anajua kabisa alishanusurika huko nyuma so mrelax kabisa.
Kwa tweets za Mdude angeshitakiwa kwa kosa la uchochezi isingekuwa na taharuki kubwa kwa jamii.
Mungu katuweza wanadamu kutuweka kundi moja na wanyama (mammalia) maana hata mahitaji ya jumla ya Nafsi zetu hatuyajui, tunapelekeshwa tu, anae tupelekesha nae hajui anatupeleka wapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wiki jana ndugu Mpaluka Saidi Nyagali maarufu kama ‘Mdude Chadema’ alikamatwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya bila kuwekwa wazi sababu za kukamatwa kwake. Hakupandishwa mahakamani kwa karibu juma zima, na baada ya shinikizo kutoka sehemu mbalimbali polisi wamempeleka mahakamani na kumshtaki kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine zenye uzani wa gramu 23.4.

Baadae kidogo zikaibuka taarifa mitandaoni kuwa Mdude aliwekewa mtego wa dawa za kulevya na binti aliyekutana nae mtandaoni, wakaanzisha mahusiano na akamtumia kiasi fulani cha fedha.

Kwa sasa mjadala mkubwa si Mdude kudaiwa kukamatwa na dawa za kulevya bali kile kinachoitwa mtego uliotumika kumnasa, yani binti aliyeanzisha nae urafiki. Inawezekana madai haya yakawa kweli au yasiwe kweli. Nitatoa nadharia nne kuhusu kwanini yanaweza yasiwe kweli.

#Mosi; Kwa sisi tunaomfahamu Mdude (watu wake wa karibu) hatujawahi kumuona huyo binti wala kusikia habari zake kutoka kwa Mdude mwenyewe au ndugu zake. Si nyumbani kwa Mdude, kazini kwake au kwenye vijiwe vyetu vya siasa ambapo Mdude amewahi kumzungumzia kwa kudhamiria au kwa bahati mbaya.

Kwahiyo kama walikuwa na mahusiano basi yalikuwa ya SIRI sana na kukutana nao kulikuwa kwa nadra na kwa kificho sana. Lakini kadri nimjuavyo Mdude si rahisi kuanzisha mahusiano na mtu aliyekutana nae mtandaoni kirahisi. Mdude anajua yeye ni ‘target’ ya serikali kwa muda mrefu, kwahiyo hawezi kuingia mtegoni kirahisi hivyo.

#Pili; Mdude si mtuaji wa pombe wala sigara achilia mbali dawa za kulevya. Jamhuri inaweza kumpima ili kuthibitisha hili. Hanywi hata ‘Serengeti lite’. Mdude ni mwanaharakati ‘sobber’ kuliko wengi wetu tunaofanya harakati. Lakini akishika ‘mic’ sisi ndo hujiona ‘sobber’ kwa jinsi anavyoshusha nondo nzito. Sasa jiulize kama hanywi pombe au havuti sigara, hizo kete za ‘heroine’ alikuwa anazifanyia nini? Kupiga nazo picha aweke instagram?

#Tatu; Kwanini polisi imetumia siku 7 kumkamata hadi kumfikisha mahakamani kama kweli alikutwa na kete za heroine? It could be just simple baaada ya kumkamata wangemfikisha mahakamani kesho yake maana ushahidi wanao. Lakini kumkamata mtu bila kumwambia kosa lake, na kukaa nae siku 7 bila kumpeleka mahakamani inaleta ukakasi. Na hata baada ya siku 7 bado mnasita kumpeleka mahakamani hadi mpate shinikizo kutoka kwa jamii?

Je mtu akisema mlimkamata bila kosa, na mlikaa nae siku zote hizo mkijipanga mumpe kosa gani atakuwa anakosea? Scenario za polisi kubambikia watu kesi zipo nyingi sana. Waziri Mkuu Kassim majaliwa aliwahi kueleza kisa cha mfanyabiashara mmoja aliyekataa kutoa rushwa kwa polisi wakambambikiza kesi ya kukutwa na mali za magendo. Bahati nzuri Rais JPM aliingilia kati na kuagiza polisi na maafisa wa TRA waliohusika wafukuzwe kazi na kushtakiwa. Pia aliagiza ofisi ya TRA Ilala imfidie mfanyabiashara huyo.

Si hivyo tu, wakati wa JK wafanyabiashara watatu wa madini ambao ni ndugu kutokea Mahenge mkoani Morogoro waliwahi kukamatwa na kunyang’anywa fedha (milioni 200) na madini waliyokuwa nayo kisha wakauawa na kupakaziwa ujambazi. Tume ya Jaji Kipenka ilibaini baadae kuwa watu hao hawakuwa majambazi.

Visa vya polisi kubambikizia raia kesi ni vingi sana. Hata katika mazingira ya kawaida unaweza kuzozana na askari ukakamatwa na kuwekwa mahabusu lakini kesho yake ukashangaa umepewa kesi ya kukutwa na bangi. Na usipohangaika utapandishwa kizimbani na wataletwa mashahidi "waliokukuta" na bangi, na unaweza kuhukumiwa kifungo, wakati kiuhalisia hujawahi kuiona bangi zaidi ya kwenye TV. Je haiwezi kuwa hivi kwa Mdude pia?

#Nne; Kuna uwezekano waliomkamata Mdude ndio haohao waliotoa taarifa kuwa amewekwa mtegoni na mwanadada ili kuhalalisha mashtaka dhidi yake. Michael Barkun wakati akielezea ‘Conspirancy theory’ alielezea dhana inayoitwa ‘Finite insight’ kwenye Event Conspirancy theory. Kwa kifupi dhana hii inahusisha kula njama za kubuni uongo na kuuvumisha ili uongo huo usaidie kuhalalisha uhalifu mlioufanya. Waswahili husema kujamba na kuwasha feni.

Bado hujanielewa? Ngoja nikupe mfano. Mwaka 1980 Rais Augusto Pinochet wa Chile alimuua mkosoaji wake mmoja Julio Parot baada ya kuilaumu serikali kukiuka haki za binadamu. Parot alidai utawala wa Pinochet hadi mwaka 1980 ulikua umeua zaidi ya watu 200,000 kwa njia mbalimbali, ikiwemo kipigo kikali, shoti ya umeme, kutupwa kwenye bwawa la mamba, kuburuzwa barabarani, kukatwa kiungo kimoja kimoja na njia nyingine za kikatili.

Parot alikamatwa na majasusi wa shirika la ujasusi la nchi hiyo National Intelligence Directorate (DINA) wakati huo likiongozwa na Manuel Contreras. Wakati akihojiwa akapewa mateso makali sana na kufariki dunia. Kwa siku mbili alizokuwa haonekani serikali haikusema kama inamshikilia. Kwahiyo alipokufa mikononi mwa vyombo vya dola ikawa mtihani mgumu.

Kwahiyo wakaipiga maiti yake risasi moja kwenye paji la uso, na kuichoma visu kadhaa tumboni kisha wakaibeba usiku wa manane hadi kwenye mtaa wa Pedro de Valdivia karibu na mto Mapocho na kuitelekeza hapo. Asubuhi polisi wakatoa taarifa kuwa wameokota maiti ya mwanaume mmoja anayesadikiwa kuwa amevamiwa na majambazi na kuuawa. Ikabainika ni Julio Parot.

Polisi ikaagiza msako mkali dhidi ya washukiwa wa uhalifu huo. Hatimaye ‘majambazi feki’ watatu wakakamatwa. Wakapandishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kusababisha mauaji ya Parot. Wakapatikana na hatia na kuhukumiwa kifo. Jamii na familia ya Parot ikaamini haki imetendeka.

Lakini jambo ambalo hawakujua ni kwamba serikali ya Pinochet ndiyo iliyomuua ndugu yao. Na majambazi walioletwa mahakamani walikuwa ni maafisa wa DINA. Na baada ya kuhukumiwa kifo ilitangazwa kuwa wamenyongwa lakini ukweli ni kuwa waliachiwa na kupangiwa kazi zingine nje ya nchi. Miaka 10 baada ya Pinochet kufurushwa madarakani, CIA ndio wakaujua ukweli huu.

Nimeeleza kisa hiki ili uelewe vizuri maana ya ‘Finite insight' tunapozungumzia 'Event conspirancy theory’. Unapokuwa huna taarifa za kutosha kuhusu jambo fulani wahalifu wanaweza kula njama za kubuni uongo na kuuvumisha ili uongo huo usaidie kuhalalisha uhalifu waliofanya.

Kwahiyo inawezekana taarifa ya Mdude kuingizwa mtegoni na mwanadada mrembo mwenye hela ni hadithi ya kubuni iliyolenga kuhalalisha mashataka dhidi yake kuhusu madawa ya kulevya. Na kwa kiasi fulani wamefanikiwa kwa sababu hata ukisoma mitandaoni ni kama vile watu wameshaamini kwamba Mdude alikutwa na dawa za kulevya.

Hakuna anayejaribu kuwaza kwamba mashatka ya Mdude yanaweza kuwa ya kubambikiziwa. Wengi wanawaza aliingiaje mtegoni kwa huyo dada?

Kwahiyo inawezekana waliomkamata Mdude ndio waliobuni na kusambaza 'hadithi' ya Mdude kuwekwa mtegoni na mwanadada ili madai yao ya kumkamata na dawa za kulevya yapate uhalali (Event conspirancy theory).

Sijui
.
tumeelewana?
.......
Malisa GJ

Sent using Jamii Forums mobile app

Umekuja na hoja dhaifu sana, hoja ambazo ni nadharia za kitoto, hoja kwmba mnamjua hanywi pombe hata sigara havuti sio hoja ya kutuambia wa2 wazma....huenda hayo madawa ilikua kwa ajili ya kuuza na kujipatia fedha.
 
Nimesoma na kukubaliana kabisa na maelezo yako kiukweli haiingii akilini Mdude Chadema aingie king kijinga namna ile huku akijua fika serikali inamuwinda usiku na mchana uko sahihi kwa asilimia Mia

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa mini isiwezekane ? Kila kiti kina tarehe moja ya kuanza

Tabia mbaya INA Siku yake ya kuanza,roho mbaya pia usije Sema ohhh Mimi yule namjua hana Tabia mbaya uongo binadamu aweza chenji any time

Kuhusu kukaa Siku saba ndio afikishwe mahskamani mbona ni siku chache hizo watu wanakaa miexi wakisubiri upelelezi kukamilika sembuse siku saba!!!

Kuhusu mahusiano na mwanamke hiyo.ni mbo yake mdude utayajuaje wakati hulali naye chumba kimoja au kitanda kimoja ni yake binafsi kwani mdude ni padri Wa kikatoliki? Mleta mada umeenda maeneo too personall dari ndizo zinajua kilichokuwa kikiendelea kwenye kitanda cha mdude iwe usiku au mchana jina lake lenyewe anaitwa MDUDE pana usalama hapo? Chezea MDUDE
 
Vijana nawasihi sana tafuteni Pesa mengine yatakuj baada ya kuwa na pesa, huu ujinga wa kulopoka unaweza ukaishia pabaya

Meno ya mtoto mchanga ayawezi kula ugali Ila akingangania mpe. Wako wp aliokuwa anawapigia ameonekana fala na hao wanamcheka na kumdhihaki.

Pole kwake na maisha yaendelee.
 
Mfanyabiashara wa fedha za kigeni nchini Burundi alitekwa siku mbili zilizopita na maiti yake kuokotwa jana kwenye viunga vya jiji la Bujumbura

Serikali ya nchi hiyo inasema vipimo vinaonesha kafa kwa Corona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom