Nadhani sasa tumemuelewa Pinda alichomaanisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nadhani sasa tumemuelewa Pinda alichomaanisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Consigliere, Aug 5, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,047
  Likes Received: 7,506
  Trophy Points: 280
  Wana-JF kwa muda wa masaa 36 yaliyopita wengi wetu tumekuwa tukishanda hapa nyavuni, tukijaribu kuangalia nini nyavu zinaweza zikanasa kuhusiana na sakata Luteni General Shimbo.

  Wachangiaji wengi tulijitokeza na kuongeza idadi ya posts (point)zetu, ambazo mwisho wake tumepigwa penalt au tumepokwa idadi baada ya uzi ule kuondolewa.

  My Take:

  Tuliwahi kumsikia waziri mkuu Mizengo Pinda akigoma kuongelea masuala yahusuyo Meremeta kwa kuwa ipo connected na Jeshi, na akaendelea kusema kwa jinsi hiyo ni suala zito na yupo tayari kwa next step/level kuliko kuongelea jambo hilo.

  Wengi walimbeza Pinda labda kwa kushindwa kumuelewa (si kila jambo tunapaswa kuelezwa na kulielewa, yatupasa tusubiri yatupate ndipo tutaelewa).

  Hali hiyo ikajitokea hapa JF (for good thou), tukaongea tuliyoyaongea, na wengine wakatoa hukumu, wengine wakanena kwa lugha na wengina pressure ziliwapanda, wengine zikawashuka.

  Wakuu wa JF wakaahidi kutoa documents ....tik tok tik tok....masaa yakaenda, nao wakafuata nyao za Pinda, wakaona ni heri walaumiwe na ikibidi wawe tayari kwa next/level (lawama), hata kushusha status, lakini ni heri waiondoe ile thread kuliko kuendelea kuliongelea suala lile nyeti(for good also).

  Mtazamo wangu na natumaini ndivyo itakuwa kwa wana JF wengi, kwangu au kwetu kamwe status zenu hazitashuka, mumefanya mengi kufika hapa tulipo. Kuondolewa kwa thread ile ni all for good, hakubadilishi hali, isipokuwa inaweza ikawa ni ugunduzi mpya ndani yake wenye ujio wa kivingine.

  Kwa wafanyakazi wana Descriptions wao hujua nini hutokea kushindwa kuzi-follow na ku-fulfill hizo descriptions, wafanyabiashara wana plans kuna kipindi huwa zina go soar, hawa itokeapo malengo yao yasitimie huwa wanatengeneza promises na ways na to avoid failures.

  Sisi wengine tuna missions, huwa inatokea tunashindwa kuzi-accomplish, japo hutugharimu lakini tunazichukulia kama changamoto na kuongeza commitments katika mikakati ijayo.

  Huu si wakati wa harakati, bali ni wakati wa mapinduzi halisi......hivyo tusimame na kupambana kwa nia, yaliyotokea hapa ni yetu sote, hatutamuacha mpambanaji yeyote nyuma bali kwa kila atakaye dondoka tutampa a suppoting hand na kuendelea kusonga mbele, mpaka kwenye mstari wa mafanikio.


  My Conclusion - Nadhani sasa tumejifunza kitu na kumuelewa Pinda. Na halii tuichukue kama gauge ya kupima mazingira yanayotukabili na tuliyoamua kukabiliana nayo.

  Tupo pamoja.
   
 2. Msusu

  Msusu Member

  #2
  Aug 5, 2011
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  good analysis.
  Ila kuna haja ya kuchukua hatua..., ni kwa faida ya nani kwamba kila linapotokea jambo linalogusa jeshi then we should keep quite hata kama ni jambo linaloumiza kiasi gani. sijui ni nini ni katiba au ni nini kinachozuia kuhoji maamuzi na mamlaka ya jeshi, kwa mtindo huu itafikia hatua hata wakiua raia wasio na hatia tutaishia kunyamaza na kusema acha tulaumiwe lakini tusihoji.

  tutafakari upya, tuje na new strategy ya kuhandle haya mambo, otherwise wote tutaamua kwenda jeshini sijui sasa nani atamnyooshea mwenzake kidole.
   
 3. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Jeshi jeshi na tusihoji kwa nini?je wao ni mungu watu?wao wako juu ya sheria?wanafanya ufisadi then tusihoji why?issue ya meremeta na jamaa wa afrika kusini ni ufisadi yani huwezi kopa 10b then ukalipa 136b,huu ni ujinga na upumbavu,then tusihojh!hela hizo ni zanani?
   
 4. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Natamani sana kama wote tungekuwa na sekunde chache tu tukafanana mawazo na fikra wote tulio kwenye jamvi lakini kwa kuw Mungu alituumba kwa utashi wake hakika haitatokea ila kila mmoja kwa wakati wake as the time goes on tunaelewana lugha na kuafikina kuwa jambo hili linalotuhusu ni sawa katika vigezo hivi na vile.

  Sniper kuna sehamu kasema swala lile ni nyeti [For so good] JF kaliweka pembeni hakika ni sahihi.Kama waelevu [Intellectuals] sio kila kitu kitawekwa usoni mwa kila mtu basi kama ndio hivyo Nchi haiwezi kutawalika.

  Kwa Mwana JF yoyote yule makini na mwelewa hakuna asiyejua nini kinachoendela katika siasa na uchumi ndani ya Nchi mambo. Na mambo mengi sana ya msingi yanaitaji BUSARA NA HEKIMA zaidi katika kuyaamua na kuyatenda kwa kuzinagtia zaidi Taifa lilipofika sasa.

  Zamani tulikua na Baba wa Taiffa ambae kisaikolojia wengi wa viongozi wetu walimuogopa na kumuheshimu kwa hadhi ya Baba na Mwana.Lakini alipotoka madarakani basi hata heshima ile ikapotea tena.Hivyo watoto hao hao wamejisimamia lakini kila mmoja kwa nafasi bila kujali maadili ya Baba kuwa anaacha keki kwa faida ya Wanataifa wote,viongozi wamegeuka kuimega keki na kula pekee yao.

  Lakini katika kula keki hiyo sio kuwa hakuna watoto wengine wasio furahiishwa na jinsi keki inavyoliwa na kuwa watapambana na walaji wa keki ya Taifa.Kama umepata kubahatika kuona ugomvi wa mali ya urithi kuna wale wenye tamaa kurithi vyote na kuwanyima wengine.Ndivyo siasa za Tanzania zimetufikisha kwa kuwa viongozi wetu wengine wamekuwa na tamaa.Na wewe ambae unatamani upate mgao wa mali ya urithi kama utatumia busara wenye uchu na mali hiyo wenzio wanaweza kukuwekea sumu kwenye maji ufe,wakuroge kwa imani zetu za kiafrika,wakusingizie kesi ufungwe na kisha wao wachukue mali zote ili usiambulie hata kile kidogo chako.

  Hakika kuna mengine ni muhimu kwa usalama wa Nchi,lakini watendaji wetu walipowachia wasiasa na wasanii wa sanaa za jukwaan [Wizi wa mjini] kuwaibia watanzania na kuwapa mamlaka na kisha baada yake kuwatosa wametumia ujuzi wa kujua dola inaendeshwaje nao kwa kuwa walitaka kukaa kiti kikuu basi wametumia udhaifu huo kuidhalilisha dola.

  Na vigezo hivyo vya usalama, MAFISADI wameingiza michezo yao leo hii HATA KWA UKWELI HALISI AMBAO NI KWA FAIDA YA USALAMA WA TAIFA,bado wananchi wakisikia HATA AMINI NA KUKUBALI NI KWA MASALAHI YA TAIFA na ili uwafafanulie waelewe bado haitakuwa sawa kwao,kwa kuwa ni Mtu kaumwa na Nyoka akiona unyasi anastuka.Na ukiwaeleza wananchi wote ili watambue dhamila ya matendo tuhumiwa bado haitakuwa ndio huo usalama unaotafutwa na kusudio zima la Usalama huo.

  Kuludi kwenye uhalisia yatakiwa kazi kubwa na yenye umakini na kufuta kabisa aina yote ya mtandao [network] chafu ambayo imekuwa ikitumiwa na MAFISADI ndani na nje ya nchi.

  Hakika ni kwelii makosa yalitokea na hapa JF ndio sehemu pia ya kulekebisha matatizo hayo pia.
   
 5. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Nchi hii ni mali ya watanzania wote,si viongozi!!
   
 6. V

  Vonix JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Ile thread ilikuwa moto na hapo ndipo Pinda na wenzake wanapoivulia kofia jf, Mods wameiondoa au ni mafia wa serikali wameiondoa???? kashfa hiyo hawataweza kuipotezea DR WA UKWELI ATAPELEKEWA nondo airushe mwemba yanga kazi ianze upyaaaa, ccm itadondoka tu na mikashfa kibao. na Shimbo ni mtu wao.kama ilivyokuwa meremeta wabunge wa cdm ivalieni nyuga hii issue sisi tupo bega kwa bega na ninyi.
   
 7. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Sijajua kwa nini watanzania wa kawaida hawafuatlilii mambo makubwa kama haya amabyo yanawaumiza directly. Think of what amount of elctricity we would get if 3 trillions were invested in Stigler's Gorge, certainly 2000 Megawatts. For surprise and great dismay, Tanzanians have become chronic with every impact of squandering our resources. Naogopa kwa utashi huu wa Tanzanian wenzangu. Amid all these man made catastrophes, we are still have and life goes as usual.
   
 8. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kilichofanyika ni uhuni wakunyamazisha watoa maada lakini ujue hata mjinga hufundishika na akawa mzuri ndani ya wajinga wenzake ccm jitadhimini kabla ya kufanya jambo nchi hii itachafuka kama Libya,tunisia, etc sio kama jeshi halikuwepo bali haki ndio inatendeka hata kama utakuwa na jeshi lenyesilaha za aina gani mwisho ni mwisho tu.
   
 9. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Nawashangaa mods sababu niwahi kuchati nao kwenye live text kuhusu watu kutumia majina ya bandia humu jamvini.Nilimwambia jamaa kuwa watu wanaogopa kujulikana kwa sababu wanaweza kufuatiliwa. Jamaa aliponda sana eti watz ni waoga sana hata kama haki yao imevunjwa.

  Mi nilimwambia kwamba watu wako sawa kwa sababu haki zao hazina guarante i.e polisi anaweza kukuua kama mbwa na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa dhidi yake so watu wako sawa kuwa waoga maana hakuna anayependa kufa.

  SASA WAMEKUBALI KUWA TZ INA WENYEWE WENGINE TUPO TUPO TU. KILICHOWAFANYA WAIONDOE ILE THREAD NI WOGA ULEULE WALIOKUWA WANAUPONDA.

  WANAOGOPA JESHI
   
 10. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,047
  Likes Received: 7,506
  Trophy Points: 280
  Binafs siwalaumu Mods kwa hatu waliyochukua, wapo sahii kabisa walichofanya ni kulinda heshima ya hii forums ili baadae waje na taarifa zinazothibitishika.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...