Nadhani Tundu Lissu anakosea hapa

wewe wacha uharoo wako nchi hii imefikishwa hapa na CCM full stop. ebu tizama nchi nyingine kama korea , Malaysia , vietnam, singapore.Tanzania muna nini ni zogo tu hamuna lolote leo ni miaka 58 ya ccm kutawala hata maji ya kunywa hakuna halafu unatuletea porojo kwa kweli watanzani wana kila haki yakuombwa radhi na CCM kwa uchama waliofanyiwa na ccm.
....kama korea , Malaysia , vietnam, singapore. Kwanini usiseme ..... kama Burundi, Kenya, Uganda, Malawi, Zambia, Sudani Kusini, Zimbabwe, Ghana? huko kote ni CCM inayotawala? iko siku tutauana wenyewe kwa wenyewe kipumbavu na kumuacha adui yetu wa kweli kuitawala Tanzania
 
Lazima tuwe maskini na tutaendelea maskini, maana tunafanya makosa yale yale kila siku.
Yaani nchi ya watu 53milion lakini maamuzi bado yanafanywa na mtu mmoja, ambaye ni binadamu kama sisi, huyo mtu mmoja ndio Alfa na omega wa Tanzania, siku tukibadilisha huu mfumo ndipo hapo tutakapoanza kupiga hatua kwenda mbele kikweli kikweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umefanya utafiti kuhusu hilo unalosema? Huu umasiki mbona uko kwenye nchi zote za afrika kusini kwa jangwa la sahara? na huko kuna CCM au KATIBA ZAO NI KAMA ZETU?
 
Hebu tuwekee mazuri ya huyu dikteta kati ya haya ni yapi mazuri yake?

  1. Kudharau katiba?
  2. Kudharau mahakama?
  3. Kudharau bunge?
  4. Kujichotea trillions hazina kinyemela?
  5. Kuminya haki ya opposition parties?
  6. Kuja na miswaada ya kidikteta?
  7. Kudhulumu wakulima na wafanyakazi?
  8. Kuminya Uhuru wa vyombo vya habari?
  9. Kuwa muongo muongo?
  10. Kutumia vikaragosi vyake kumchafua na kumtisha CAG
  11. Kutumia vikaragosi vyake kumchafua na kumtisha Lissu?
  12. Kutumia zaidi ya bilioni 80 kununua wabunge na madiwani wachumia gumbo?
  13. Kufanya Watanzania walio wengi kuishi kwa hofu Lunda?
  14. Kukurupuka na maamuzi ya ajabu ajabu yanayoathiri uchumi?
  15. Kutoa Kauai za hovyo hovyo kila mara?
Nadhani anajaribu kutenda tofauti na kila kitu kilichotufikisha hapa. Hivi vyote ulivyovitaja vilikuwepo kwenye awamu zilizomtangulia lakini hali yetu inazidi kudidimia, kuna ubaya gani akibadilisha uelekeo wa namna ya kuyaendea mambo? yaani wengine wametumbukia shimoni kwa kufuata njia hiyo, nayeye akatumbukie kama akiamua kuifuata njia hiyohiyo vilevile? lazima atumie uncommon sense, ili tumhukumu vizuri baada ya muda wake kumalizika, au veepee!
 
Kwahiyo unataka kusema lissu hana tofauti ni yale matoto yanayopenda kujiliza liza nakwenda kule bbc hardtalk ilikuwa nisawa na kwenda kusema kwa baba kuwa amepigwa?maana hakuna cha maana alichokuwa anaongea zaidi ya kuonesha chuki zake kwa jpm ndo maana jamaa kamuona kama chizi fresh vile.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli Stephen Sucker alijuta kumualika kwenye kipindi chake chenye hadhi ya hali ya juu. Hana alichoambulia pale, alitamani kusikia hoja conc.
 
Umetaja mazuri anayoitendea nchi yasiyo paswa kukosolewa, Fine. Mbona hujataja hata moja baya yanayowapasa wapinzani wake kumkosoa ?!. Au ni malaika asiyepaswa kukosolewa ?!
HEBU JARIBU KU BALANCE U A STORY. Kwa sababu nchi ni ya wote (watawala & watawaliwa).

Sent using Jamii Forums mobile app
Maoni yangu: Ni mapema mno kumkosoa, nadhani amekuta taarifa nyiiiiiiiiingi sana za kiintellegensia ambazo ndizo zilizokuwa zinalitafuna taifa hili ambazo huenda zilikuwa hazifanyiwi kazi na waliomtangulia kutokana na sanabu zao mbalimbali. sasa unapoona Rais anazifanyia kazi sisi tusiofahamu tunawezakumuona anakosea kumbe ni njia sahihi ya kutatua tatizo la vibaraka wa magharibi, wakwepa kodi, mafisadi, majangili wa wanyama pori, majambazi, wahamiaji haramu, wafanyakazi na wanafunzi hewa, wezi, wauaji, nk ambao bila shaka ni wengi saana. Hebu tuwe na subira kidogo jamani, maana kama wewe hujauawa wala kutekwa basi wewe uko safi, huna mawaa, keep it up!!.
 
Kwahiyo 'uncommon sense' ndiyo humtuma Jiwe kuua watu?
Hatuna ushahidi na hilo mkuu, lakini hata angekuwa mm nisingeona taabu sana kuua majangili wa tembo, vibaraka wanaohatarisha usalama na uchumi, majambazi. Vilevile nisingekuwa vigumu kwangu kupambana kwa nguvu zangu zote na wakwepa kodi wote, viongozi wasiowajibika kwa watu, wanaotumia ruzuku kwa manufaa ya familia, ukoo na ukanda wao.
 
Ununuzi wa ndege kwa cash kuna ufisadi wa kutisha sana pesa nyingi imepigwa na wajanja wachache kwani bei halisi ya ndege ipo chini kuliko pesa waliyonunua kifisadi, kuna ujanja mwingi kwenye ununuzi wa ndege na hata CAG wanataka kumtoa ofisini ili kukwepa asiwaumbue kabla ya 2020.
Habari kama hizo ni nzuri sana, leta ushahidi uone watu watakavyoungana na wewe kukusuport hoja yako, lakini sio kuongea tuhuma kama hizo bila ushahidi, na huo ndio uliokuwa ugonvi wa Stephen Sucker na lissu.
 
Watetezi wa CCM wengi ni mbumbumbu vilaza hawaoni mapungufu ya mtukufu malaika toka chato bali wamekomalia kitu kimoja tu.
Inaonyesha kama 2015 mgombea wako angepita Tanzania ingeuzwa kwa bei poa. Hivi utatumia miujiza gani kumlazimisha mkwepa kodi kwa miaka 20 akubali kulipa kodi, jambazi aache kuiba, jangili aache kuua wanyama, hakimu asichukue rushwa, traffic asichukue rushwa, vyama vitumie ruzuku kama mali yao, makuwadi wa nchi za magharibi wache ukuwadi, mafisadi waache tabia yao, wafanyakazi na wanafunzi hewa waondoke? Wataacha kwa kutabasamu kweli? Watu walikuwa wanafanyia mikutano kwenye mahoteli makubwa Dar es Salaam, Arusha, Morogoro, dododma, uarabuni, sa wataacha kweli kwa kiongozi mwenye akili kama yako?
 
Tanzania ni nchi masikini sana, tangu tupate Uhuru hatujawahi kuwa na nafuu, hata Rais Magufuli ameikuta hivyohivyo ikiwa na hali mbaya. Sio siri, wote tunafahamu kuwa wakoloni hawakuondoka kipumbavu wakati wanaliachia bara la Africa ikiwemo Tanzania yetu. Tunafahamu kuwa wakoloni wanatumia njia mbali kuendelea kupata malighafi, masoko ya bidhaa zao, na nguvukazi. Tunafahamu kuwa wakoloni wanatumia mafariki zao ambao sisi tunawaamini sana kama vile viongozi maarufu, watu maarufu, mashirika ya hisani, mashirika na taasisi za kidini, viongozi wa vyama vya siasa, wanaharakati, WB, IMF, WTO na majasusi kufanikisha adhima zao hizo.

Rais Magufuli ameamua kujilipua na kutumia uncommon sense kutatua common problems zinalolikumba bara lote la Africa hasa kusini mwa jangwa la Sahara. Maana huwezi kutumia common sense kutatua common problems yaliyowashinda Marais wenzako waliokutangulia. Hata wazungu walitumia uncommon sense kufika pale walipofika, uncommon sense yao Ndiyo iliyowatuma watutawale, watufanye watumwa, watufanyishe kazi nyingi bila ujira, kuua Marais wetu waliopinga kunyonywa nk.

Tundu Lissu hakupaswa kupinga kila kitu cha Rais Magufuli kwakuwa vitu ambavyofanya kamavile kuondoa wafanyakazi na wanafunzi hewa, kukamata wakwepa kodi, wauza madawa ya kulevya, kuwaondoa viongozi wasiowajibaka, kujenga miundombinu ya kisasa kama barabara, madaraja na reli, elimu bure , kufufua shirika la ndege na reli, nk. hivi vyote vinaonekana hadharani Kwa watanzania na wasiokuwa watanzania.

Tundu Lissu anapaswa ku acknowledge mazuri na ku condemn mabaya, hapo kila mtu angemuelewa. Rais wetu kuna vitu anavifanya kinyume kabisa na matarajio ya wakoloni tusipomsaidia sio Tu atapandwa na hasira lakini tunaweza kuhatarisha uhai wake Kwa ajili yetu sote.
Hata wademocratics wana vitu wanamkosoa Trump lakini kuna vitu hawezi kumkosoa navyo kwakuwa ni kwamanufaa ya Yao
wote
Tundu Lissu alikosea kutokimbilia Muhimbili baada ya kupewa risasi 38.
 
mimi ni ccm na kwa kisiasa simkubali Lissu kabisa,lakini kibinaadamu ntamtetea kwa akili zangu zote,nguvu zangu zote na uwezo wangu wote

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna vitu kwenye projects vinaitwa nuisances, outliers, na confounders. Hivi vitu ni vitu hatari sana wakati unapotafuta matokeo mazuri ya project yako. Wako watu ambao ni nuisances, outliers, na confounders wakati serikali inapotaka kutufuta chanzo halisi cha matatizo na umaskini unaowakabili wananchi na kufanya utekelezaji (interventions). Lazima project manajor atufute mbinu madhubuti wa kutambua vyanzo vya nuisances, outliers, na confounders na namna ya kuvi address (keep them constant). Na mara nyingi watu hawa ni wale au wawakilishi wao wanaotaka na kulilia "status quo"
 
Wasadika wanadhani tundu lissu au mbowe akiwa rais basi watasahau shida zao, wanadhani hakutatokea mauaji tena, wanadhani watakua huru kuongea chochote hata matusi kwa viongozi.
Wasadikika wanadhani tatizo la nchi hii ni CCM pekee na magufuli, hakika wasadikika wamechoka kiakili na kimwili. Sehemu pekee ya kutolea hasira zao ni hapa kwenye social networks.... waacheni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata matusi yakiwa mengi kiasi gani, Magufuli atabaki kiongozi mwenyewe kujielewa Sana katika Bara Afrika, huwezi ukajenga nchi kwa kubembeleza watu, kuongoza nchi maskini kunahitaji mtu mwenye kuthubutu, na mwenye maamuzi, Huyu ndiye kiongozi hasa wa kizazi cha wenye matusi.
 
Tanzania ni nchi masikini sana, tangu tupate Uhuru hatujawahi kuwa na nafuu, hata Rais Magufuli ameikuta hivyohivyo ikiwa na hali mbaya. Sio siri, wote tunafahamu kuwa wakoloni hawakuondoka kipumbavu wakati wanaliachia bara la Africa ikiwemo Tanzania yetu. Tunafahamu kuwa wakoloni wanatumia njia mbali kuendelea kupata malighafi, masoko ya bidhaa zao, na nguvukazi. Tunafahamu kuwa wakoloni wanatumia mafariki zao ambao sisi tunawaamini sana kama vile viongozi maarufu, watu maarufu, mashirika ya hisani, mashirika na taasisi za kidini, viongozi wa vyama vya siasa, wanaharakati, WB, IMF, WTO na majasusi kufanikisha adhima zao hizo.

Rais Magufuli ameamua kujilipua na kutumia uncommon sense kutatua common problems zinalolikumba bara lote la Africa hasa kusini mwa jangwa la Sahara. Maana huwezi kutumia common sense kutatua common problems yaliyowashinda Marais wenzako waliokutangulia. Hata wazungu walitumia uncommon sense kufika pale walipofika, uncommon sense yao Ndiyo iliyowatuma watutawale, watufanye watumwa, watufanyishe kazi nyingi bila ujira, kuua Marais wetu waliopinga kunyonywa nk.

Tundu Lissu hakupaswa kupinga kila kitu cha Rais Magufuli kwakuwa vitu ambavyofanya kamavile kuondoa wafanyakazi na wanafunzi hewa, kukamata wakwepa kodi, wauza madawa ya kulevya, kuwaondoa viongozi wasiowajibaka, kujenga miundombinu ya kisasa kama barabara, madaraja na reli, elimu bure , kufufua shirika la ndege na reli, nk. hivi vyote vinaonekana hadharani Kwa watanzania na wasiokuwa watanzania.

Tundu Lissu anapaswa ku acknowledge mazuri na ku condemn mabaya, hapo kila mtu angemuelewa. Rais wetu kuna vitu anavifanya kinyume kabisa na matarajio ya wakoloni tusipomsaidia sio Tu atapandwa na hasira lakini tunaweza kuhatarisha uhai wake Kwa ajili yetu sote.
Hata wademocratics wana vitu wanamkosoa Trump lakini kuna vitu hawezi kumkosoa navyo kwakuwa ni kwamanufaa ya Yao wote
Hakuna anayesema huyu rais hajafanya zuri lolote. Yapo mengi lakini kupata swali moja au mawili katika mtihani wenye maswali 10 yenye alama zinazolingana hakukupi ushindi wa mtihani mzima. Kupata A -100% ya somo la chemistry na F kwenye masomo matatu ya sayansi na hisabati kunakufanya ukose combination. Hicho ndicho tunacho kisema. Nimeufanyia tathimini utawala wa awamu ya tano, angalia kiaambatanisho.
 
Wasadika wanadhani tundu lissu au mbowe akiwa rais basi watasahau shida zao, wanadhani hakutatokea mauaji tena, wanadhani watakua huru kuongea chochote hata matusi kwa viongozi.
Wasadikika wanadhani tatizo la nchi hii ni CCM pekee na magufuli, hakika wasadikika wamechoka kiakili na kimwili. Sehemu pekee ya kutolea hasira zao ni hapa kwenye social networks.... waacheni

Sent using Jamii Forums mobile app
Ikiwa hivyo tutasema. tatizo lenu hamtaki tuseme.
 
Back
Top Bottom