Nadharia 4 kuhusu kisa cha Mdude na dawa za kulevya

Kwa huyu mjinga wacha ale alichopanda, kuna njia sahihi za kudai na kupigania haki lakini unapotusi viongozi wa juu wa nchi walioshikilia dola ina maana upo tayari kwa lolote.
 
Komredi Malisa umetegua kitendawili cha sitofahamu! Kuhusu 'kubambikiwa' hili halina mjadala hata kdg.
 
Kwa huyu mjinga wacha ale alichopanda, kuna njia sahihi za kudai na kupigania haki lakini unapotusi viongozi wa juu wa nchi walioshikilia dola ina maana upo tayari kwa lolote.
Usimwite mjinga yeye alikuwa akikupigania wewe usiyejitambua.
 
Mkweli Nani kigogo au huyu?
db91976a2438db38d48b4da9eaa59838.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usimwite mjinga yeye alikuwa akikupigania wewe usiyejitambua.
Kuna tofauti kati ya Utambuzi na kufanyia kazi Utambuzi na hapo ndo Ujinga unapong'amuliwa.

Itikadi za kisiasa zikikupofusha ndo utaona kutukana ni kujitambua. Ni ujinga kumsifu huyu bwege wakati wale anaowatukana na hao waliomzunguka ni jamii ile ile ya wenye dhambi ya udhalimu na ufisadi
 
Ukosoaji wa kistaarabu unaruhusiwa
lkn matusi na lugha chafu ni lazima ujiandae kukutana na wenye mamlaka.....
 
Huyu bwege anataka tu umaarufu wa kisiasa wa kijinga. Kwasababu wale anaowatukana wakihamia CHADEMA wanakuwa wapigania haki...WTF
Shida kubwa ni kushika dola ndiyo maana wanaomtuma walikubali kula matapishi yao kumkaribisha fisadi ili mradi azma itimie.
 
mambo yanayohusu serikali tuyaache maana hao ndo wamiliki wa sheria wanachi ni vivuli tu hawana chochote ni sawa wewe unanguvu asiye na nguvu anataka kushindana na wewe hutomwacha salama

hata makachero hakuna aliyewahi kuishi kwa amani ukitaka kuishi vizuri unakijua cha kufanya kaa kimya acha bwebwe
bwebwe ndio nini ?
hujui kuandika!!
 
huyu jamaa akitoka hata rudia tena kutoa matusi.
mpaka sasa hivi navyokwambia keshakabiziwa kwa jamaa wa kumpakata huko jela na keshaanza kutafunwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wiki jana ndugu Mpaluka Saidi Nyagali maarufu kama ‘Mdude Chadema’ alikamatwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya bila kuwekwa wazi sababu za kukamatwa kwake. Hakupandishwa mahakamani kwa karibu juma zima, na baada ya shinikizo kutoka sehemu mbalimbali polisi wamempeleka mahakamani na kumshtaki kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine zenye uzani wa gramu 23.4.

Baadae kidogo zikaibuka taarifa mitandaoni kuwa Mdude aliwekewa mtego wa dawa za kulevya na binti aliyekutana nae mtandaoni, wakaanzisha mahusiano na akamtumia kiasi fulani cha fedha.

Kwa sasa mjadala mkubwa si Mdude kudaiwa kukamatwa na dawa za kulevya bali kile kinachoitwa mtego uliotumika kumnasa, yani binti aliyeanzisha nae urafiki. Inawezekana madai haya yakawa kweli au yasiwe kweli. Nitatoa nadharia nne kuhusu kwanini yanaweza yasiwe kweli.

#Mosi; Kwa sisi tunaomfahamu Mdude (watu wake wa karibu) hatujawahi kumuona huyo binti wala kusikia habari zake kutoka kwa Mdude mwenyewe au ndugu zake. Si nyumbani kwa Mdude, kazini kwake au kwenye vijiwe vyetu vya siasa ambapo Mdude amewahi kumzungumzia kwa kudhamiria au kwa bahati mbaya.

Kwahiyo kama walikuwa na mahusiano basi yalikuwa ya SIRI sana na kukutana nao kulikuwa kwa nadra na kwa kificho sana. Lakini kadri nimjuavyo Mdude si rahisi kuanzisha mahusiano na mtu aliyekutana nae mtandaoni kirahisi. Mdude anajua yeye ni ‘target’ ya serikali kwa muda mrefu, kwahiyo hawezi kuingia mtegoni kirahisi hivyo.

#Pili; Mdude si mtuaji wa pombe wala sigara achilia mbali dawa za kulevya. Jamhuri inaweza kumpima ili kuthibitisha hili. Hanywi hata ‘Serengeti lite’. Mdude ni mwanaharakati ‘sobber’ kuliko wengi wetu tunaofanya harakati. Lakini akishika ‘mic’ sisi ndo hujiona ‘sobber’ kwa jinsi anavyoshusha nondo nzito. Sasa jiulize kama hanywi pombe au havuti sigara, hizo kete za ‘heroine’ alikuwa anazifanyia nini? Kupiga nazo picha aweke instagram?

#Tatu; Kwanini polisi imetumia siku 7 kumkamata hadi kumfikisha mahakamani kama kweli alikutwa na kete za heroine? It could be just simple baaada ya kumkamata wangemfikisha mahakamani kesho yake maana ushahidi wanao. Lakini kumkamata mtu bila kumwambia kosa lake, na kukaa nae siku 7 bila kumpeleka mahakamani inaleta ukakasi. Na hata baada ya siku 7 bado mnasita kumpeleka mahakamani hadi mpate shinikizo kutoka kwa jamii?

Je mtu akisema mlimkamata bila kosa, na mlikaa nae siku zote hizo mkijipanga mumpe kosa gani atakuwa anakosea? Scenario za polisi kubambikia watu kesi zipo nyingi sana. Waziri Mkuu Kassim majaliwa aliwahi kueleza kisa cha mfanyabiashara mmoja aliyekataa kutoa rushwa kwa polisi wakambambikiza kesi ya kukutwa na mali za magendo. Bahati nzuri Rais JPM aliingilia kati na kuagiza polisi na maafisa wa TRA waliohusika wafukuzwe kazi na kushtakiwa. Pia aliagiza ofisi ya TRA Ilala imfidie mfanyabiashara huyo.

Si hivyo tu, wakati wa JK wafanyabiashara watatu wa madini ambao ni ndugu kutokea Mahenge mkoani Morogoro waliwahi kukamatwa na kunyang’anywa fedha (milioni 200) na madini waliyokuwa nayo kisha wakauawa na kupakaziwa ujambazi. Tume ya Jaji Kipenka ilibaini baadae kuwa watu hao hawakuwa majambazi.

Visa vya polisi kubambikizia raia kesi ni vingi sana. Hata katika mazingira ya kawaida unaweza kuzozana na askari ukakamatwa na kuwekwa mahabusu lakini kesho yake ukashangaa umepewa kesi ya kukutwa na bangi. Na usipohangaika utapandishwa kizimbani na wataletwa mashahidi "waliokukuta" na bangi, na unaweza kuhukumiwa kifungo, wakati kiuhalisia hujawahi kuiona bangi zaidi ya kwenye TV. Je haiwezi kuwa hivi kwa Mdude pia?

#Nne; Kuna uwezekano waliomkamata Mdude ndio haohao waliotoa taarifa kuwa amewekwa mtegoni na mwanadada ili kuhalalisha mashtaka dhidi yake. Michael Barkun wakati akielezea ‘Conspirancy theory’ alielezea dhana inayoitwa ‘Finite insight’ kwenye Event Conspirancy theory. Kwa kifupi dhana hii inahusisha kula njama za kubuni uongo na kuuvumisha ili uongo huo usaidie kuhalalisha uhalifu mlioufanya. Waswahili husema kujamba na kuwasha feni.

Bado hujanielewa? Ngoja nikupe mfano. Mwaka 1980 Rais Augusto Pinochet wa Chile alimuua mkosoaji wake mmoja Julio Parot baada ya kuilaumu serikali kukiuka haki za binadamu. Parot alidai utawala wa Pinochet hadi mwaka 1980 ulikua umeua zaidi ya watu 200,000 kwa njia mbalimbali, ikiwemo kipigo kikali, shoti ya umeme, kutupwa kwenye bwawa la mamba, kuburuzwa barabarani, kukatwa kiungo kimoja kimoja na njia nyingine za kikatili.

Parot alikamatwa na majasusi wa shirika la ujasusi la nchi hiyo National Intelligence Directorate (DINA) wakati huo likiongozwa na Manuel Contreras. Wakati akihojiwa akapewa mateso makali sana na kufariki dunia. Kwa siku mbili alizokuwa haonekani serikali haikusema kama inamshikilia. Kwahiyo alipokufa mikononi mwa vyombo vya dola ikawa mtihani mgumu.

Kwahiyo wakaipiga maiti yake risasi moja kwenye paji la uso, na kuichoma visu kadhaa tumboni kisha wakaibeba usiku wa manane hadi kwenye mtaa wa Pedro de Valdivia karibu na mto Mapocho na kuitelekeza hapo. Asubuhi polisi wakatoa taarifa kuwa wameokota maiti ya mwanaume mmoja anayesadikiwa kuwa amevamiwa na majambazi na kuuawa. Ikabainika ni Julio Parot.

Polisi ikaagiza msako mkali dhidi ya washukiwa wa uhalifu huo. Hatimaye ‘majambazi feki’ watatu wakakamatwa. Wakapandishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kusababisha mauaji ya Parot. Wakapatikana na hatia na kuhukumiwa kifo. Jamii na familia ya Parot ikaamini haki imetendeka.

Lakini jambo ambalo hawakujua ni kwamba serikali ya Pinochet ndiyo iliyomuua ndugu yao. Na majambazi walioletwa mahakamani walikuwa ni maafisa wa DINA. Na baada ya kuhukumiwa kifo ilitangazwa kuwa wamenyongwa lakini ukweli ni kuwa waliachiwa na kupangiwa kazi zingine nje ya nchi. Miaka 10 baada ya Pinochet kufurushwa madarakani, CIA ndio wakaujua ukweli huu.

Nimeeleza kisa hiki ili uelewe vizuri maana ya ‘Finite insight' tunapozungumzia 'Event conspirancy theory’. Unapokuwa huna taarifa za kutosha kuhusu jambo fulani wahalifu wanaweza kula njama za kubuni uongo na kuuvumisha ili uongo huo usaidie kuhalalisha uhalifu waliofanya.

Kwahiyo inawezekana taarifa ya Mdude kuingizwa mtegoni na mwanadada mrembo mwenye hela ni hadithi ya kubuni iliyolenga kuhalalisha mashataka dhidi yake kuhusu madawa ya kulevya. Na kwa kiasi fulani wamefanikiwa kwa sababu hata ukisoma mitandaoni ni kama vile watu wameshaamini kwamba Mdude alikutwa na dawa za kulevya.

Hakuna anayejaribu kuwaza kwamba mashatka ya Mdude yanaweza kuwa ya kubambikiziwa. Wengi wanawaza aliingiaje mtegoni kwa huyo dada?

Kwahiyo inawezekana waliomkamata Mdude ndio waliobuni na kusambaza 'hadithi' ya Mdude kuwekwa mtegoni na mwanadada ili madai yao ya kumkamata na dawa za kulevya yapate uhalali (Event conspirancy theory).

Sijui
.
tumeelewana?
.......
Malisa GJ
Kila mtu Ashinde mechi zake.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nachojiuliza masikini kama yule kilo 23 za heroine ni mamilioninya shilingi.Angeshaporomosha hata mnjengo wa maana hapo Vwawa.Lakini alikuwa mtu wa kawaida tu.Angeficha hela benki zingeonekana.Au anaficha chini hizo pesa kwenye mahandaki? Mungu ampe wepesi

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu, sio kilo, ni gramu 23.
 
Kuna maudhui ya mabandiko ya mdude huwa yanakela Sanaaaa kutokana na lugha anayo TUMIA

Rai YANGU kwa mamlaka husika wamwachie huru huyu kijana....
Mfano
Ningekua na mamlaka kweny serikali ya magu ningemchukua huyu kijana nikampa fund alafu nikamwambia aandae proposal ya mradi kweny sekta yeyote alaf nikamfinance
Zile nguvu alizo kua anatumia kutoa lugha ngumu na kashifa kwa selikali...
Itumike katika kuleta maendeleo kwenye JAMII..
Ninge mpa kila rasilimali na wataalam wa kumpa mwongozo kufikia lengo la huo mrad alio uchagua...
Sijui Kama atapata muda wa kua ana post lugha ngumu na matusi kwa Watawala
Mm najaribu kutazama ishu ya mdude in positive way
 
Back
Top Bottom