Nadhani Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lipo katika hali mbaya ya kifedha

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,327
24,209
Hili shirika la kujenga nyumba kwa wananchi, National Housing Corporation NHC, sasa imethibitika liko katika hali mbaya sana kifedha.

Hii ni licha ya kuambiwa uchumi wetu wa viwanda unakua kwa zaidi ya 7%.

Miradi iliyo mbele ya macho na inaonekana kila siku pale Morocco na Kawe, imesimama kabisa kwa miaka takriban minne sasa.
Hiyo ni dalili tosha kudorora kwa NHC.

Siyo siri, tutakachosikia punde ni shirika kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi.

MAHAME YA KAWE BEACH

20191023_153452.jpg
20191023_150858.jpg
 
Hlo shirika lilikuwa kiupigaji zaidi.....!!! Na kama hlo shirika lingefata sera yao nafkr watu wasingehangaika kujenga nyumba , but likageuzwa kuwa mradi wa watu wachache wa kupeana tenda , nyumba ya mil 25 inauzwa mil 85,....mwisho wakaamua kurundika maghorofa dsm ambayo sasa ni makaz ya popo
 
ujenz wa NHC ni wa kipigaji sana.. wananunua kilo moja ya misumari kwa laki moja... kiwanja porini wananunua mabilioni
 
Kwa akili ya kawaida NHC kuwa na shida ya ukwasi inajieleza yenyewe
1. Miradi mingi mikubwa ilikuwa Dar, Wapangaji wengi hawapo
2. Hali ya kiuchumi so nzuri, hivyo makampuni mengi yamejenga ofisi zao au wamepanga majengo ya bei rahisi
3. Wapangaji wengi kwa ajili ya makaazi nao hawana hela
 
Kujenga nyumba siyo kazi rahisi mkuu, ndo maana kuna taasisi kubwa mfano vyama vya siasa vikubwa na vikongwe lakini hadi leo vinaishi kwenye nyumba za kupanga.
 
Hlo shirika lilikuwa kiupigaji zaidi.....!!! Na kama hlo shirika lingefata sera yao nafkr watu wasingehangaika kujenga nyumba , but likageuzwa kuwa mradi wa watu wachache wa kupeana tenda , nyumba ya mil 25 inauzwa mil 85,....mwisho wakaamua kurundika maghorofa dsm ambayo sasa ni makaz ya popo
Waziri mwenye dhamana yuko kimya utafikiri hayaoni yale maghorofa kila siku.

Watumie Force Account kuyamalizia.
 
Hili ni janga kubwa litakalotikisa mabenki muda si mrefu.

Fikiria mtu alichukua mkopo benki kwa ajili ya kununua nyumba, hapo inamaana anaanza kuulipia mkopo wake kuanzia sasa.

Walionunua walitegemea kufikia muda flani watakabidhiwa nyumba zao waanze kuingiza pesa zipunguze mzigo wa marejesho ya mkopo, kwa mwendo huu inamaana wengi watashindwa kurejesha pesa. Kilio kitasambaa kwa benki zilizowakopesha hawa jamaa.
 
Hili shirika la kujenga nyumba kwa wananchi, National Housing Corporation NHC, sasa imethibitika liko katika hali mbaya sana kifedha.

Hii ni licha ya kuambiwa uchumi wetu wa viwanda unakua kwa zaidi ya 7%.

Miradi iliyo mbele ya macho na inaonekana kila siku pale Morocco na Kawe, imesimama kabisa kwa miaka takriban minne sasa.
Hiyo ni dalili tosha kudorora kwa NHC.

Siyo siri, tutakachosikia punde ni shirika kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi.
Ni wazi kuwa Magufuli haipendi NHC. Ndio maana akasimamisha hata mradi wa Kigamboni.
Shirika litakufa kwa kiasi flani ila lipo bussy kufawa viwanja na kuijenga chato
 
Hili ni janga kubwa litakalotikisa mabenki muda si mrefu.

Fikiria mtu alichukua mkopo benki kwa ajili ya kununua nyumba, hapo inamaana anaanza kuulipia mkopo wake kuanzia sasa.

Walionunua walitegemea kufikia muda flani watakabidhiwa nyumba zao waanze kuingiza pesa zipunguze mzigo wa marejesho ya mkopo, kwa mwendo huu inamaana wengi watashindwa kurejesha pesa. Kilio kitasambaa kwa benki zilizowakopesha hawa jamaa.
Meko doesnt care!
 
Nilitaka kununua hapo apartment mwaka 2015, kama nakumbuka vizuri. Walikuwa wanauza kabla ya ujenzi kukamilika. Rafiki yangu akanambia kwa nini ninunue kabla nyumba haijamalizika? Machale yakanicheza. Nje ya nchi watu wananunua baada ya nyumba kumalizika, siyo kununua apartment kabla ya ujenzi kumalizika. Asante rafiki kwa ushauri wako. Kwa jinsi bei za apartments hapo zilivyo kubwa, labda ningejiua kama hiyo pesa ingekwenda bure.
Miradi iliyo mbele ya macho na inaonekana kila siku pale Morocco na Kawe, imesimama kabisa kwa miaka takriban minne sasa.
Hiyo ni dalili tosha kudorora kwa NHC.
 
Hapa ndio huwa tunakosea. Kwa nini ununue nyumba ambayo haijakamilika?
Walionunua walitegemea kufikia muda flani watakabidhiwa nyumba zao waanze kuingiza pesa zipunguze mzigo wa marejesho ya mkopo, kwa mwendo huu inamaana wengi watashindwa kurejesha pesa. Kilio kitasambaa kwa benki zilizowakopesha hawa jamaa.
 
Kwa akili ya kawaida NHC kuwa na shida ya ukwasi inajieleza yenyewe
1. Miradi mingi mikubwa ilikuwa Dar, Wapangaji wengi hawapo
2. Hali ya kiuchumi so nzuri, hivyo makampuni mengi yamejenga ofisi zao au wamepanga majengo ya bei rahisi
3. Wapangaji wengi kwa ajili ya makaazi nao hawana hela
Sio sahihi kabisa,shirika lilikuwa na upigadili wa hali ya kutisha ndio maana unaona kila kilichofanyika kiwizi kimesimama....
 
Hapa ndio huwa tunakosea. Kwa nini ununue nyumba ambayo haijakamilika?

NHC walikuja na mbwembwe sana mkuu.
Yale matangazo na uhamasishaji ukawapagawisha watu. Kwa vile kulikua na uhakika wa ile miradi kukamilika kwa wakati, mabenki na wateja wakaingia mkenge.
 
Hili shirika la kujenga nyumba kwa wananchi, National Housing Corporation NHC, sasa imethibitika liko katika hali mbaya sana kifedha.

Hii ni licha ya kuambiwa uchumi wetu wa viwanda unakua kwa zaidi ya 7%.

Miradi iliyo mbele ya macho na inaonekana kila siku pale Morocco na Kawe, imesimama kabisa kwa miaka takriban minne sasa.
Hiyo ni dalili tosha kudorora kwa NHC.

Siyo siri, tutakachosikia punde ni shirika kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi.
Umesikia (usidhani), usituaminishe kuwa umefanya uchunguzi na kuliona hilo, weka habari kama wote tulivyoisikia na chanzo chake si wewe.
 
Back
Top Bottom