Nadharia 4 kuhusu kisa cha Mdude na dawa za kulevya

Nadharia 4 kuhusu kisa cha Mdude na dawa za kulevya

Ameyataka mwenywe! Angefunga zipu labda angepona. Kwa sasa Miujiza itokee. Yeye siyo wa kwanza duniani kuwa false accused! Let him enjoy the prison, akaonyeshe ubabe huko.
Wewe ni wale wale na hujasoma, umekomenti tu fasta kama balo la kwanza.

Umeambiwa hiyo ni "conspirancy na kesi ya kutengeneza na hata Pinnochet wa Chile aliua mpinzani wake mkuu ikatengenezwa story kama hiyo" ila baadae CIA wakaja kugundua, kama ambavyo KIFO CHA AZORY, ALPHONCE MAWAZO , SAA-NANE VITAGUNDULIKA na CIA, na watu watahukumiwa tu hata kama watakuwa wamestaafu na wamezeeka vipi!
 
Thus tunataka mifumo ya uendeshaji nchi ifumuliwe isuke upya inayotoa haki na kuleta heshima Kati ya watawaliwa na watawala.
Proof anayomuhusika mwenyewe
A cause infused

Similarly, the preponderance of legal opinion at the time was that Augusto Pinochet's immunity shielded him for life from prosecution in the domestic courts of other countries for acts carried out as part of his official duties. Most international lawyers were agreed: after the shock of the arrest and the formality of a court hearing, Pinochet would be freed and sent home within a matter of weeks.

These limited expectations were completely justified at the time. True, the legal principle was established at the Nuremberg trials after 1945 that there should be no immunity for perpetrators of the most egregious abuses of human rights; this was enshrined too by the UN general assembly, and international agreements protecting human rights. But few states have the courage to render these principles a reality, and the victims of torture and crimes against humanity have usually been unable to bring their tormentors to justice. The Realpolitik character of much foreign policy, and the legal notions of "sovereign immunity" and "amnesties", made a mockery of the new law-based international order created after the second world war.

The Pinochet case, and the universal jurisdiction that sustained it, turned the world upside down. It challenged the idea that important folk should be deemed "more equal than others" before the law. In effect, the House of Lords vindicated the principle that executive power and sovereignty are subject to the limits imposed by the rule of law.

The decisions of the courts in Spain and Britain injected a new energy to the struggle to address massive violations of human rights. In particular, it encouraged countries to pursue ex-leaders and their accomplices in their own courts. At the time, the struggle to deal with legacies of repression was barely alive in many countries, especially those experiencing a transition from authoritarian or totalitarian to democratic rule, as in Latin America. Indeed, what some saw as an unnatural silence prevailed, with neither the courts nor the press able or willing to address past crimes. Now the unimaginable was possible (see "From unimaginable to possible: Spain, Pinochet and the judicialization of power", Journal of Spanish Cultural Studies, 3/1, March 2002). The Pinochet affair gave a huge fillip to human-rights movements, galvanising victims and their loved ones, activists and lawyers. Judiciaries hitherto admonished for their deference in the face of military dictatorships, were emboldened.

An era retrieved

In Chile, while some advances in human-rights accountability were evident prior to Pinochet's arrest, since 1998 the progress of human-rights trials has dramatically improved. The process is ongoing: on 15 October 2008, Chile's supreme court jailed five retired senior military officers responsible for the extra-judicial murder of seventy-five prisoners by the "caravan of death", a military death-squad that travelled up and down the country in October-November 1973.
 
Hizi nguvu mnazotumiaga kumnasua kwenye matokeo anayopata kwa nini msingezitumia kumshauri pindi awapo uraiani aishi kama RAIA mwema? Au ndo unafiki wenyewe huu! Hiyo njia kachagua mwenyewe maana yanaepukika hayo na anajua kabisa alishanusurika huko nyuma so mrelax kabisa.
 
Hizi nguvu mnazotumiaga kumnasua kwenye matokeo anayopata kwa nini msingezitumia kumshauri pindi awapo uraiani aishi kama RAIA mwema? Au ndo unafiki wenyewe huu! Hiyo njia kachagua mwenyewe maana yanaepukika hayo na anajua kabisa alishanusurika huko nyuma so mrelax kabisa.
Pumbav kweli kweli wewe, Zombe alipoua wale wafanya biashara wa Madini pale Sinza-ukuta wa Posta si mlisema hivi hivi na mkapiga makofi kwamba kaua majambazi kumbe yeye na maaskari wenzake ndio walikuwa majambazi?

Shwain/swine kabisa wewe, hiyo kosa la kubambikizia unasema ashauriwe?
Mshauri Kigwangala na wabunge wa ccm warudishe mali walizoiba na nyumba za serikali walizouza
 
Kwa taarifa za siri nilizonazo, baada ya biashara ya madawa kuota nyasi Dares salaam baada mkuu wa mkoa kuwataja hadharani ,wakuu wa ufipa waliweka kikao na kuamua kuhamishia biashara yao nyanda za juu kusini na wakamteua rasmi Mdude kuwa agent wao.!

Angalia baada ya Mdude kukamatwa ,mwenyekiti akapanic balaa na kuamua kuita waandishi wa habari ili kutengeneza mazingira ya kwamba Chadema wanaonewa kwa kubambikwa kesi.



Sent using Jamii Forums mobile app
unachikichiwa, Wewe ni Musiba, najua avatar yako , una psychopath , lehemu imekuzidi.
Gram 23 unajua ni bei gani na ujazo gani?Subiri kwanza UTAIRIWE kwa MSAADA wa watu wa MAREKANIakili zikukae vizuri, sisi tunaongea mambo ya msingi wewe unaleta upuuzi hapa.
 
KAMA NI KWELI BASI WANAWAKE SIO WA KUWAAMINI KABISA, HUWA WANATUMIKA SANA KUTUANGUSHA WANAUME
wewe ni perfect target ya event conspiracy theory iliyotumiwa na jeshi la polisi kwa bwana mdude.
 
Wiki jana ndugu Mpaluka Saidi Nyagali maarufu kama ‘Mdude Chadema’ alikamatwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya bila kuwekwa wazi sababu za kukamatwa kwake. Hakupandishwa mahakamani kwa karibu juma zima, na baada ya shinikizo kutoka sehemu mbalimbali polisi wamempeleka mahakamani na kumshtaki kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine zenye uzani wa gramu 23.4.

Baadae kidogo zikaibuka taarifa mitandaoni kuwa Mdude aliwekewa mtego wa dawa za kulevya na binti aliyekutana nae mtandaoni, wakaanzisha mahusiano na akamtumia kiasi fulani cha fedha.

Kwa sasa mjadala mkubwa si Mdude kudaiwa kukamatwa na dawa za kulevya bali kile kinachoitwa mtego uliotumika kumnasa, yani binti aliyeanzisha nae urafiki. Inawezekana madai haya yakawa kweli au yasiwe kweli. Nitatoa nadharia nne kuhusu kwanini yanaweza yasiwe kweli.

#Mosi; Kwa sisi tunaomfahamu Mdude (watu wake wa karibu) hatujawahi kumuona huyo binti wala kusikia habari zake kutoka kwa Mdude mwenyewe au ndugu zake. Si nyumbani kwa Mdude, kazini kwake au kwenye vijiwe vyetu vya siasa ambapo Mdude amewahi kumzungumzia kwa kudhamiria au kwa bahati mbaya.

Kwahiyo kama walikuwa na mahusiano basi yalikuwa ya SIRI sana na kukutana nao kulikuwa kwa nadra na kwa kificho sana. Lakini kadri nimjuavyo Mdude si rahisi kuanzisha mahusiano na mtu aliyekutana nae mtandaoni kirahisi. Mdude anajua yeye ni ‘target’ ya serikali kwa muda mrefu, kwahiyo hawezi kuingia mtegoni kirahisi hivyo.

#Pili; Mdude si mtuaji wa pombe wala sigara achilia mbali dawa za kulevya. Jamhuri inaweza kumpima ili kuthibitisha hili. Hanywi hata ‘Serengeti lite’. Mdude ni mwanaharakati ‘sobber’ kuliko wengi wetu tunaofanya harakati. Lakini akishika ‘mic’ sisi ndo hujiona ‘sobber’ kwa jinsi anavyoshusha nondo nzito. Sasa jiulize kama hanywi pombe au havuti sigara, hizo kete za ‘heroine’ alikuwa anazifanyia nini? Kupiga nazo picha aweke instagram?

#Tatu; Kwanini polisi imetumia siku 7 kumkamata hadi kumfikisha mahakamani kama kweli alikutwa na kete za heroine? It could be just simple baaada ya kumkamata wangemfikisha mahakamani kesho yake maana ushahidi wanao. Lakini kumkamata mtu bila kumwambia kosa lake, na kukaa nae siku 7 bila kumpeleka mahakamani inaleta ukakasi. Na hata baada ya siku 7 bado mnasita kumpeleka mahakamani hadi mpate shinikizo kutoka kwa jamii?

Je mtu akisema mlimkamata bila kosa, na mlikaa nae siku zote hizo mkijipanga mumpe kosa gani atakuwa anakosea? Scenario za polisi kubambikia watu kesi zipo nyingi sana. Waziri Mkuu Kassim majaliwa aliwahi kueleza kisa cha mfanyabiashara mmoja aliyekataa kutoa rushwa kwa polisi wakambambikiza kesi ya kukutwa na mali za magendo. Bahati nzuri Rais JPM aliingilia kati na kuagiza polisi na maafisa wa TRA waliohusika wafukuzwe kazi na kushtakiwa. Pia aliagiza ofisi ya TRA Ilala imfidie mfanyabiashara huyo.

Si hivyo tu, wakati wa JK wafanyabiashara watatu wa madini ambao ni ndugu kutokea Mahenge mkoani Morogoro waliwahi kukamatwa na kunyang’anywa fedha (milioni 200) na madini waliyokuwa nayo kisha wakauawa na kupakaziwa ujambazi. Tume ya Jaji Kipenka ilibaini baadae kuwa watu hao hawakuwa majambazi.

Visa vya polisi kubambikizia raia kesi ni vingi sana. Hata katika mazingira ya kawaida unaweza kuzozana na askari ukakamatwa na kuwekwa mahabusu lakini kesho yake ukashangaa umepewa kesi ya kukutwa na bangi. Na usipohangaika utapandishwa kizimbani na wataletwa mashahidi "waliokukuta" na bangi, na unaweza kuhukumiwa kifungo, wakati kiuhalisia hujawahi kuiona bangi zaidi ya kwenye TV. Je haiwezi kuwa hivi kwa Mdude pia?

#Nne; Kuna uwezekano waliomkamata Mdude ndio haohao waliotoa taarifa kuwa amewekwa mtegoni na mwanadada ili kuhalalisha mashtaka dhidi yake. Michael Barkun wakati akielezea ‘Conspirancy theory’ alielezea dhana inayoitwa ‘Finite insight’ kwenye Event Conspirancy theory. Kwa kifupi dhana hii inahusisha kula njama za kubuni uongo na kuuvumisha ili uongo huo usaidie kuhalalisha uhalifu mlioufanya. Waswahili husema kujamba na kuwasha feni.

Bado hujanielewa? Ngoja nikupe mfano. Mwaka 1980 Rais Augusto Pinochet wa Chile alimuua mkosoaji wake mmoja Julio Parot baada ya kuilaumu serikali kukiuka haki za binadamu. Parot alidai utawala wa Pinochet hadi mwaka 1980 ulikua umeua zaidi ya watu 200,000 kwa njia mbalimbali, ikiwemo kipigo kikali, shoti ya umeme, kutupwa kwenye bwawa la mamba, kuburuzwa barabarani, kukatwa kiungo kimoja kimoja na njia nyingine za kikatili.

Parot alikamatwa na majasusi wa shirika la ujasusi la nchi hiyo National Intelligence Directorate (DINA) wakati huo likiongozwa na Manuel Contreras. Wakati akihojiwa akapewa mateso makali sana na kufariki dunia. Kwa siku mbili alizokuwa haonekani serikali haikusema kama inamshikilia. Kwahiyo alipokufa mikononi mwa vyombo vya dola ikawa mtihani mgumu.

Kwahiyo wakaipiga maiti yake risasi moja kwenye paji la uso, na kuichoma visu kadhaa tumboni kisha wakaibeba usiku wa manane hadi kwenye mtaa wa Pedro de Valdivia karibu na mto Mapocho na kuitelekeza hapo. Asubuhi polisi wakatoa taarifa kuwa wameokota maiti ya mwanaume mmoja anayesadikiwa kuwa amevamiwa na majambazi na kuuawa. Ikabainika ni Julio Parot.

Polisi ikaagiza msako mkali dhidi ya washukiwa wa uhalifu huo. Hatimaye ‘majambazi feki’ watatu wakakamatwa. Wakapandishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kusababisha mauaji ya Parot. Wakapatikana na hatia na kuhukumiwa kifo. Jamii na familia ya Parot ikaamini haki imetendeka.

Lakini jambo ambalo hawakujua ni kwamba serikali ya Pinochet ndiyo iliyomuua ndugu yao. Na majambazi walioletwa mahakamani walikuwa ni maafisa wa DINA. Na baada ya kuhukumiwa kifo ilitangazwa kuwa wamenyongwa lakini ukweli ni kuwa waliachiwa na kupangiwa kazi zingine nje ya nchi. Miaka 10 baada ya Pinochet kufurushwa madarakani, CIA ndio wakaujua ukweli huu.

Nimeeleza kisa hiki ili uelewe vizuri maana ya ‘Finite insight' tunapozungumzia 'Event conspirancy theory’. Unapokuwa huna taarifa za kutosha kuhusu jambo fulani wahalifu wanaweza kula njama za kubuni uongo na kuuvumisha ili uongo huo usaidie kuhalalisha uhalifu waliofanya.

Kwahiyo inawezekana taarifa ya Mdude kuingizwa mtegoni na mwanadada mrembo mwenye hela ni hadithi ya kubuni iliyolenga kuhalalisha mashataka dhidi yake kuhusu madawa ya kulevya. Na kwa kiasi fulani wamefanikiwa kwa sababu hata ukisoma mitandaoni ni kama vile watu wameshaamini kwamba Mdude alikutwa na dawa za kulevya.

Hakuna anayejaribu kuwaza kwamba mashatka ya Mdude yanaweza kuwa ya kubambikiziwa. Wengi wanawaza aliingiaje mtegoni kwa huyo dada?

Kwahiyo inawezekana waliomkamata Mdude ndio waliobuni na kusambaza 'hadithi' ya Mdude kuwekwa mtegoni na mwanadada ili madai yao ya kumkamata na dawa za kulevya yapate uhalali (Event conspirancy theory).

Sijui
.
tumeelewana?
.......
Malisa GJ

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo kakamatwa kwa amri kutoka Chato
Iwe amri imetoka chato au ahera yote sawa tu,wewe hizo post zake unaziona ziko sawa tu katika jamii na familia yako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wewe ni perfect target ya event conspiracy theory iliyotumiwa na jeshi la polisi kwa bwana mdude.
DAAH MKUU TUNAPOELEKEA HII NCHI KUNA SIKU KITAWAKA,HASA AKIPATIKANA TENA RAISI AINA YA MKULU BAADA YA MKULU KUMALIZA MUDA WAKE
 
Sawa dudu lawasha hujakosea..wana sak it?
Maelezo yako ya kishuleshule hayabadilishi ukweli kuwa mwenzetu ananyea debe...

Nipe mwongozo fundraising inafanyika wapi?

Ama tumemtosa mwana kimtindo?

Again kwa system za Africa keyboard huwa haisaidii sana..

. Let's do something
Unawashwa Wewe, WEKA HUO MSAADA maana mimi nimeona maelezo yanatosha.
MDUDE yupo gerezani.
Kesi imeanza.
Changie fedha za mawakili.
Ungana na wapinzaninkuondoa mfumo dhalimu, kisheria-sanduku la kura.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini pia utawala wa awamu ya tano unapoanza kutolewa mifano ya namna watu kama pinochet waliongoza serikali zao kwa kweli inabidi ujitafakari, hasa magufuri inabidi ajitafakari sana, maneno yanaumba na lisemwalo lipo.
 
Kwa taarifa za siri nilizonazo, baada ya biashara ya madawa kuota nyasi Dares salaam baada mkuu wa mkoa kuwataja hadharani ,wakuu wa ufipa waliweka kikao na kuamua kuhamishia biashara yao nyanda za juu kusini na wakamteua rasmi Mdude kuwa agent wao.

Angalia baada ya Mdude kukamatwa ,mwenyekiti akapanic balaa na kuamua kuita waandishi wa habari ili kutengeneza mazingira ya kwamba Chadema wanaonewa kwa kubambikwa kesi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ama kweli akili ni nywele kila mtua ana zake
 
Na mimi nakujibu kwa Nadharia!!

Nadharia yako 2:

Kutokutumia bidhaa haimaanishi huwezi kuuza bidhaa hiyo. Morocco ni wauzaji wakubwa wa mvinyo pombe lakini hawanywi. Mdude kinadharia alikuwa anauza kama wauza wengine.

Nadharia yako 3

kinadharia waliomkamata walitumia muda mwingi kabla ya kumpeleka mahakamani lengo wahakikishe wanajua mtandao ambao alikuwa anatengeneza wa 'hiyo biashara haramu '.Kazi hiyo kinadharia haiwezi kufanywa siku moja ama masaa michache.

Nadharia yako 4:

Kinadharia unatuaminisha kuwa 'kisiki2014' ambaye alitoa taarifa naye anahusika katika mchezo huu! Kwamba kinadharia ndiye alimuandalia honeytrap na kumuunganisha kwa madrugs lords!?

=====
Acheni vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vifanye kazi yake kwa usahihi. Acha kuvuruga uchunguzi kwa makusudi mleta mada.
 
Back
Top Bottom